[Back to the Main Page!]

UHURU HATARINI!

Mataifa yanaungana kiuchumi, kisiasa na kijeshi.
Kwa nini yanaungana kidini pia? Litakuwepo tukio gani hivi karibuni?

Kufuatia kushambuliwa kwa Kituo cha Biashara Duniani (World Trade Center) na jumba la pentagon , Marekani imemulikwa zaidi ya wakati mwingine wowote hapo mbeleni. Hapana shaka kuwa kitendo hicho cha kigaindi kilikuwa ni kiovu, lakini pia twaona waziwazi jinsi Marekani inavyotumia fursa hii kuyakusanya mataifa yote ya Dunia dhidi ya adui mmoja. Je, wajua kuwa marekani imebashiriwa kwenye unabii wa biblia? Husema kuwa taifa hili litainuka kwa mfano wa mwana kondoo, lakini kwamba baadaye litaanza kunena kama joka. Ndiyo, Biblia yadhihirisha kuwa taifa lili hili la Marekani ndilo litakaloongoza katika kukiinua kile kiitwacho "mnyama".

Watu wengi watashtuka watakapotambua kuwa Marekani, ijulikanayo kama nchi yenye uhuru wa kuabudu, itazidharau dhamiri za watu na kuwalazimisha kuabudu utawala wa kidini kupitia kwenye sheria za kidini, zitakazotiwa nguvu na serikali (Ufunuo 13:11).

Hivi sasa wanawaadhibu magaidi, lakini biblia yafunua kuwa taifa hili ambalo lafaa kuusimamia uhuru wa Kiprostenti wala sio kuzitilia nguvu sheria za kidini hatimaye litahadaa, kuadhibu na pia kutoa amri ya kifo ili kuwaangamiza wale ambao hawataikubali " samamu ya mnyama na alama ya mnyama"

Wale waliotabiri na kuwaonya watu hapo awali kuhusu matukio haya walichukuliwa kuwa "manabii wa mikosi", lakini tangu Marekani ilipoanza kuwatesa magaidi kote duniani, wengi walianza kuelewa kuwa neno hili `magaidi' litapanuka. Huenda hatimaye hili neno likatumika kuwalenga wale ambao `wenye mamlaka' huwachukulia kuwa "wanamgambo wa Kikristo" yaani wale walioamua kumtiiMungu badala ya binadamu, wakati sheria za watawala ziendapo kinyume na sheria za Mungu.

Hivyo basi swali letu leo ni hili , je , twaweza kuona jinsi Marekani inavyoanza kunena kama joka? Na je, Marekani itatuamrisha katika kila safu ya maisha? Na pia, "Mnyama" ni nani, na "alama" ni nini?

Leo ni dhahiri kuwa kila mmoja atakabiliwa na swala lifuatalo: mtawala wangu ni nani, Mungu au binadamu? Kwa nini? kwa sababu Mungu muumba ametukabidhi sheria fulani, ambazo kwakuzifuata hupatikana furaha maishani. Binadamu ambao ni viongozi wa dunia hii wamefanya uamuzi mwingine tofauti. Hawakumkubali Mungu kama mtawala wao.

Ni katika amri zake kumi ambapo Mungu hujifunua kama mpaji wa sheria, muumba wa mbingu na ardhi. Yeye ndiye tutakayemtii, tutakayemtumikia na kumsimamia . kwa sababu hii, si ajabu kuwa shetani., aitwaye ibilisi, ambaye ndiye adui wa Mungu, amekuwa akijitahidi kuziangamiza amri kumi za Mungu. Ama kwa hakika Biblia imeelezea utawala fulani utakaojaribu kuzibandilisha majira na sheria (Daniel 7:25)Kuambatana na hayo, tutaliuliza swala hili, je, wajua kuwa upapa ndio uliozibandilisha amri kumi za Mungu? katika katekisimu, wameiondoa amri ya pili ambayo hukataza ibada ya sanamu. hali kadhalika wameyatoa maneno karibu yote katika amri inayohusu siku ya pumziko, inayosema kuwa tutaitakasa siku ya saba ya juma, ambayo ni sabato wala sio jumapili, ambayo kwa mujibu wa Bibilia ni siku ya kwanza ya juma. Kwa vile waliondoa mojawapo wa zile amri, zilibakia tisa pekee. Ili kuzipata amri kumi , waligawanya amri ya kumi kuwa vifungu viwili. huu ni undanganyifu usiokubalika (waweza kulinganisha aina hizi mbili za amri kwenye ukurasa wa pili ili kujihakikishia mwenyewe)

Mabandiliko haya ya undanganyifu dhidi ya amri kumi za Mungu yatujulisha kuwa Mungu haheshimiwi kama mtawala na mpaji wa sheria. Hebu tuutazame undanganyifu huu kwa makini, kwani unao undani wake zaidi ya vile wengi wetu tunavyojua.

Mojawapo ya amri zilizobandilishwa na Kanisa Katoliki ni ile inayohusu siku ya pumziko. Amri kamili (ya nne) kwenye biblia kuhusu siku ya pumziko imeandikwa hivi:"Ikumbuke siku ya sabato uitakase. Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote, lakini siku ya saba ni sabato ya Bwana , Mungu wako. siku hiyo usifanye kazi yeyote , wewe , wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako. Maana kwa siku sita Bwana aliifanya mbingu, na nchi ,na bahari, na vyote vilivyomo , akastarehe siku ya saba, kwa hivyo Bwana akaibariki siku ya sabato akaitakasa".Katika amri hii twasoma ya kwamba siku ambayo ni sabato, ndiyo siku ya pumziko. Tukisoma kwa makini tutagundua muhuri wa Mungu katika maneno ya amri hii. Muhuri hushirikisha jina na cheo cha mwenyewe. Hudhihirisha pia mamlaka na milki yake. Mungu ameutia muhuri wake kwenye sheria yake, na huo muhuri hupatikana kwenye amri ya nne. Jina la mwenye sheria ni Bwana, cheo chake ni Muumbaji ( aliyetengeneza ) na milki yake ni mbingu na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo. Lilikuwa ni tendo la hila pale Kanisa Katoliki lilipouondoa huu muhuri kwa kuchapisha amri zingine zenye upungufu na uchuku katika katekisimo yao. Hapa watu hawaelekezwi tena kuelewa ni nani mpaji wa sheria ambaye yawapasa kumtii. Kwa mujibu wa nguvu za kidini na mamlaka waliojitwalia, watu hawa huzibandilisha amri watakavyo:

SHERIA YA MUNGU
ILIVYO KATIKA BIBLIA
KUTOKA 20: 13 - 17

SHERIA YA MUNGU
KAMA ILIVYOBADILISHWA NA
MTU KWENYE KATEKISIMU

1.

Usiwe na miungu mingine ila mimi.

1.

Ni mimi Bwana Mungu wako, usiwe na miungu mingine ila mimi.

2.

Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu chochote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia, usivisujudie wala kuvitumika; kwa kuwa mimi, Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao, nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao na kuzishika amri yangu.

2.

Usilitaje jina la bwana Mungu wako.

3.

Usilitaje bure jina la BWANA, Mungu wako, maana Bwana hatamhesabia kuwa hana hatia mtu alitajaye jina lake bure.

3.

Ikumbuke siku ya sabato ukaitakase.

4.

Ikumbuke siku ya sabato uitakase, siku sita fanya kaza, utende mambo yakoyote, lakini siku ya saba ni sabato ya Bwana, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yoyote, wewe, wala mwana yako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako. Maana kwa siku sita Bwana alifanya mbingu na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba, kwa hivyo Bwana akaibariki siku ya sabato akaitakasa.

4.

Waheshimu baba na mama yako.

5.

Waheshimu baba yako na mama yako, siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na Bwana Mungu wako.

5.

Usiue.

6.

Usiue.

6.

Uzisini.

7.

Usizini.

7.

Usiibe.

8.

Usiibe.

8.

Usimshuhudie jirani yako uongo.

9.

Usimshuhudie jirani yako uongo.

9.

Usimtamani mke wa jirani yako.

10.

Usiitamani nyumba ya jirani yako, usimtamani mke wa jirani yako, wala mtumwa wake, wala mjakazi wake, wala ng'ombo wake, wala punda wake, wala chochote alicho nacho jirani yako.

10.

Usiitamani mali ya jirani yako.

Katika katekisimo ile amri inayoihusu siku ya pumziko imeandikwa hivi "ikumbuke siku ya sabato ukaitakase" katika katekisimo ya Lutheran, twasoma "utaitakasa siku ya pumziko". hapa hatuambiwi ni siku gani hasa ambayo ni ya pumziko, na mpaji wa sheria ni nani.

Kanisa Katoliki hukubali hadharani, waziwazi, kuwa ndilo lililoigeuza siku ya pumziko kuwa Jumapili baadala ya sabato.

Kitabu cha imani ya wa Katoliki wa Kirumi kinasema hivi:

"Swali: Siku ya sabato ni gani? Jibu: Siku ya Sabato ni Jumamosi. Swali: Kwa nini tunaabudu siku ya Jumapili badala ya Jumamosi? Kwa sababu Kanisa Katoliki, katika Balaza la Laodikia (A.D. 336) liliuhamisha utaratibu huu toka Jumamosi hadi Jumapili. Swali: Je, unayo njia nyingine ya kuthibitisha kuwa kanisa (Katoliki ya Kirumi) linao uwezo wa kuzisimamisha sherehe na sheria? Jibu: Kama halingekuwa na huo uwezo, halingelifanya jambo ambalolimekubaliwa na dini zote za kisasa - halingeihamisha ibada hadi Jumapili ambayo ni siku ya kwanza ya juma, kutoka ibada ya Jumamosi, ambayo ndiyo siku ya saba; mabadiliko haya hayakuidhinishwa na Biblia". 3

Ni jambo la kuhuzunisha, lakini la kweli, ya kuwa utawala wa kikanisa umefanya uamuzi ambao ni kinyume cha mafundisho ya biblia.

Waliisimamisha siku ya uongo ya pumziko zama za historia zaidi ya miaka 1000 kabla ya Luther kuzaliwa. hii ndiyo sababu watu wengi hawalijui jambo hili. Je , umearifiwa juu ya jambo hili na makuhani, waalimu wa shule ya Jumapili au waalimu wa kidini wilayani mwako?

Martin Luther, ambaye alilelewa kama Mkatoliki kabla ya kuugundua ukweli kulihusu shirika hili la undanganyifu, alisema: "Ni dhahiri kwamba alama za mpinga Kristo zinalingana na za ufalme wa papa na wafuasi wake". 34 unaweza kuipata taarifa hii kwenye kitabu kitwacho" Concord; the confessions of the Evangelical Lutheran Church. Luther hakukosea hapa, kwani ushahidi wote utokanao na biblia wa kumtabua mpinga Kristo mkuu, yaani -"mnyama" - waingiana na upapa.

Mojawapo ya alama za kumtambua huyu "mnyama" ni kuwa anayo "alama". Katika biblia twasoma hivi; "mtu awaye yote akimsujudu huyo mnyama na sanamu yake, na kuipokea chapa katika kipaji cha uso wake, au katika mkono wake , yeye naye atakunywa katika mvinyo wa ghahabu ya Mungu iliyotengenezwa pasipo kuchanganywa na maji, katika kikombe cha hasira yake; naye atateswa kwa moto wa kiberiti mbele ya malaika watakatifu, na mbele za mwana kondoo" na pia; " Naye awafanya wote, wadogo kwa wa kubwa, na matajiri kwa maskini, na waliohuru kwa watumwa watiwe chapa katika mkono wao wa kuume, au katika vipaji vya nyuso zao, tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza, isipokuwa ana chapa ile , yaani jina la mnyama yule au hesabu ya jina lake". 17 Kwa vile alama zote za Biblia za kumtambua "mnyama" zaingiana na upapa, ishara hii (kuhusu alama) ni lazima pia iingiane na upapa katika taarifa mbalimbali. Kanisa Katoliki huthibilisha kuwa linayo alama fulani. twasoma hivi: "Jumapili ndiyo alama ya mamlaka yetu. Kanisa li juu zaidi ya Biblia, na kuhamisha huku kwa Sabato (hadi Jumapili) ni dhihirisho la ukweli huu".2 Hebu tutazame dondoo lingine; "Bila shaka Kanisa Katoliki hudai kuwa mabadiliko hayo yalitokana nalo …. Na ya kwamba kitendo hicho ni Alama ya mamlaka yake katika mambo ya kidini".5

Ni jambo la kushangaza na la kuhuzunisha kuwa Kanisa la Kilutheri, pamoja na matawi yake yote, limeungana na Wakatoliki katika kuikubali siku bandia ya pumziko na amri bandia zinazopatikana kwenye katekisimu. Wamekubali kuharibiwa kwa amri zilizopeanwa na Mungu. Wale wote wanaoelewa ukweli huu, lakini huzikubali hila hizi, na kukataa kuziachilia, pia wazivunja sheria za Mungu.

Hebu tusikie jinsi waprotestanti kadhaa watakavyosema kuhusu mageuzi haya ya siku ya pumziko:

1. "Ni wapi katika maandiko tunaposhauriwa kuitakasa siku ya kwanza? Tumeamrishwa kuitakasa siku ya saba lakini hapana amri ya kuikumbuka siku ya kwanza"6

2. "Kwa upande mwingine, hakuna amri ya kusherehekea siku ya jumapili katika Agano Jipya. Na bila shaka hamna amri isemayo kuwa Jumapili itachukuliwa kama sabato (Jumamosi ) kwa Mkristo."7

KUFUFUKA KWA YESU

Sasa, mimi naelewa ukweli huu kwamba Wakristo wengi hushikilia ibada ya siku ya kwanza ya juma kama kumbukumbu la kufufuka kwa Yesu. Lakini hata kama mtu ataanza kuisherehekea siku ya ufufuo, ni makosa kuchukulia kuwa jambo hilo latuletea siku nyingine mpya ya pumziko. Maandiko yasema kuwa yesu ndiye Bwana wa sabato.8 Yeye aliumba dunia hii, na ni yeye aliyeisimamisha siku ya pumziko. Imeandikwa pia kuwa "Vitu vyote viliumbwa kwa yeye, na bila yeye hakuna chochote kilichofanyika."9 Yesu ndiye Bwana wa sabato, kwa hivyo kama siku ya pumziko ingehitaji kubandilishwa, Yesu ndiye angaliyafanya hayo. Ni upapa (mnyama) ambao umeyafanya hayo mageuzi.

Biblia yasema kuwa Mungu aliibariki na kuitakasa siku ya saba. Je, waweza kupata katika Biblia mahali ambapo Yesu anatuhimiza tuache kuitakasa siku ya saba, na badala yake kutuamrisha tuikumbuke siku ya kwanza? Je, waweza kupata pahali isemapo kuwa amezigeuza Amri kumi, pamoja na amri ya kutakasa siku ya saba ya sabato, amri ambazo Mungu aliziandika kwa kidole chake mwenyewe? Je, waweza kupata kuwa Mungu au yesu aliitakasa na kuibariki siku ya kwanza ya juma? Kuwa na roho safi na ukayajibu maswali haya. Ni jambo dhahiri kwamba kama isemavyo Biblia, Mungu aliitenga siku ya saba na kuitakasa kwa kusudi fulani. Ni siku ambayo, kwa njia ya kipekee, imetengwa kwa kusudi la kutuburudisha kimwili na kiroho. Ni siku ya kweli, siku ya Bwana kwa ajili yetu.

Mungu alitupa siku ya pumziko kwa sababu anatupenda, na angetaka kutubariki kwa njia ya kipekee kwa kuwepo kwake. Ikiwa tunampenda Mungu, tutataka kubainisha imani na utiifu wetu kwa Mungu kwa kuitakasa siku ya pumziko ambayo yeye mwenyewe aliisimamisha kwa manufaa yetu. Hapo tu ndipo tutakapoipokea mibaraka ya siku ya pumziko.8&10

"Lakini siku ya saba ni gani kulingana na Biblia", huenda utauliza. Kuambatana na kifo, mazishi na ufufuo wa Yesu, Biblia huita siku ambayo Yesu alikufa "siku ya matayarisho" au " siku iliyo kabla ya sabato." Hujulikana leo kama "ijumaa njema." Siku ambayo Yesu alifufuka toka kaburini imetajwa kuwa siku ya kwanza ya juma, au Jumapili kwa lugha ya kisasa. Siku iliyo katikati mwa siku mbili hizi huitwa "sabato" "siku ya saba " Jumamosi Yesu, ambaye ndiye Bwana wa sabato, alipumzika kaburini siku ya Jumamosi, na akafufuka katika siku mpya ya kazi ambayo ndiyo Jumapili. Hivyo basi kulingana na Biblia, Jumapili ndiyo siku ya kwanza baina ya siku zile sita za kazi katika juma, na wafuasi wa Kristo hawana budi kulikubali jambo hili.1&33

Hata baada ya kufufuka kwa Yesu, wanafunzi wake waliendelea kuikumbuka sabato kama siku ya pumziko, ambalo ndilo agano jipya. Kwa vile Yesu ni yule yule jana, leo, na milele, wale wanaodai kuwa ni Wakristo wanafaa hata sasa kuitunza siku takatifu ya pumziko, yaani siku ya saba ya sabato, ambayo ni ya Mungu na Kristo.40

Biblia huielezea sabato kama siku takatifu ya Bwana (soma Isaya 58:13). Hivyo basi; "siku ya Bwana" Sio Jumapili, lakini ni Sabato (Jumamosi) Jumapili (yaani Sunday) lina maana ya "siku ya jua," wala sio siku ya mwana (au son's day)

Baadhi ya nchi zimezipanga upya siku za kutenda huko Norway, jambo hili lilifanywa mnamo Januari 1, 1973, kabla ya tarehe hiyo, Jumamosi ndiyo iliyokuwa siku ya saba kulingana na kalenda. Lakini tangu tarehe hiyo, Jumamosi imefanywa kuwa siku ya sita ya wiki. Jumapili, ambayo hapo mbeleni iliorodheshwa kama siku ya kwanza, sasa husimama kama siku ya saba ya wiki. Hiki ni kitendo cha kupotoa. Watu hufanywa wakadhania kuwa Jumapili ndiyo siku ya saba ya Biblia. Baadhi ya watu hata wameanza kuitaja Jumapili kuwa siku ya sabato. Lakini wale watakao kufanya uchanguzi kidogo watagundua hivi karibuni kuwa Jumapili nsabato bandia. Tangu mwanzo, Jumapili ilikuwa ni siku ya kwanza ya wiki, na kulingana na hesabu ya Biblia, bado siku hii huchukuliwa kuwa ni siku ya kwanza ya kufanya kazi katika wiki.33

Hivyo basi, kwa mujibu wa mabadiliko haya yaliyofanywa kuihusu siku ya pumziko, itatubidi kufanya uamuzi. Je, tungetaka kumtii Mungu kwa kuitunza siku ya sabato yake takatifu iliyo ya dhamani, au tutamtii binadamu kwa kuitunza Jumapili?

WACHUNGAJI BANDIA

Yamkini washangaa ni kwa nini wahubiri wamekuwa wamelinyazia jambo hili linalohusu kugeuzwa kwa amri kumi? Yawezekana kuwa baadhi yao bado hawayagundua mabadiliko haya, lakini jawabu rahisi ni kwamba wengiwao wamekuwa wakimwakilisha Mungu kwa hila, hivyo basi huwaficha watu ukweli kuhusu "alama ya mnyama" Husema kuwa "sabato ilitengenezewa wayahudi", na kuwa "sisi twaishi chini ya agano jipya", kwa hivyo "Jumapili ndiyo siku ya pumziko", lakini hebu fikiria mwenyewe! Sabato ilikuwepo haya kabla ya Myahudi wa kwanza ambaye ndiye Ibrahim kuwepo. Sabato ilisimamishwa hapo mwanzo, wakati wa uumbaji, na Yesu mwenyewe husema kuwa "iliumbwa kwa ajili ya mwanadamu."8 Iliumbwa mradi tu tutaendelea kuliona mbingu juu yetu na nchi chini yetu, amri za Mungu zitokuwa halali.11 Amri kumi za Mungu ni halali hata leo wakati wa agano jipya. Lakini tofauti iliyotokea baada ya agano la kale ni kuwa sasa katika agano jipya, twasema kumjia Yesu moja kwa moja ili kupata msamalia wa dhambi zetu, bila kutoa kafara ya mwana kondoo. Ule mfumo wa kutoa sadaka za kafara umeondolewa, umefikia utimilifu katika Kristo. Yesu amekuja kama mwana kondoo wa kutolewa kafara aliye wa kweli, na ametolewa kafara mara moja tu hata milele.12

Hata ikiwa tunalijadili swala hili kuhusu amri ya sabato kwa undani zaidi katika kikaratasi hiki, twaelewa pia ya kuwa amri zingine zote ni muhimu.Biblia husema kuwa "yeyote atakaye ishika sheria yote, ila akajikwaa katika neno moja,amekosa juu ya yote.20 Ukweli huu ni muhimu wa kutafakari kwa wasabato, kwa wale wanaopinga utoaji wa miba, hali kadhalika wale wote ambao huwa na juhudi za kuwakilisha amri moja ya kipekee.

HARAKATI ZA KUIPENDEZA JUMAPILI

Harakati za kuipendeza Jumapili hivi sasa zapamba moto duniani kote. Kunavyo vikundi vya kidini huko Marekani, kama vile " muungano wa siku ya Bwana, " " kongamano la Kikristo ," na vinginevyo, ambavyo hufanya juu chini hadi vihakikishe ya kuwa Jumapili imesimamishwa kama siku ya pumziko kwa mataifa yote. Kwa sababu ya utovu wa tabia, hali ya kiuchumi yenye kutisha, hali kadhalika kupungua kwa hamu ya Ukristo, wanaharakati hawa wanaamini ya kuwa ni lazima watu na taifa kwa jumla wazirudie Amri kumi iliwapate baraka za Mungu. Ni kwa njia hii wanatarajia kuirejesha ile siku bandia ya pumziko.

Leo hii twaona maaskofu na makasisi wakishikana na miungano ya kikristo, pamoja na ulimwengu wa kibiashara, vyama vya wafanyi kazi na mashirika mengineo, ili kuipatia uhai Jumapili kama siku ya pumziko. Wanajarabu kuhuisha alama ya mnyama.

Katika umoja wa Uropa (EU), wanajitahidi kuifanya Jumapili siku ya pamoja ya pumziko. Jaques Dolors , Mkatoliki ambaye alikuwa rais wa umoja wa Uropa hapo awali anatoa mwito kuwe na " roho moja, wazo moja na hali moja ya kiroho katika mashirika yote ya Uropa3 wanaendelea kujenga juu ya msingi huu, na wanafikiria kuwa jumapili, kama siku ya pumziko, itawafunganisha wote katika hali moja ya kiroho. Wanajaribu kuzitafuta sehemu za imani ambazo hukubalika na wote katika umoja huo, na ni wazi kuwa swala la jumapili kama siku ya pumziko ni jambo ambalo wakatoliki na waprotestanti wanaweza kukubaliana kwa pamoja. Hu ni mkutaniko wa hila kwa upande wa wakatoliki kwani ukweli ni kwamba harakati hizi za kuinua Jumapili ni juhudi za ukatoliki ili kuitia nguvu ile alama yao ya mamlaka (yaani Jumapili) dhidi ya mataifa yote.

SHURUTISHO LA KUTUNZA JUMAPILI

Leo hii mataifa ya kikatoliki na ya Kiprotestanti yanazo sheria za kuikazia Jumapili katika katiba zao, japokuwa hazitekelezwi. Wakati sheria hizi zitaanza kutiliwa mkazo kwa kutumia nguvu, basi litakuwa ni jambo la lazima kuitunza Jumapili kama siku ya kustarehe. Hapo ndipo unabii wa "alama ya mnyama" utakapotimia

Biblia yasema kuwa hatimaye, dunia yote itavutwa kwenye vita hivi vikuu vya mwisho. Itatubidi kuchagua baina ya kumuabudu Mungu na kumheshimu kama muumba wa mbingu na nchi kwa kuitakasa siku ya Mungu na ya Yesu ya pumziko ambayo ni sabato au kumsujudu "mnyama" (yaani upapa) na kuichukua alama yake, ambayo ni Jumapili. Wote wampendao mwokozi na waliojazwa na Roho mtakatifu watadhihirishwa msimamo wao kwa Mungu kwa kuitunza sheria yake. Watakataa kuikubali sabato bandia, na watasimama chini ya bendera ya Bwana. Hao ndio watakaopokea muhuri wa Mungu aliye hai.39

Wale wanaouachilia ukweli utokao mbinguni na kuikubali Jumapili kama sabato, watapokea alama ya mnyama.

Watakaoamua kupokea alama ya mnyama wataipokea alama hiyo kwenye vipaji vya nyuso zao (kudhihirisha uamuzi ufanyikao kwenye mawazo) au waipokee katika mikono yao ya kuume (kudhihirisha vitendo au nguvu zao35) Lakini hapana yeyote (kama ilivyotajwa hapo awali) alakayezihisi hasira za Mungu dhidi ya mvunjaji wa sheria hadi apate kuletewa huo ukweli katika mawazo na hisia zake, na kisha kuukataa.

Japo kuwa vita kuhusu swala la Jumapili na sabato vimbele, uamuzi wa kuwa mwaminifu wafanyika leo. Kwa vile twajua ukweli kuhusu uvunjaji wa sheria za Mungu na aganola udanganyifu lililofanyika kuhusu siku ya pumziko, ni jambo la muhimu kwetu sisi kwa wakati huu tusimame imara dhidi ya sabao bandia. Yatupasa kuchagua kuzifuata nyayo za Yesu sasa, na yeye mwenyewe alitunza siku ya saba ya juma tangu jua kutua ijumaa hadi jua kutua Jumamosi.1&33

Twaamini kuwa kunao watu waaminifu na wasio na hatia katika madhehebu mbalimbali, hata kwenye kanisa katoliki. Pale watu hawa binafsi watakapogundua undanganyifu huu unaozihusu amri kumi za Mungu, hasa amri ya sabato baadhi yao wataupinga huo undanganyifu watazikata kamba zinazowafunga, na wawe vifaa vyenye nguvu vya kutumiwa na Mungu katika kuifunga kazi nyakati za mwisho.

Wakati ambapo twawafunulia yale yaliyotendeka kwenye kikaratasi hiki, jinsi kanisa katoliki lilivyosababisha wabadiliko haya, watu wahukumu waumini wa kikatoliki kama waumini binafsi bali twawaangazia na kuwazaidia wao na sisi zote kwa jumla, ili tuweze kuafikia uamuzi bara kuhusu swala hili.

UMOJA WA UROPA NA WA ULIMWENGU

Biblia hutufunulia kuwa viongozi wa dunia hii wataungana muda mfupi kabla ya kurudi kwake Yesu kristo, aliye mwokozi wetu.15 Leo twauona utangulizi wa muungano huu. Watawala wa dunia hii kwenye mashiraka yao ya siri wanaiandaa mielekeo ambayo itatengeneza njia ya kuungana kwa Uropa na ulimwengu uliosalia chini ya utawala wenye maarifa na mfumo wao wa sheria za kimataifa

Twauona umoja huu kupitia kwenye mashirika kama vile EEC, EU, CATT, NATO, Umoja Wa Uropa Ya magharibi, UN, na leo twauona pia kupitia kwenye Mpangilio Mpya wa Ulimwengu, ambao George Bush alikuwa akiutajaa mara kwa mara wakati wa vita vya Guba, ambao pia watawala wote wa dunia wanauunga mkono.

Kwa kweli, Uropa itayari kuungana na ulimwengu uliosalia kiuchumi, kisiasa na kidini, na Biblia yafunua kwani "yule kahaba" (yaani kanisa katoliki) ambaye anauendesha mpango huu. Imeandikwa kwenye neno la Mungu, ya kuwa wafalme wa dunia watafanya washerati na kahaba yule. Wanabiashara na watu wote waliosifika duniani wafanya biashara na huo wa kibiashara. Wamelewa na mvinyo wake, na kupumbazwa na huo uchawi wa kipapa.16

Wakati huu twaona jinsi utendaji wa miujiza (kupitia kwenye kizazi kipya au new age) unaunganisha ukatoliki na Uprotestanti. Kuhusu huu muungano baina ya Ukatoliki na Uprotestanti, ni waprotestanti ambao wanaziacha imani zao na kuelekea polepole kwenye Azimio la Porvoo, Azimio la pamoja, ushirikiano wa makanisa makubwa, kwenye taratibu na tamaduni za kanisa, hali kadhalika kwenye mipango iliyopo ya kuwaelimisha watoto na vijana wetu, na kwengineko serikari pia huchangia pale inapozisukumia mbele hisia hizi ambazo hugongana na sera za Kiprotestanti.

WANALO WAZO MOJA

Tuko kwenye ufuo wa mng'ang'ano ukuu na wa kukamilisha hapa duniani biblia husema! "wafalme wa dunia wanajipanga, na wakuu wanafanya shauri pamoja,juu ya Bwana na juu ya masihi wake."16

Biblia pia husema kuwa watawala wa ulimwengu "wanalo wazo moja, na watamkabidhi mnyama uwezo wao na nguvu zao"18 maelezo yanayodhihirisha waziwazi nguvu na umoja uliyopo kwenye mtukutiko huu. "Utakuwepo ufungamano wa kimataifa utangamano mkuu, ushirikiano wa majeshi ya ibilisi." Katika vita vitakavyopiganwa siku za mwisho, nguvu zote potovu, ambazo hazionyeshi utiifu kwa sheria ya Mungu, zitaungana ili kumpinga Kristo pamoja na walewanaosimama upande wake",19 "wale wazishikao amri za Mungu, na ushahuda wa Yesu".29 Kanisa litapokea usaidizi kutoka kwa serikari. Watashauriana pamoja na kuungana ili kuitilia nguvu na kuinua siku bandia ya kustarehe ya upapa yaani Jumapili iliyo kinyume na siku ya pumziko iliyohalalishwa na Biblia.

Amri ya nne ya Biblia yaani amri ya sabato, itakuwa ni swala nyeti, kwa vile ndani yake mtengenezaji wa sheria amejitambulisha kuwa muumbaji wa mbingu na nchi.19

Je, unayo mashaka kuhusu matokeo yake? Yesu anasema, "nimepewa mamlaka yote mbinguni na dunia."21 Mungu na Kristo ndio wanaoshika usukani. Shetani, aliyemwasi Mungu huko mbinguni na hatimaye kurushwa hapa duniani, amepewa nafasi ili authibilishe mfumo wa serikali yake anayoipendekeza Mungu ni upendo, hamshurutishi yeyote awe ni shetani au sisi, lakini hatuachilia ili tuchague kati ya mema na maovu, uhai na kifo. Hivi karibuni, pambano hili litakwisha, na biblia yatujulisha matokeo yake. "Hawa (yaani mamlaka yote ya dunia yaliyopotoka) watafanya vita dhidi ya mwana kondoo, naye mwana kondoo atawashinda.18 "Ni Yesu Kristo aliye mwokozi wa ulimwengu , Bwana wa mabwana na mfalme wa wafalme, pamoja na wale waliochagua kuwa upande wake ambao watashinda katika pambano hili baina ya mema na maovu, kati ya Kristo na shetani. Je, wewe utasimama upande gani?

MAANDALIZI

Katika pambano hili lote, yatupasa tukumbuke kuwa karama ya wokovu na uzima wa milele ipo kwa kila mmoja. Yesu anasema, "kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa mwanawe wa pekee, ili yeyote amwaminiye asipotee,bali awe na uzima wa milele"23 kwa hivyo ni juu yako na mimi kama tutaipokea zawadi hii ya wokovu. Hakuna njia nyingine ya kuokolewa kwani Yesu anatangaza. " mimi ndiye njia , ukweli na uzima mtu haji kwa baba ila kwa njia ya mimi."23

Hebu na tufanye kama alivyofanya yule mwana mpotevu, alyekuwa ametanga mbali na nyumbani. Kwanza alifikiria kuwa ilimpasa kwenda nyumbani mwa babake. Lakini hilo halikutosha ni pale tu alipotenda kulingana na mawazo haya pale aliposimama na kwenda, ndipo alipokuja nyumbani.

Kama vile baba yake alivyomtambua kwa mbali na kumkimbilia, kisha kumkubali kila amjiaye kwa imani.24 Yesu anasema, "yeyote ajaye kwangu sitamtupa nje kamwe."24

Sasa swali la kibinafsi lajitokeza ambalo ni hili , Je, ungependa kuipokea zawadi hii ya wokovu, na ukaseme ndiyo kwa Yesu.

Ishara za nyakati zadhihirisha kuwa kurudi kwa Yesu Kristo ku karibu. Kwa hivyo sasa uamuzi wetu kusimama upande wake ni jambo la muhimu sana. Yesu atakaporudi, hadi kutuokoa kutoka kwa dhambi zetu au kuyaosha mawazo yetu ili kuziondoa taka zote. La, kusafishwa huku hufanyika kabla ya kurudi kwa Yesu. Ni kwa jinsi hiyo tu ambayo twaweza kukubaliwa naye pale arudipo kuwakusanya watu wake.26

Pengine unauliza ni nini maana yake kusema ndiyo kwa Yesu na kujitia katika upande wake? Kwa kinagaubaga, jawabu ni hili.

Biblia yasema kuwa "wote wameasi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu" "dhambi ni uasi" na "mshahara wa dhambi ni mauti"27 kwa hivyo tangu mwanzo sisi zote tu katika hali ya kupotea.

Tukiwa katika hali hii, Yesu anatukabidhi neema na wokovu wake. Mungu anatutafuta. Hataki tupotee kwa hivyo alimtuma mwanawe afe badalayetu sisi, ili "yeyote amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele"23

Roho mtakatifu anatuita tujinyenyekeze, tutubu, tugeuke kutoka dhambini na kufanya mapenzi ya Mungu. Tukiukubali mwito huu, tutajua ya kwamba ameahidi kutusamehe dhambi zetu kupitia kwa nguvu za damu yake. Hatimaye tutasimama kwa wasafi mbele za Mungu, huku tumevikwa kanzu ya haki ya Yesu, japo hatufai, lakini kwa njia ya neema kupitia kwa imani.28&29

Mara tu mtu asikiapo injili ya Yesu Kristo, na kwa imani kumkubali Yesu kama mwokozi wake binafsi, basi huwa wakati wake umewadia kubatizwa. Kwa Biblia kufanya kwa kutumbukizwa majini. Anayebatizwa hutubukizwa majini ; ishara inayoonyesha kuwa dhambi zake huzikwa majini, naye mwenye kubatizwa kuinuka toka majini huku akiwa na maisha mapya pamoja na Kristo. Pia humaanisha kuwa kwa kitendo hiki chenye ishara, wayashuhudia yale yaliyotendeka moyoni mwako, ya kuwa sasa waamini kuwa Yesu alikufa, akazikwa na kufufuka toka kaburini kwa ajili yako.36 Yesu mwenyewe alibatizwa kwa njia hii ( japokuwa hapakuwa na haja , kwani hakuwa na dhambi) lakini alifanya hivi kama kielelezo kwetu, ili tuzifuate nyayo zake.37 Tunapoamua kumfuata Yesu kabisa, kwa moyo wote, baada ya kubatizwa kwa namna hii, basi tumeahidiwa ya kwamba Yesu atatupa Roho

mtakatifu. Roho mtakatifu basi ni uwezo katika maisha ya Mkristo unao tuwezesha kuyakataa majaribu yanayotukabili.38

Yesu anapoingilia maisha ya muumini, tabia hubadilika, litakuwa jambo la Kufurahia kuubeba msalaba na kumfuata Yesu Kristo. Kwa msaada wa Rohomtakatifu, utaziacha anasa za ulimwengu. Kwa huo huo msaada wa Roho mtakatifu, utayashika mawazo yote mateka na kuyatiisha. Kwa neema na msaada wa Mungu, utamfuata na kumtii Roho wala sio mwili. Kwa msaada wa Roho mtakatifu, utaisafisha roho yako ili iweze kutii ukweli, na pale Utakapogundua kuwa siku ya saba ndiyo siku ya Yesu ya Kustarehe, na kuwa Mungu aliitakaza na kuibariki, hapo utazifuata nyayo za Kristo ka kumfurahia na kumpenda - katika jambo hili pia.29

Roho mtakatifu anapoanza kuyatawala maisha ya muumini, yeye atakuwa hana budi kuutawanya mwangaza kwa ukweli kwa wengine huku akishangilia. Yesu ndiye mwajili. Naye asema hivi: "Enendeni basi, mkawafundishe mataifa yote."Je, utaikubali changamoto hii?

Ndani ya kikaratasi hiki, tungalipenda kumuinua Kristo kama mwokozi. Hata hivyo tutawaonya _ japo kwa upendo _ dhidi ya "mnyama" na "alama ya mnyama." Dunia kwa hakika yahitaji ujumbe wa maonyo na ujumbe wa wokovu, kama unavyopatikana katika Ufunuo 14 : 1-12, na ufunuo 18:1-4.30 Dunia yangojea kwa hamu kuiona imani na tabia ya Yesu maishani mwa muumini, na kuusikia ujumbe wa wokovu toka dhambini ukihubiriwa kwa usafi. Yesu alikuja duniani ili kuwaokoa watu kutoka dhambini, bali sio ndani ya dhambi zao. Yesu alikuwa mmoja na baba. Alikuwa Mungu. Alikuwa muumbaji. Pale Yesu alipokuja kuwaokoa binadamu kutoka dhambini, aliuvika ubinadamu juu ya uungu wake. Kwa muda wa miaka 4000, binadamu walikuwa wakizorota katika nguvu za kimwili, kimawazo na kitabia; hata hivyo Kristo alijivika unyonge huo wa binadamu waliozoroteka. Alijaribiwa kwa kila namna kama vile sisi, hata hivyo hakutenda dhambi. Ilimpasa kuzipokea nguvu na uwezo kutoka kwa Mungu ili aweze kuishi maisha yasiyo na dhambi. Sisi pia twaweza kuupokea uwezo na nguvu kwa kila jaribu ili tuishi maisha yasiyo na dhambi. Kama vile tawi halina budi kushikamana na mti ili kuishi na kuzaa matunda, vivyo hivyo sisi pia yatupasa kushikamana na Yesu kila wakati ili tusitende dhambi. Tukitenda dhambi basi ni sisi tuliofeli, sio Yesu.31

Hebu na tufuatilie kuyatenda mapenzi ya Mungu kila wakati, na pia kuyaelekeza mawazo yetu mbinguni. Hapo tutaendelea toka ushindi, hadi ushindi katika maisha yetu ya Ukristo, katika vita vikuu vya mwisho, wale wazitunzao amri za Mungu na walio na imani ya Yesu, hawataipokea alama ya mnyama, lakini- kwa neema za Mungu - wataupokea muhuri wa Mungu.17&39 Ombi langu ni kwamba wewe na mimi tuwe tayari wakati wowote. Ndiposa Yesu Kristo ambaye ndiye mwokozi wa dunia hii, atakaporudi na malaika wake ili kuwakusanya waaminifu wake, twende na yeye hadi kwenye mji wa nuru ulio juu mbinguni, ambao amewatayarishia wale wampendao na kumtii.32 Twatarajia kukutana na wewe huko!

Wanaojabika kukihusu kikaratasi hiki ni Christian Information Service, Bente na Abel Struksness Solberg, 3522 Bjoneroa, Norway.


Marejeo:

1. Luka 4:16, Luka 23:54-56
2. "Catholic Record" London/Ontano, Sept. 1, 1923
3. "Doctrinal Catechism", P. 147 na "Converts catechism ya mafundisho ya Kikristo" (1977 Edition) Page 50
5. H. F. Thomas, Chancellor wa kadinali Gibbons
6. Isaac Williams "Plain sermons on the catechism" P. 334, 336
7. Catechims note (22) "sabbath og sondagen" by Odd Sverre Hove. The norwegion newspaper "Dagen" Oktoba 7, 1995.
8. Marko 2:27, 28
9. Yohana 1:1-3, Mwanzo 1:26
10. Mwanzo 2:1-3, Kutoka 20:11, 1 Yohana 5:3
11. Mathayo 5:17,18
12. Waebrania 9:24-28
13. "dagen" Septemba 29, 1992
14. 1 Yohana 2:1-2, Wafilipi 2:5-7 na Yohana 14:4-6
15. Zaburi 2:2, Ufunuo 17:12-13, Ufunuo 16:13-14
16. Ufunuo Sura 17 na 18
17. Ufunuo 13:16-17 na Ufunuo 14:9-10.
18. Ufunuo 17:12-14
19. Ellen G. White: Review and Herald Oktoba 13, 1904, Ufunuo 14:12
20. Ufunuo 14:12, Yakobo 2:10-12
21. Mathayo 28:18-20
22. The Norwegian Newspaper "Vartland" Septemba 12, 1990 "Daggen" April 6 1995
23. Yohana 3:16; 14:6, 1 Yohana 6:37
24. Luka 15:17-20 na Yohana 6:37
26. Mathayo 1:21 na Ufunuo 21:27
27. Warumi 3:23; 6:23 na 1 Yohana 3:4
28. Matendo 2:38, Waefeso 2:8-10
29. 1 Wakorintho 10:13 1 Yohana 3:1-9, 1 Yohana 2:1-6 na Warumi 8:10 1 Yohana 5:2-3, 2 Wakorintho 3:16, 1 Petero 1:22
30. Ufunuo 14:1-12 na 18:1-4
31. Yohana 1:1-3,14, Warumi 8:3, Waebrania 4:15, Yohana 17:21-23;5:30;14;3-4, I Yohana 3:3-10, 2 Petero 1:4; 1 Yohana 2:1-2.
32. 1 Wathesalonike 4:15-17, Ufunuo 22:12
33. Mambo ya Walawi 23:32, Nehemia 13:16-21
34. The Book of concord; the confessions of the Evangelical Lutheran Church, Page 327.
35. Kumbukumbu 6:6-8, Waebrania 10:16
36. Warumi 6:3-5, 1 Petero 3:21, Yohana 3:23
37. Mathayo 3:13-17, 1 Petero 2:21
38. Matendo 2:38, Matendo 5:32
39. Ufunuo 7:1-4, Ezekieli 9:4, Ufunuo 15:2; 14:1-5
40. Matendo 16:11-13, 18:4-1, Waebrania 13:8.


[Back to the Main Page!]


This page belongs to Abel Struksnes. For more information contact Christian Information Service, Bente & Abel Struksnes, Vestrumsbygda 26, 2879 Odnes, Norway or send me an e-mail at abels@online.no