[Back to the Main Page!]

MFALME YUAJA

Misiba na Masikitiko ya Nguvu za Asili

Ajali na majanga ya angani, baharini na nchi kavu, mioto mikubwa, vimbunga, mvua ya dhoruba itishayo, tufani, sunami, matetemeko ya nchi, mimea kushindwa kukua, njaa, mapigo ya maafa, magonjwa ya kuambukizana kati ya wanadamu na wanyama, ongezeko la usherati, ukahaba, kudhulumiwa kwa mambo ya kimapenzi, mauaji, vita na matetesi ya vita. Je, mbona haya yote yanaendelea? `Lakini ufahamu neno hili ya kuwa siku za mwisho kutakuwako nyakati za hatari maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kutukana, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio safi, wasiojizuia, wakali, wasiopenda mema, wasaliti, wakaidi wenye kujivuna, wapendao anasa kuliko kumpenda Mungu; (II Timotheo 3:1-5) Wenye mfano wa utauwa, lakini wakikana nguvu zake, hao nao ujiepusha nao.

Mipaka ya nchi inaondolewa, mataifa ya ulimwengu yakiwepo ya Yuropa, yanaungana. Makampuni makubwa, mabenki, sehemu za hifadhi na kadhalika zinaungana, zikiwa mashirika makubwa yenye nguvu. Matajiri wanazidi kuwa matajiri zaidi na masikini wanazidi kudidimia katika umaskini. Maskini wanafanywa watumwa kutokana na mipangilio na mikataba iliowekwa na wasomi. Miji mikubwa na elimu ya kiteknolojia, jamii inayoongozwa na mipangilio ya kompyuta waifanya ulimwengu kutawaliwa nayo.

Hizi zote ni dalili za nyakati. Haya yote yalitabiliwa yatafanyika muda mfupi tu kabla ya mfalme wa wafalme Yesu Kristo, mwokozi wa ulimwengu kurejea mara ya pili.

Kwa hivyo, Yesu atarudi wakati gani, na ni kwa njia gani atakapoonekana? Ni akina nani wakataokolewa na watakaopotea? Siku sijazo zitakuwa za namna gani? Haya, na maswali mengine yatafafanuliwa ndani ya kijitabu hiki.

Kunyakuliwa

Wengi hufundisha kutakuwa na kunyakuliwa kwa siri, na mamilioni ya watu wote duniani watatoweka na wanyakuliwe hadi mbinguni kabla ya nyakati za taabu kuu haijaanza. Wengine wataachwa nyuma. Hata hivyo Biblia husema nini kuhusu haya?

`Kwa maana kama vile ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake mwana wa Adamu. Kwa kuwa kama vile siku zile zilizokuwa kabla ya gharika watu walikuwa wakila na kunywa, wakioa na kuolewa, hata siku ile aliyoingia Nuhu katika safina, wasitambue, hata gharika ikaja, ikawachukua wote, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake mwana wa Adamu. Wakati ule, watu wawili watakuwako kondeni, mmoja atatwaliwa, mmoja ataachwa. Kesheni basi, kwa maana hamjui ni siku ipi atakayokuja Bwana wenu'. (Mathayo 24:37-42).

Fungu hili likitoka kinywani mwa Yesu, hutuambia tu ni siku ile Yesu atarejea, ya kwamba wengine watanyakuliwa ili hali wengine wataachwa nyuma. Ni wakali huo tu, wakati wa marejeo ya Kristo, ndipo kunyakuliwa kutakuwa tukio la hakika. Mafungo mengine mawili yathibitisha haya. `Ndipo itakaponekana ishara yake Mwana wa Adamu mbinguni; ndipo mataifa yote ya ulimwengu watakapoomboleza, nao watamwona mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya mbinguni pamoja na nguvu na utukufu mwingi. Naye atawatuma malaika wake pamoja na sauti kuu ya paraparanda, (Mathayo 24:30-31) nao watawakusanya wateule wake toka pepo nne toka mwisho huu wa mbingu mpaka mwisho huu.

`Lakini, ndugu, hatutaki msijue habari za hao waliolala mauti, msije mkahuzunika kama na wengine wasio na matumaini. Maana ikiwa twaamini ya kwamba Yesu alikufa akafufuka vivyo hivyo na hao waliolala katika Yesu, Mungu atawaleta pamoja naye. Kwa kuwa twawaambieni haya kwa neno la Bwana, kwamba sisi tulio hai, tutakaosalia hata wakati wa kuja kwake Bwana, hakika hatutawatangulia wao waliokwisha kulala mauti. Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na paraparanda ya Mungu, nao waliokufa katika kristo watafufuliwa kwanza; Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele'. (1Wathesalonike 4:13-17)

Mafungu haya hutoa maelezo kuwa kunyakuliwa kutafanyika tu Yesu atakapowakusanya wateule wake. Kwa kweli maandiko hulenga wale watakaoishi duniani wakati wa marejeo ya pili, hawatanyakuliwa kabla ya ufufuo wa waliokufa. Ni wakati huo tu, kwa wale waliokufa wakimwamini kristo, watafufuliwa tena kuungana pamoja na wateule wataokuwa hai katika dunia. Mafundisho ya watu kunyakuliwa kisiri kabla ya marejeo ya yesu kristo hayana msingi katika mafundisho ya Biblia.

Leo wengi huamini Yesu atashuka mara moja zaidi katika sayari na kuketi katika kiti cha enzi cha Daudi katika Yerusalemu. Ndiposa Wayaudi wanadhaniwa watakuwa wanenaji wa Mungu, wakiwahubiria wale ambao hawakuokolewa kwa muda wa miaka elfu moja. Fundisho hili, nalo pia halipo katika maandiko. Kwa kweli ni udanganyifu! Baada ya haya yote Yesu mwenyewe aliweka wazi ya kwamba ufalme wake sio wa ulimwengu huu (Yohana 18:36). Tena, na tena, tumeweza kusoma wakati Yesu atakaporudi, kesi zote zitakuwa zimeamuliwa. Ndiposa itakuwa imejulikana ni nani ameokolewa na nani atakayepotea. Hakutakuwa na kipindi cha rehema. Ni sasa wakati wakupata kipawa cha wokovu au tukatae. Yesu atakaporudi, tutakuwa tumekwisha chelewa kubadilisha mawazo yetu.

Fungu hili tulilolisoma (1 Wathesalonike 4:13-17) pia hutufundisha ya kwamba Yesu hatakanyaga nchi. Pia linasema, waliookolewa watachukuliwa ama kunyakuliwa hadi mawinguni. Watakutana na Yesu mawinguni, wakiandamana naye pamoja na malaika wake Mungu.

Hadi Mbinguni

Yeyote asiwe na shaka ya kwamba waliookolewa hawataenda mbinguni. Ufunuo 4: inasema kiti cha enzi cha Mungu na Kristo kiko mbinguni. Tukisoma zaidi, waliookolewa walionekana wamesimama mbele ya kiti cha enzi huko mbinguni (Ufunuo 7:9). Tukiendelea zaidi katika ufunuo tunasoma kuhuszu waliookolewa wakiwa katika makao ya Mungu katika ufalme wake. Inasema, `kisha nikaona ishara nyingine katika mbingu, iliyokubwa na ya ajabu malaika saba wenye mapigo saba ya mwisho; maana katika hayo ghadhabu ya Mungu imetimia. "Tena nikaona kitu kama mfano wa bahari ya kioo iliyochangamana na moto, na wale wenye kushinda watokao kwa yule mnyama na sanamu yake na kwa hesabu ya jina lake, walikuwa wamesimama kando_kando ya hiyo bahari ya kioo wenye vinubi vya Mungu" (Ufunuo 15:1-2)

Muda mfupi kabla ya kuenda mbinguni, Yesu aliwaambia wanafunzi wake `Nyumbani mwa Baba yangu mnao makao mengi; kama sivyo ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali. Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu ili nilipo mimi, nanyi mwepo (Johana 14-2-3).

Katika hotuba ya kuagana, aliweza kuyasema haya kwa wanafunzi wake `lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu huyo roho mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote na Samaria na hata mwisho wa nchi. Akiisha kusema hayo, walipokuwa wakitazama, akainuliwa juu, wingu likampokea kutoka machoni pao. Walipokuwa wakikaza macho mbinguni yeye alipokuwa akienda zake, tazama watu wawili wakasimama karibu nao, wenye nguo nyeupe, wakisema enyi, watu wa Galilaya, mbona mmesimama mkitazama mbinguni? Huyu Yesu aliyechukuliwa kutoka kwenu kwenda juu mbinguni; atakuja jinsi hiyo hiyo mlivyomwona akienda zake mbinguni' (Matendo ya mitume 1:8-11)

Maandiko haya, yamekusanywa pamoja, kuonyesha wazi ya kwamba, watachukuliwa na kunyakuliwa hadi mbinguni. Mbinguni ni makao ya Baba yetu ambayo wamfuatao Yesu wanayatazamia kuenda. Paulo akiwaandikia mashujaa wa imani, akathibitisha haya `Hawa wote wakafa katika imani, wasijazipokea zile ahadi, bali wakiziona tokea mbali na kuzishangilia, na kukiri ya kwamba walikuwa wageni na wasafiri juu ya nchi. Maana hao wasemao maneno kama hayo waonyesha wazi kwamba wanatafuta nchi yao wenyewe. Na kama wangalikumbuka nchi ile waliyotoka, wangalipata nafasi ya kurejea. Lakini sasa waitamani nchi iliyo bora, yaani ya mbinguni. Kwa hiyo Mungu haoni haya kuitwa Mungu wao; maana amewatengenezea mji' (Waibirania 11:13-16)

Dhiki Kuu kabla ya marejeo ya pili

Bibilia huweka wazi ya kwamba, muda mfupi tu kabla ya Yesu kurejea, watu wote watajaribiwa; kama ni kumuabudu Mungu muumbaji au kuabudu mnyama na kupokea `alama yake' (Ufunuo 14:6-12) wengine huonelea ya kwamba nyakati za taabu zitakazoletwa na alama ya mnyama, zitakuwa baada ya kunyakuliwa. Hata hivyo Biblia huthibitisha watakatifu wakiwa katika makao katika ufalme wa Mungu, walishinda vita dhidi ya kile ambacho biblia hutaja kama sanamu ya mnyama na alama ya mnyama. Yohana asema hivi `kisha nikaona viti vya enzi, wakaketi juu yake nao wakipewa hukumu; nami nikaona roho zao waliokatwa vichwa kwa ajili ya neno ya ushuhuda wa Yesu na kwa ajili ya neno la Mungu na hao wasiomsujudia yule mnyama, wala sanamu yake wala hawakuipokea ile chapa katika vipaji vya nguso zao wala katika mikono yao; nao wakawa hai, wakatawala pamoja na Kristo miaka elfu'. (Ufunuo 20:4).

Waliookolewa kupitia nguvu za mwana kondoo (Kristo) walipata ushindi dhidi ya mnyama na sanamu yake pamoja na alama yake, kwa hivyo wale watakaoishi kabla ya marejeo ya pili watakuwa wamepitia kipindi cha dhiki kuu. Kwa nini Bibilia inasema "wote" matajiri. `Akapewa kutia pumzi katika ile sanamu ya mnyama, hata ile sanamu ya mnyama inene, na kuwafanya hao wote wasiosujudu sanamu ya mnyama wauawe. Naye awafanya wote, wadogo kwa wakubwa na matajiri kwa maskini na walio huru kwa watumwa, watiwe chapa katika mkono wao wa kuume, au katika vipaji vya nyuso zao; tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza, isipokuwa ana chapa ile yaani jina la mnyama yule au hesabu ya jina lake. Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na akili na aihesabu hesabu ya mnyama huyo, maana ni hesabu ya kibinadamu. Na hesabu yake ni mia sita sitini na sita'. (Ufunuo 13:15-18)

Jifunze zaidi katika maelezo makubwa katika kijitabu kilichotangazwa. Kumwabudu Mungu kama muumbaji au mnyama na kupokea alama, litakuwa jaribio kuu la mwisho, kabla ya marejeo ya Kristo. Huu ndio wakati wa kuamua kwa kusema `ndio' kwa Yesu. Naye atatupea msaada unaoitajika na uzoefu, tena atatusaidia katika magumu yaliyo mbele yetu. Atatupa nguvu na kutufanya imara kumtii Mungu na amri zake, badala ya kutii mnyama na kumwabudu.

Masihi wa Uongo

Hata hivyo turudi tena katika marejeo ya Yesu. Baadhi ya wengi pia, husema Yesu atakuja kisiri, ya kwamba atajionyesha kwa mtu mmoja hapa na baadaye kwa mtu mwingine kwingineko. Yesu alionya kuhuzu udanganyifu huu. Alijua matukio haya yatakuepo naye akasema `Wakati huo mtu akiwaambia, tazama, Kristo yupo hapa, au yuko kule msisadiki. Kwa maana watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu, wapate kuwapoteza, kama yamkini, hata walio wateule. Tazama, nimekwisha kuwaonya mbele. Basi wakiwaambia, yuko jangwani, msitoke; yumo nyumbani; msisadiki kwa maama kama vile umeme utokavyo mashariki ukaonekana hata Magharibi, hivyo ndivyo kutavyokuwa kuja kwake mwana wa Adamu' (Mathayo 24:23-27)

Jinsi tumejifunza, Yesu hataikanyaga nchi kwa miguu yake katika marejeo yake ya pili, kwa hivyo, hatupaswi sisi wenyewe kuingizwa katika uongo wakati mtu mmoja anapodai kwamba Yesu amerejea na ni katika sehemu fulani tu. Kwa kweli tumeona ya kwamba yesu atakuja na mawingu ya mbinguni wakati wa tarumpeta ya mwisho, ikiwa wazi na yakuonekana kama vile umeme utokavyo na kuonekana angani, na kuonekana kwa macho, tutamtazama Yesu ajapo mara ya pili. Waona sasa Biblia hufundisha wazi kurudi kwa Yesu hivi, `tazama, yuaja na mawingu na kila jicho litamwona, na hao waliomchoma (Ufunuo 1:7). Tunasoma tena - wote waliokombolewa, watanyakuliwa mawinguni kukutana na Yesu angani. Hawatakutana na Yesu katika nchi bali huko juu angani.

Badiliko

Sasa, kutafanyika nini kwa waliokombolewa katika marejeo ya pili? Ndio sababu biblia husema wote watakaobadilishwa. `Angalieni, nawaambieni siri; sisi hatutalala zote, lakini zote tutabadilishwa, kwa dakika moja, kufumba na kufumbua, wakati wa parapanda ya mwisho maana parapanda italia na wafu watafufuliwa, wasiwe na uharibifu, nasi tutabadilika. Maana sharti huu uharibikao uvae kutoharibika, nao huu wa kufa uvae kutokufa. Basi huu unaharibikao utakapovaa kutaharibika na huu wa kufa utakapovaa kutokufa, hapo ndipo litakapokuwa lile neno lililoandikwa, mauti imemezwa kwa kushinda'. (1 Wakorinto 15:51-54)

Paulo pia anatoa maelezo kuhusu kubadilishwa kwa maneno haya. `Kwa maana sisi, wenyeji wetu uko mbinguni, kutoka huko tena tunamtazamia Mwokozi Bwana Yesu Kristo atakayeubadilisha mwili wetu wa unyonge, upate kufanana na mwili wake wa utukufu, kwa uweza ule ambao kwa huo aweza hata kuvitiisha vitu vyote viwe chini yake'.

Biblia hufananisha kwamba wanadamu (Adamu na Hawa) waliumbwa kwa mfano wa Mungu. Wangekuwa mbele za Mungu ndipo wangekuwa na mwili wa utukufu ili waweze kukubalika mbele zake. Lakini walipoasi kwa kula tunda la mti wa ujuzi wa mema na mabaya, waliupoteza utukufu wa Mungu (Mwanzo 3:6-9). Hawangeweza kumwona na kuishi tena. Miili yao ikawa midhaifu na ya mauti. Sisi zote tunayo miili ya aina hiyo. Hata hivyo Mungu alikusudia kuwarudisha wanadamu katika hali ile ya kwanza kabla ya dhambi. Wakati watakapokubalika mbele za Mungu bila mauti tena. Haya yote yatatokea wakati Yesu kristo arejeapo kuwakusanya wateule wake.

Wafu katika makaburini mwao

Tunasoma tena kuhusu mwili uharibikiao, ni lazima uvalishwe mwili wa kutoharibika. Ni Mungu tu asiye na mwili wa mauti. Biblia huthibitisha katika hali hii ambaye peke yake hapatikani na mauti (1Timotheo 6:16).

Wakati mtu anapokufa, yeye hukoma kuwepo. Imeandikwa `Kwa sababu hiyo walio hai wanajua ya kwamba watakufa, lakini wafu hawajui neno lolote wala hawana ijara tena; maana kumbukumbu lao limesahauliwa, mapenzi yao na machukio yao na husuda yao imepotea yote pamoja wala hawana sehemu tena katika jambo lolote lilifanyika chini ya jua'…. lolote mkono wako utakalolipata kulifanya, ulifanye kwa nguvu zako kwa kuwa hakuna kazi wala shauri, wala maarifa, wala hekima huko kuzimu ueondako wewe. (Mhubiri 9:5-6,10)

Kwa hivyo, wakati mwanadamu amekufa, yeye huwa ni kama jiwe lisilokuwa na uhai. Yeye hana uhai, fikara, wala hana ijara tena maana kumbukumbu lake limesahaulika. Wanalala mavumbini na kuwa mavumbi, ndio sababu itakuwa ni muujiza yesu atakapowaita wanadamu kutoka makaburini wengine kwa uzima wa milele, na wengine kwa aibu ya milele. (Mwanzo 3:19 Johana 5:29)

Wakati mmoja, rafiki yake Yesu (Lazaro) alikufa na kukaa kaburini siku nne, Yesu aliita kifo chake kuwa amelala. Naye akasema Lazaro amekufa (Johana 11:1-44) Kwa hivyo, wafu wapo makaburini/wamelala. Wale wanaokufa wakimwamini Yesu wataamshwa katika marejeo ya Yesu, lakini wenye dhambi waliosalia, hawatafufuliwa hata itimie miaka elfu. (Maelezo haya ni baadaye)

Kama jinsi Yesu alipomfufua Lazaro kutoka kaburini ndivyo atakavyowafufua waaminio wanaopumzika makaburini katika asubuhi ya ufufuo. Katika tukio hili Lazaro atapewa mwili wa kutoharibika katika marejeo ya Yesu mara ya pili. Tunatarajia na kuamini Lazaro atakuwa kati ya kikundi cha ushindi.

Hakuna ufufuo bila ufufuo wa Yesu

Yesu alikuwa mzaliwa wa kwanza kwa wale waliofufuliwa alipoamuka kutoka wafu siku ya kwanza ya juma (Luka 24:6) Paulo hutoa maelezo haya `lakini sasa Kristo amefufuka katika wafu, limbuko lao waliolala; maana kwa kuwa mauti ililetwa kwa mtu mmoja, kadhalika na kiyama ya wafu ililetwa na mtu. Kwa kuwa kama katika adamu wote wanakufa, kadhalika na katika Kristo wote watahuishwa, lakini kila mmoja mahali pake limbuko ni Kristo atakapokuja. [1 Wakorintho 15:20-23]

Sehemu yako kwenye mti wa uzima

Fikiria waliokombolewa wakipewa mwili wa utukufu na kutoharibika; wengine wakibadilishwa badiliko la hakika! Hakuna mtu anaweza kumwona Mungu na akaishi, lakini waliokombolewa watamwona uso kwa uso (Ufunuo22: 4)

Je ni kusudi lako kubadilishwa? Nadhani ni hivyo. Kwa hivyo shikilia ahadi zake sasa. Mungu anafanya kazi ndani yako, itika `ndio' kwa Yesu, fanya uamuzi huu, lazima tubadilishe mawazo yetu na mienendo yetu kumwelekea Mungu. Sasa kama tutapewa mwili wa utukufu katika marejeo ya pili ya Yesu_lazima tuchukue hatua hii. Mungu amethibitisha wazi kuwa yeye ni pendo. Utakapochukua hatua hii utahitajika kujiweka katika maombi ili upate nguvu ya kumfuata yeye. Katika yeye twaweza kupata ushindi mkuu. Ahadi za ushindi ni nyingi . Hapa kuna chache tu `yeye aliye na sikio na alisikie neno hili ambalo roho ayaambia makanisa. Yeye ashindaye nitampa baadhi ya ile mana iliyofichwa, nami nitampa jiwe jeupe, na juu ya jiwe hilo limeandikwa jina jipya asilolijua mtu ila yeye anayelipokea` (Ufunuo 2:17). Yeye ashindaye nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi (Ufunuo 3:21)

Heri wazifuao nguo zao. Wawe na amri kuuendea huo mti wa uzima na kuingia mjini kwa milango yake (Ufunuo 22:14).

Badiliko katika mawazo

Kupitia kwa nguvu za Roho Mtakatifu, waliokombolewa wakiwa hai watakuwa wamepata ushindi dhidi ya ibilisi na zaidi ya hayo, katika marejeo ya pili watapitia katika hali ya kubadilishwa itakayowawezesha kwenda pamoja na mwokozi, malaika wote wa mbinguni na waliokombolewa. Hata hivyo, je badiliko hili la mwanzo litakuwaje; Badiliko hili litakuja Yesu ajapo au kabla ya marejeo ya pili ya Yesu? Tutafute jibu katika neno la Mungu. `Petro akawaambia, tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo mpate ondoleo la dhambi zenu nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu. (Matendo 2: 38)

Basi, ndugu zangu, nawasihi kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana. Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu. Kwa maana kwa neema nilipewa namwambia kila mtu aliyeko kwenu asinie makuu kupita ilivyompasa kunia bali awe na nia ya kiasi, kama Mungu alivyomgawia kila mtu kiasi cha imani. Kwa kuwa kama vile katika mwili mmoja tuna viungo vingi, wala viungo vyote havitendi kazi moja, vivyo hivyo na sisi tulio wengi tu mwili mmoja katika kristo. Basi kwa kuwa tuna karama zilizo mbalimbali kwa kadiri ya neema mliyopewa, ikiwa unabii; tutoe unabii kwa kadiri ya imani. Ikiwa huduma, tuwemo katika huduma yetu; mwenye kufundisha, katika kufundisha kwake, mwenye kuonya katika kuonya kwake; mwenye kukirimu, kwa moyo mweupe; mwenye kurehemu kwa furaha. Pendo na lisiwe na unafiki lichukieni lililo ovu, mkiambatana na lililo jema, kwa pendo la undugu, mpendane mkiwatanguliza wenzenu, kwa bidii si walegevu; mkiwa na juhudi katika dhiki, mkisubiri katika kusali, mkidumu. (Warumi 12:1-12). Iweni na nia iyo hiyo ndani ya Kristo Yesu (Wafilipi 2:5). Heri wenye moyo safi; maana hao watamwona Mungu` (Mathayo 5:8). Ni nani atakayepanda katika mlima wa Bwana? Ni nani atakayesimama katika patakatifu pake? Mtu aliye na mikono safi na moyo mweupe. (Zaburi 24:3-4).

Wakati huo, Yesu atakaporudi kuwakusanya wateule, watakuwepo masalio wanaoishi wa Mungu` (Zephania 3:12-13, Ufunuo 12:17) Hawa walikataa alama ya mnyama na wakakubali kupokea muhuri wa Mungu katika vipaji vya nyuzo zao. Mungu wa milele atakuwa amekubali kundi hili. Biblia hutoa maelezo kwa njia hii` Na ndani yake hakitaingia kamwe chochote kilicho kinyonge, wala yeye afanyaye machukizo na uongo, bali wale walioandikwa katika kitabu cha uzima cha mwana kondoo' Bwana akamwambia, pita kati ya mji, kati ya Yerusalemu, ukatie alama katika vipaji vya nyuso za watu wanaougua na kulia kwa sababu ya machukizo yote yanayofanyika kati yake. (Ezekieli 9:4)

Upendo wa Mungu ukiwa unawaka ndani ya mioyo yao, wataugua na kulia kwa sababu ya machukizo yanayofanywa kati ya wana wa Mungu.Na watakuwa wameonya wenzao kuhuzu matokeo ya uasi huo. Masalio wa watu wa Mungu watatubu na kumfuata mwana na kondoo popote aendapo. Watakuwa wamekubaliwa na Mungu na kupokea chapa ya uthibitisho katika vipaji vya nyuzo zao. Kwa imani watakuwa wamepokea msamaha na haki ya Kristo, na watakuwa wamepokea nguvu za roho mtakatifu za kufanya yaliyo mema. (1 Yohana 1:9) (2: 29) Katika maono, Yohana aliona waliokombolewa wamesimama, juu ya mlima Zayuni. Ndivyo anatoa maelezo ya tabia zao` hawa ni wale hawakunajiziwa na wanawake (makanisa yanayotangaza mafundisho yasiyo ndani ya biblia). (Wakorintho 11:2) kwa kuwa hao ni bikira, hawa ndio wamfuatao mwana kondoo (Kristo) Yohana 1:29) popote aendako hawa ndio waliokombolewa kati ya wanadamu, wakiwa wazaliwa wa kwanza kwa Mungu na mwana kondoo. Na katika midomo yao hawakuonekana na hila wala kunyazi mbele ya kiti cha enzi cha Mungu. (Ufunuo 14:1-5).

Katika sehemu hii, maandiko haya na mengine mengi yanatueleza mabadiliko ya mawazo ya uzima yanayohitajika sasa. Tusipobadilika katika mawazo kabla ya kifo chetu au kabla ya marejeo ya Kristo, hatutakombolewa na kwa hivyo hatutaenda pamoja na Yesu mbinguni. Ni wao tu walio wasafi katika roho zao watachukuliwa wakati wa marejeo. Hawa ni wazaliwa wa kwanza watakaofufuliwa.

Mavuno

Biblia huthibitisha wazi kwamba, wakati ujumbe wa onyo la mwisho, utakuwa umepeanwa kwa sauti kuu kwa dunia yote Yesu Kristo mwokozi wa ulimwengu atakuja katika mawingu ya mbinguni (Mathayo 24:13) ufunuo 14:6-12) ndipo wakati wa mavuno utaanza, Yohana autaja wakati huu wa mavuno kuwa `kisha nikaona, na tazama wingu jeupe, na juu ya wingu hilo ameketi mmoja, mfano wa mwanadamu, mwenye taji ya dhahabu juu ya kichwa chake, na katika mkono wake mundu mkali. Na malaika mwingine akatoka katika hekalu, akimlilia kwa sauti kuu yeye aliyekuwa ameketi juu ya lile wingu, tia mundu wako, ukavune kwa kuwa saa ya mavuno imekuja kwa kuwa mavuno ya nchi yamekomaa. Nayeye aliyeketi juu ya wingu akautupa mundu wake juu ya nchi, nchi ikavunwa. (Ufunuo 14:14-16).

Maandiko hayo yote ni thibitisho tosha ya kwamba Yesu Kristo anakuja kuwakusanya walio wake; kwa kuvuna mavuno yalio tayari. Atavuna wale ambao kupitia kwa neema ya Mungu na nguvu zake wamejifunza tabia na kufanana naye Yesu. Watakuwa wamebadilika wakionyesha uzuri, usafi na upole wa Yesu katika maisha yao. Kupitia kwa neema ya Mungu na nguvu za Roho Mtakatifu katika maisha yao kwa furaha watazitunza amri za Mungu na imani ya Yesu (Ufunuo 14:12, 1 Yohana 5:2-3)

Paulo huzungumzia mabadiliko ambayo yanahitajika kuchukua nafsi katika maisha yetu ila tungali tunaishi wakati wa muda wa rehema, lakini sisi sote tukitazama kana kwamba ni katika kioo utukufu wa bwana tunabadilishwa nafsi zetu kutoka utukufu hadi utukufu kama vile roho wa Bwana anaponena, (II Korintho 3:18) nimesulubiwa pamoja na Kristo; "lakini ni hai wala si mimi tena bali Kristo yu hai ndani yangu; na uhai nilio nao sasa katika mwili, ninao katika imani ya mwana wa Mungu ambaye alinipenda, akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu. (Wagalatia 2:20).

`Lakini tunda la roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria. Na hao walio wa Kristo Yesu wameusulibisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake. Tukiishi kwa roho na tuenende kwa roho' (Wagalatia 5:22-25). Kama mkijua ya kuwa yeye ni mwenye haki, jueni ya kuwa kila atendaye haki amezaliwa na yeye` (Yohana 2:29). Heri wazifua nguo zao wawe na amri kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa milango yake'. (Ufunuo 22:14).

Ni mazao yalio tayari- watu waliosulubisha nafsi zao kwa kupitia kwa neema ya Mungu na nguvu zake wataonekana katika maisha yao_hao ndio Kristo anakuja kuchukua.

Mfalme wa _Wafalme, Bwana wa Mabwana

Biblia husema nyakati za mwisho, nguvu zote za uovu katika dunia watafanya vita dhidi ya Kristo na walio pamoja naye. Imeandikwa `hawa watafanya vita na mwana kondoo na mwana kondoo atawashinda, kwa maana yeye ni Bwana wa mabwana na mfalme wa wafalme na hao walio pamoja naye ndio walioitwa ni wateule na waaminifu' (Ufunuo 17:14). Katika marejeo ya pili, wakati mfalme wa wafalme na bwana wa mabwana atakaporejea ataonekana katika utukufu wake'

`Ndipo itakapoonekana ishara yake mwana wa Adamu mbinguni, ndipo mataifa yote ya ulimwengu yatakapoomboleza nao watamwona mwana wa adamu akija juu ya mawingu ya juu pamoja na nguvu na utukufu mwingi naye atawatupa malaika zake pamoja na sauti kuu ya parapanda nao watawakusanya wateule wake kutoka pepo nne kutoka mwisho huu wa mbingu mpaka mwisho huo' (Mathayo 24:30-31). Hapa tunasoma kwamba Yesu atarudi tena pamoja na nguvu na utukufu mwingi. Wale waliokombolewa ambao watapewa mwili wa utukufu, hawataona shida, atakapoonekana watasema kwa furaha, `Huyu ndiye Mungu wetu, ndiye tulimngojea atusaidie, huyu ndiye Bwana tuliyemngojea na tushangilie na kuufarahia wokovu wake' Isaya 25:9

Fikiria siku ya ajabu siku ya ukombozi! Tazama picha ya siku hii ya kusherekea itakavyokua kwa watakatifu waliofufuliwa kutoka makaburini na waliokombolewa wakiwa hai watakapomwona mwokozi akija tena. Hao wamehubiri kuhusu tukio hili, wamepambana na upinzani, matezo na mauti; lakini haya yote nini kulinganisha na utukufu watakaoupokea! Sasa wanamwona mfalme wa wafalme na Bwana wa mabwana akija kuwakusanya pamoja wakiwa na furaha kuu. Nyuzo zao zikionyesha miili ya furaha. Hakuna kalamu inayoweza kueleza furaha itakayojaa ndani ya waliokombolewa watakapomwona mkombozi wao na jeshi la malaika na wapendwa wao waliokuwa waaminifu kwa bwana hadi kifo.

Macho yote yatamtazama mwokozi kama jinsi tumeona katika neno la Mungu watakatifu waliokombolewa watanyakuliwa hadi mawinguni ili kumlaki Bwana angani. Ni tukio la ajabu namna gani tukisafilishwa hadi mawinguni-wenye mwili wa utukufu walio huru na waliokombolewa. Sasa wako salama pamoja na Mungu. Maadui zao hawawezi kuwafikia tena. Sasa wako katika mikono ya usalama. Wakati watakaponyakuliwa hadi mawinguni wakipita kati ya nyota zingaao wakiacha nyuma nyota za miali na sayari, wakiingia katika mji mtakatifu mbinguni, watavuta hewa ya kuridhisha kwa furaha. Waliokombolewa kupitia kwa damu ya mwana kondoo, sasa watapumzika. Hakuna ibilisi au mshtaki, wahalifu au amri za binadamu. Amani, upendo, furaha, urafiki vitatawala huko. Matunda yote ya roho ni dhahiri.

Milenia Hukumu kuendelea Mbinguni

Biblia husema kuwa waliokombolewa watakuwa mbinguni kwa muda wa miaka elfu moja. Imeandikwa `kisha nikaona viti vya enzi, wakaketi juu yake, nao wakapewa hukumu; nami nikaona roho zao waliokatwa na kwa ajili ya neno la Mungu, na hao wasiomsujudia yule mnyama, wala sanamu yake, wala hawakuipokea ile chapa katika vipaji vya nyuso zao, wala katika mikono yao; nao wakawa hai, wakatawala pamoja na Kristo miaka elfu' (Ufunuo 20:4). Fungu hili linaandamana na (1wakorinto 6:2).

Kwa hivyo waliokombolewa wataketi viti vya hukumu huko mbinguni. Ni akina nani watakaowaukumu? Hukumu ya upelelezi imechunguza matendo ya watakatifu kwa ajili ya waliokombolewa. Kwa haki Yesu amechunguza maisha yao. Biblia imeelezea jinsi hukumu hii itakavyoendeshwa kwa maneno haya. `Rehema na msamaha ni kwa Bwana Mungu wetu, ingawa tumemuasi; wala hatukuitii sauti ya Bwana, Mungu wetu, kwa kuenenda katika sheria zake; alizoziweka mbele yetu kwa kinywa cha watumishi wake, manabii'. (Danieli 7:9-10)

Matendo ya wenye haki yamechunguzwa na kukubalika kwa ajili ya wokovu wao.

Paulo huweka wazi, kuwa kila mmoja atatoa habari zake mwenyewe. `Basi ni hivyo, kila mtu miongoni mwetu atatoa habari zake mwenyewe mbele za Mungu'. (Warumi 14:12)

Hatutapotea au kuokolewa kwa vikundi bali kila mmoja kivyake. Watu wengi watakaokuwa wanaishi dunia wakati wa Yesu kurejea mara ya pili hawataenda mbinguni. Kufikia wakati huo hukumu ya kila mmoja itakuwa imepitishwa; hawatakuwa wamepokea malipo ya mazao yao ya mwisho. Sasa watakatifu watakubalika kusoma wenyewe kutoka vitabu vya kumbukumbu vya mbinguni ya kwamba waliopotea, wamepokea hukumu inayowasitahili; hata hivyo waume wengine watawakosa wake wao wapendwa na watakuwa wakishangaa ni kwa nini wapendwa wao hawakuingia mbinguni? Katika vitabu vya mbinguni, vitu vyote vimenakiliwa na waliokombolewa watauhukumu ulimwengu.

Watahakikisha ya kwamba kila mmoja aliyepotea amepata hukumu inayostahili. Unajua twaweza kuwashuku watu kwa maneno yao na matendo yao, lakini Mungu anahukumu roho zetu. Anajua kila dhambi ambayo hatujatubu. Dhambi zote zimenakiliwa katika vitabu vya mbinguni na wateule watakagua vitabu hivyo. Waovu wataukumiwa kulingana na kazi zao au matendo yao. Hii inaleta swali la kibinafsi; mngetaka wengine wachunguze maisha yako? Mngependa waone matendo yako maovu? Dhambi hasa ulioitenda kwa siri bila wengine kujua? Kama hautaki wateule kuchunguza matendo yako ya siri, ni heri sasa uamue kuchukua dhambi zako kwa Yesu ili aweze kufanya upatanisho kwa ajili yako. Wokovu umetolewa kwa masharti. Yesu amefanya yote ili sisi tuishi milele bila mauti, lakini ni jukumu letu kukubali zawadi ya wokovu; mwaliko wa mwokozi uko wazi. `Tukiziungama dhambi zetu, yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolea dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote'. (1 Johana 1:9)

Rafiki mpendwa usikubali dhambi itawale maisha yako. Ilete miguuni pa Yesu; omba upate neema na ujasiri ili kufanya mambo yawe sawa kwa yule uliyemkosea na Yesu atakupa msamaha. Utakuwa huru na dhambi na kujifunganisha na Yesu, na utakua mmoja watakao uhukumu ulimwengu badala ya maisha yako kuchunguzwa na kuhukumiwa.

Na Mungu atusaidie tusiwe wenye mioyo migumu au wenye kiburi bali tuwe wanyenyekevu mbele za Bwana. Unyenyekevu huelekeza kuheshimiwa. Ni sasa muda wa rehema ungalipo ambapo twaweza kunyenyekea mbele za Bwana ili kwa damu yake mwana kondoo, dhambi zetu zipate kuondolewa na kuweza kusimama katika siku ile arudipo.

Shetani kifungoni miaka elfu moja

Sasa tumeona watakatifu watakuwa mbinguni kwa miaka elfu nao watakalia viti vya hukumu, nao wataishi miaka elfu moja mbinguni. Wakati huu, ni nini kitafanyika kwa waovu? Tunasoma ya kwamba, katika marejeo ya Yesu mara ya pili, Yesu ataonekana katika utukufu wake. Watakatifu watastahimili mwanga huo lakini kulingana na Biblia, ni heri walio na moyo safi maana hao watamwona Mungu. Wale wasio na mioyo safi na miili ya utukufu, hawatamwona Mungu wala kusitahimili kuja kwake, kwa hivyo waovu wataangamia kutokana na mwanga wa uwepo Wake. Biblia hutoa maelezo kuhuzu marejeo ya Yesu hivi. `Mbingu zikaondolewa kama ukurasa ulivyokunjwa, na kila mlima na kisiwa kikahamishwa kutoka mahali pake; na wafalme wa dunia, na wakuu, na majemadari, na matajiri, na wenye nguvu, na kila mtumwa, na mwungwana, wakajificha katika pango na chini ya miamba ya milima, wakiiambia milima na miamba, tuangukieni, tusitirini, mbele za uso wake yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na hasira ya Mwana-kondoo. Kwa maana siku iliyo kuu, ya hasira yao, imekuja; naye ni nani awezaye kusimama?' (Ufunuo 6:14-17

`Wateule peke yao ndio wataweza kusimama na kumwona uso wake Mungu na kuishi kwa sababu mioyo yao ni safi na watakuwa wamepokea miili ya utukufu. Waovu watakuwa na miili ya kuharibika huku mioyo yao ikijaa dhambi. Hawataweza kusimama mbele ya utukufu wa uwepo wake. Hivyo watakufa wakiomba milima na majambali iwaangukie na kuwaficha mbele za uso wake.

Kwa hivyo waovu watakufa wakimwona Yesu akirudi. Shetani akiwa hana mtu wa kudanganya atakuwa anatembea huku na huku katika dunia bila mtu wa kudanganya. Biblia hutoa maelezo ya tukio hili kwa njia hii. `Kisha nikaona malaika akishuka kutoka mbinguni, mwenye ufunguo wa kuzimu, na mnyororo mkubwa mkononi mwake; akamshika yule joka, yule nyoka wa zamani, ambaye ni Ibilisi na Shetani, akamfunga miaka elfu; akamtupa katika kuzimu, akamfunga, akatia muhuri juu yake, asipate kuwadanganya mataifa tena, hata ile miaka elfu itimie, na baada ya hayo yapasa afunguliwe muda mchache'. (Ufunuo 20:1-3)

Shetani atafungwa kwa hali ngumu. Hatakuwa na mtu wa kudanganya tena; watakatifu watakuwa mbinguni na waovu hawatakua hai, kutokana na marejeo ya Kristo, Biblia huelezea hivi. `Tazama, siku ya Bwana inakuja, siku ya hasira kali na ghadhabu kuu, ili iifanye nchi kuwa ukiwa, na kuwaharibu watu wake, wenye dhambi wasikae ndani yake'. (Isaya 13:9). `Hiyo siku ya Bwana iliyo kuu i karibu; karibu nayo inafanya haraka sana; Naam, sauti ya siku ya Bwana Shujaa hulia kwa uchungu mwingi huko. Siku ile ni siku ya ghadhabu, siku ya fadhaa na dhiki, siku ya uharibifu na ukiwa, siku ya giza na utusitusi; siku ya mawingu na giza kuu. Siku ya tarumbeta na ya kamsa, juu ya miji yenye maboma, juu ya buruji zilizo ndefu sana. Nami nitawaletea wanadamu dhiki, hata watakwenda kama vipofu, kwa sababu wamemtenda Bwana dhambi na damu yao itamwagwa kama mavi. Fedha yao wala dhahabu yao havitaweza kuwaokoa katika siku ile ya ghadhabu ya Bwana; bali nchi yote pia itateketezwa kwa moto wa wivu wake; maana atawakomesha watu wote wakaao katika nchi hii, naam, ukomo wa kutisha'. (Sefania 1:14-18). Pia tutaunganisha na ushindi nabii Yeremia anasema `Naliiangalia nchi, na tazama ilikuwa ukiwa, haina watu; naliziangalia mbingu, nazo zilikuwa hazina nuru. Naliiangalia milima, na tazama, ilitetemeka, na milima yote ilisongea huko na huko. Nikaangalia, na tazama, shamba lililozaa sana limekuwa ukiwa na miji yake yote ilikuwa imebomoka mbele za Bwana, na mbele za hasira yake kali'. (Yeremia 4:23-26)

Baada ya Milenia

Je, ni nini kitakachofanyika baada ya miaka elfu? Ndio waovu waliokufa watafufuliwa kutoka makaburini mwao. Huu utakuwa ufufuo mwingine, ufufuo wa pili, Biblia hutoa maelezo kwa maneno haya. `Hao wafu waliosalia hawakuwa hai, hata itimie ile miaka elfu'.(Ufunuo 20:5)

Zaidi tena, baada ya miaka elfu moja, dunia itajaa na watu. Waovu wataijaza dunia, wale waliomkataa Yesu na kukataa kufuata nyayo zake (1Petero 2:21-24), watafufuliwa, wakiwa na miili ya kufa, sio kama wateule, hao watakuwa jinsi walivyokuwa duniani, wakiwa na tamaa zao, mafikira zao za ukatili na matarajio yao maovu. Katika mauti yao haitabadilishwa.

Hata hivyo, sio waovu tu watakaoajibika, shetani naye pia atafunguliwa kutoka kifungoni mwake. Tena atakua na wengi wa kudanganya . Biblia husema, `Na hiyo miaka elfu itakapomalizika, Shetani atafunguliwa, atoke kifungoni mwake' Ufunuo 20:7). Na Biblia inazidi kusema `Naye akatoka kuwadanganya mataifa walio katika pembe nne za nchi, Gogu na Magogu, kuwakusanya kwa vita, ambao hesabu yao ni kama mchanga wa bahari. Wakapanda juu ya upana wa nchi, wakaizingira kambi ya watakatifu na mji huo uliopendwa. Moto ukashuka kutoka mbinguni, ukawala'. (Ufunuo 20:8-9)

Hii ndio vita vya Gogu na Magogu. Wengine hufundisha kuwa vita hivi vitapiganwa kabla ya miaka elfu moja; lakini kama jinsi tulivyoonyeshwa, vitafanyika baada ya miaka elfu ndipo shetani atakapowafanya waovu kuueleka mji mtakatifu uliopendwa; Yerusalemu mpya ambao utashuka kutoka mbinguni kama bibi arusi aliyetayarishwa kwa mumewe. Biblia husema kuhusu mji huu. `Nami nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari, kama bibi-arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe. (Ufunuo 21:2)

Yerusalemu mpya kusimama juu ya mlima wa Mizeituni

Nabii Zekaria anaandika hivi kuhusu mji wa Yerusalemu mpya, ulioonekana ukishuka juu ya mlima wa mizeituni, anasema. `Na siku hiyo miguu yake itasimama juu ya mlima wa Mizeituni, unaoelekea Yerusalemu upande wa mashariki, nao mlima wa Mizeituni utapasuka katikati yake, upande wa mashariki na upande wa magharibi; litakuwako huko bonde kubwa sana; na nusu ya mlima ule utaondoka kwenda upande wa kaskazini, na nusu yake utaondoka kwenda upande wa Kusini. Nanyi mtakimbia kwa njia ya bonde la milima yangu, kwa maana bonde lile la milima litaenea hata Aseli, naam, mtakimbia kama vile mlivyokimbia mbele ya tetemeko la nchi, siku za Uzia, mfalme wa Yuda; na Bwana Mungu wangu, atakuja, na watakatifu wote pamoja naye'. (Zekaria 14:4-5)

Hapa tumeona baada ya wateule kukaa miaka elfu mbinguni, palipo mji mtakatifu wa mbinguni, Yerusalemu mpya utashuka juu ya mlima wa mizeituni. Biblia haisemi kwamba Bwana Mungu atakuja pamoja na wateule wake. Kwa hivyo kwa mara ingine wateule wataikanyaga dunia. Hata hivyo, kabla Mungu hajaumba mbingu mpya na nchi mpya, mahali patakatifu patadumu ndipo vita vya Gogu na Magogu vifanyike. Tunasoma kuwa shetani atauelekea mji mtakatifu, Yerusalemu mpya atawakusanya waovu wote kwa vita dhidi ya Mungu, malaika wa mbinguni na waliokombolewa. Shetani na waovu mara ingine watauzingira mji ili kuwakamata watakatifu. Lakini tukio ambalo halikutazamiwa litatokea. Moto ukashuka kutoka mbinguni na kuwaka; ndivyo shetani na malaika zake, mnyama na nabii wa uongo na watu wote walio katika makanisa na vikundi vya kidini na wote waliomkataa kumkubali Yesu Kristo kama mwokozi wao, wataangamizwa milele. (Ufunuo 20:7-10). Ndiposa watapokea matunda ya matendo yao. Walichagua njia zao, bali sio njia ya Yesu ndipo watawauliza viongozi wao `kwa nini mlitupeleka kwa njia potovu? Kwa nini mlituongoza kuamini ya kwamba tungetenda dhambi na kuichezea na kusherekea na mwisho wake tukombolewe? Kwa nini watakuwa wamechelewa. Ndipo watapotea wakitazamia hukumu yenye kutisha ya milele.

Katika barua yake ya pili ya mtume Petero anaandika. `Lakini siku ya Bwana itakuja kama mwivi; katika siku hiyo mbingu zitatoweka kwa mshindo mkuu, na viumbe vya asili vitaunguzwa, na kufunuliwa, na nchi na kazi zilizomo ndani yake zitateketea'. (II Petero 3:10)

Yohana naye anaandika, `Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili'. (Ufunuo 21:8) Kama jinsi tulivyoona, Biblia hutaja ziwa la moto kuwa ndio mauti ya pili (Ufunuo 20:14) Jehanamu ni mahali ambapo mateso makali yatakuwa kwa wale ambao sio wa Mungu kulingana na Biblia kila mtu atahukumiwa kulingana na matendo yake. (Ufunuo 20:12-13). `Na iwapo mtu yeyote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto'. (Ufunuo 20:15)

Nabii Malaki pia ametoa maelezo kuhusu hukumu hii ya ziwa la moto, na anaeleza hivi. `Kwa maana angalieni, siku ile inakuja, inawaka kama tanuru; na watu wote wenye kiburi, nao wote watendao uovu, watakuwa makapi; na siku ile inayokuja itawateketeza, asema Bwana wa majeshi; hata haitawaachia shina la tawi'. (Malaki 4:1)

Waovu watachomeka kama majani, shina la mti mbichi laweza kuchomeka kwa muda mrefu lakini matawi na vijiti vidogo vitachomeka kwa muda mfupi tu. Hili ni fundisho la kutuonyesha kuhusu hukumu ya kila mmoja. Watahukumiwa kulingana na matendo yao, shetani atapokea hukumu ilio kali kama uchungu na matezo ya ziwa la moto yataishia kifo cha milele. Hayo ndiyo matokeo ya uovu, waovu pamoja na maovu yao wataangamizwa katika moto uuwakao wa kuangamiza shina na tawi, shetani akiwa ni shina na watumishi wake ni matawi. Matezo ya kuvunja amri yatakuwa yamekamilishwa na matarajio ya wenye haki kutimizwa. Mbingu na nchi zitatangaza kuwa Mungu ni mwenye haki.

Hakutakuwa na kifo tena, wala uchungu, wala maombolezo wala kuchukizwa kwa sababu maovu yatakuwa yameangamizwa.

Mbingu mpya na Nchi mpya

Katika kipindi hicho, Mungu ataumba mbingu mpya na nchi mpya. Yohana huonyesha matokeo ya kazi hii ya ajabu ya kwamba; `Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya; kwa maana mbingu za kwanza na nchi za kwanza zimekwisha kupita, wala hapana bahari tena'. (Ufunuo 21:1)

Kile kilichopotezwa kutokana na dhambi kitafanywa upya. Dunia mpya itakuwa makao ya milele ya waliokombolewa, fikira ya kufikiria mambo yajayo kama urithi wa vitu, uwewavumba wengi macho ya kiroho ili kutoangazia ukweli utakaotuongoza hata kuangalia makao yetu ya milele. Yesu aliwahakikishia wanafunzi wake kuwa ameenda kuwaandalia makao huku nyumbani kwa Baba. Wale wote wanaoamini mafundisho ya neno la Mungu, hawatapuuza kamwe kuhusu makao ya mbinguni. `Lakini, kama ilivyoandikwa; mambo ambayo jicho halikuyaona wala sikio halikusikia, (wala hayakuingia katika moyo wa mwanadamu,) mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao'. (1 Wakorinto 2:9)

Lugha ya binadamu ni finyu kuelezea zawadi ya wenye haki ijulikanayo tu na wale watakaipokea. Hakuna lugha ya kuelezea kuhusu utukufu wa paradizo ya Mungu. Katika biblia, urithi wa wateule umeelezwa kuwa ni mji (Waebirania 11:14-16). Huko mchungaji wa mbinguni akiongoza kundi lake hadi kwenye chemi chemi za maji ya uzima. Mti huu wa uzima huzaa matunda yake kila mwezi na matawi yake ni ya kuwaponya mataifa. Kuna mito isiyokauka, maji safi kama kioo. Miti inayoleta kivuli chake kwa njia iliotengenezwa kwa ajili ya waliokombolewa wa Bwana. Nchi tambalale yenye vilima vidogo vya kupendeza na milima ya Mungu itakuwa kilele chake. Katika njia hizo tambalale kando ya mito ya uzima, watu wa Mungu watazunguka-zunguka kwa muda mrefu, wapitaji na wageni katika dunia, mwishowe watapata makao yao ya milele. `Na watu wangu watakaa katika kao la amani; na katika maskani zilizo salama, na katika mahali pa kupumzikia penye utulivu'. `Nao watajenga nyumba na kukaa ndani yake; watapanda mizabibu, na kula matunda yake. Hawatajenga, akakaa mtu mwingine ndani yake; hawatapanda akala mtu mwingine; maana kama siku za mti ndivyo zitakavyokuwa siku za watu wangu, na wateule wangu wataifurahia kazi ya mikono yao muda wa siku nyingi. (Isaya 32:18, 65:21-22)

`Nyika na mahali palipo ukiwa patafurahi, jangwa litashangilia na kuchanua maua kama waridi'. `Badala ya michongoma utamea msunobari; na badala ya mibigili, mhadesi; jambo hili litakuwa la kumpatia Bwana jina, litakuwa ishara ya milele isiyokatiliwa mbali. Mbwa-mwitu atakaa pamoja na mwana-kondoo, na chui atalala pamoja na mwana-mbuzi; ndama na mwana-simba na kinono watakuwa pamoja, na mtoto mdogo atawaongoza. Ng'ombe na dubu watalisha pamoja; watoto wao watalala pamoja; na simba atakula majani kama ng'ombe. Na mtoto anyonyaye atacheza penye tundu la nyoka, na mtoto aliyeachishwa atatia mkono wake katika pango la fira. Hawatadhuru wala hawataharibu katika mlima wangu wote mtakatifu; maana dunia itajawa na kumjua Bwana, kama vile maji yanavyoifunika bahari'. (Isaya 35:1, 55:13, 11: 6-9)

`Asubuhi panda mbegu zako wala jioni usiuzuie mkono wako kwa maana wewe hujui ni zipi zitakazofanikiwa, kama ni hii au hii, au kama zote zitafaa sawasawa. Kweli nuru ni tamu, tena ni jambo la kupendeza macho kutazama jua. Naam, mtu akiishi miaka mingi, na aifurahie yote; lakini na azikumbuke siku sijazo za giza, kwa maana zitakuwa nyingi. Mambo yote yajayo ni ubatili. Wewe kijana, uufurahie ujana wako, na moyo wako ukuchangamshe siku za ujana, ukaziendee njia za moyo wako na katika maono ya macho yako, lakini ujue wewe ya kwamba kwa ajili ya hayo yote Mungu atakuleta hukumuni'. (Mhubiri 11: 6)

Uchungu hauwezi kustahimili katika anga ya mbinguni. Hakuna machozi tena, hakuna maombolezo na hakuna laana. Humo hamna kifo, huzuni au kulia, kwa sababu mambo ya kwanza yamekwisha kupita. Hakuna mwenyeji atakayepewa mgonjwa kwa sababu watu wakao humo watasamehewa maovu yao. (Ufunuo 21.4) (Isaya 33:24)

Pale kuna Yerusalemu mpya, mji mkuu wenye utukufu wa dunia, nchi ya watakatifu itakuwa mikononi mwa Bwana. `Nawe utakuwa taji ya uzuri katika mkono wa Bwana, na kilemba cha kifalme mkononi mwa Mungu wako'. (Isaya 62:3). `Umestahili wewe, Bwana wetu na Mungu wetu, kuupokea utukufu na heshima na uweza; kwa kuwa wewe ndiwe uliyeviumba vitu vyote na kwa sababu ya mapenzi yako vilikuwako, navyo vikaumbwa'. (Ufunuo 4:11)

Katika mji wa Mungu hakutakuwa na usiku tena. Hakuna atakayetaja kuhusu kupumzika. Hakuna mtu atakayepungukiwa kwa kufanya mapenzi ya Mungu au kutoa shukrani kwa jina lake. Tutauona uzuri wa asubuhi na hatutakuwa karibu na mwisho wake. Hawahitaji nuru wala mwangaza wa jua kwa sababu Bwana Mungu huwapa nuru (Ufunuo 22:5). Nuru ya Bwana itazidi mwangaza wa jua la mchana, lakini mwangaza huo hautakuwa na madhara yeyote kwa waliokombolewa. Utukufu wa Mungu na Mwana-kondoo utaijaza mji na mwangaza usio na kikomo, na waliokombolewa watatembea bila kuhitaji nuru ya jua. `Nami sikuona hekalu ndani yake; kwa maana Bwana Mungu Mwenyezi na Mwana-kondoo, ndio hekalu lake'. (Ufunuo 21:22) Ni pendo kwa watu wa Mungu kuwa na ushirika na Mungu, na mwanaye,

`Maana wakati wa sasa tunaona kwa kioo kwa jinsi ya fumbo; wakati ule tutaona uso kwa uso; wakati wa sasa nafahamu kwa sehemu; wakati ule nitajua sana kama mimi nami ninavyojulishwa sana'. (1 Wakorinto 13:12)

Tunatazama ufunuo wa Mungu ukimulikwa kana kwamba ni katika kioo kwa kazi yake ya uumbaji, na matendo yake pamoja na wanadamu. Lakini wakati huo tutamwona uso kwa uso bila kuwa na pasia litakalo tutenganisha. Tutasimama mbele zake na kuona utukufu wa uwepo wake.

Ushindi wa Pendo la Mungu

Hapo pendo la Mungu mwenywe alilolipanda mioyoni mwa watu, litakamilisha ushirikiano na viumbe watakatifu, na umoja wa kweli usio na kasoro, jamii yote ya mbingu na ya duniani watadumisha furaha ya milele iliyo kamilika. Waefeso 3:15 Hapa tukiwa na mawazo yetu makamilifu tutaona maajabu ya uwezo wa Mungu muumba, na ile siri ya upendo wa Ukombozi wetu. Kila kiungo kitaendelea kukuwa. Mambo makuu ya ajabu yatafunuliwa. Hata hivyo kutakuwa na mambo mengi ya ajabu ya kujua. Katika umilele na milele, kutakuwa na mafundisho yaziyo na nwisho wala hakuna kuchoka

Hazina zote za Mungu zitafunuliwa kwa wana wa Mungu waliokombolewa. Watatembea dunia zingine bila nuru na safari ya kuchosha. Wana wa nchi hii wataingia katika ulimwengu wa wasiokuwa na dhambi na kushiriki maajabu ya elimu yao isiyokuwa na kasoro, ambayo wao wamekua nayo Vizazi kwa vizazi

Wataangalia utukufu wa uumbaji bila kuwa na kisuizi machoni. Na jua na nyota na sayari zote zitakizunguka kiti cha enzi. Kadiri miaka ya milele itakavyoendelea, ndivyo ufunuo wa utukufu wa Mungu na Kristo utakavyofunuliwa kwa njia ya ajabu. Na kadiri watu watakavyojifunza tabia ya Mungu, ndivyo watazidi kumwabudu na kumpenda. Yesu atakapofunuliwa kama siri za ukombozi wetu, ndivyo tutakavyozidi kumtukuza na kumtumikia, na kumwimbia kwa sauti za watu maelfu mara elfu kumi "Na kila kiumbe kilichoko Mbinguni na juu ya nchi na chini ya bahari na vitu vyote vilivyo ndani yake, nalivizikia, vikizema, Baraka, heshima na utukufu; na uweza una yeye aketiye juu ya kiti cha enzi na yeye mwana kondoo hata milele na milele". Ufunuo 5:13

Mapambano makuu yamekoma. Dhambi na wenye dhambi hawako tena. Ulimwengu mzima sasa umesafika. Umoja na ushirika mkamilifu umeenea ulimwenguni. Kutoka kwa muumbaji ukivurika uzima, nuru na furaha na kuenea mahali pote. Tangu mdogo hata yule mkubwa katika ulimwengu kote, vitu vyote, vilivyo hai na visivyo hai; katika hali yao yote, hutangaza kuwa Mungu ni upendo. (E.G White - Pambano Kuu) (G.C pgs 674 - 678)

Jaribu linapotokea, Kama jinsi tawi linahitaji kutegemea shina, ndivyo nasi tutakwa na furaha tukiendelea kuwa na Yesu, ili tusitende dhambi. Tukitenda dhambi sisi ndio wa kulaumiwa. Yohana 14:4-5. Yesu hatakuacha uanguke, lakini tukianguka, ni lazima turudi kwa Yesu na kuushikilia mkono wake wa nguvu, kisha kutubu na kukubali dhambi zetu na kisha kupokea msamaha kwa Yesu Kristo ili tuweze kuurudisha uhusiano pamoja naye (1Yohana 2:1-2)

Kilele cha Umilele

Ishara za nyakati zinatueleza kama mtu anayepiga kelele kuu kutoka paa ya nyumba, Yesu Kristo Mwokozi wa ulimwengu yuaja hivi karibuni. Nasi bado tunaketi tukingoja nini? Tutapitia wakati mgumu huko tukipambana kati ya wema na ubaya, tunavyokaribia mwisho wa nyakati; matukio ya mwisho yatafuatana kwa haraka sana kama vile uchungu umujiapo mwanamke aliye tayari kuzaa. Sefania 1:14, Warumi 9:21, 1 Wathesalonike 5:1-3, Kutoka sasa ni muhimu kufanya uamuzi kusimama pamoja na Yesu siku baada ya siku, saa baada ya saa, dakika kwa dakika, nukta kwa nukta.

Yesu alikuja duniani kuwa mfano wetu. Yeye alikuwa ni Mungu, bali alinyenyekea mwenyewe na akaacha uungu wake ili akavaa mwili wa binadamu. Ingawa alikuwa Mungu, alikuja kama mwanadamu. (Yohana 1:1-3) Wafilipi 2:5-8) Kama mwanadamu, alituonyesha jinsi ya kuwa washindi. Kama jinsi alivyokuwa duniani na akapata ushindi kutoka kwa Mungu, na akaishi maisha yasiyo na dhambi, hata nasi twaweza kupata nguvu katika kila hitaji.

Lazima mawazo yako yatakaswe kabla ya marejeo ya pili:

Bibilia husema, hakuna machukizo yatakayokubaliwa katika ufalme wa Mungu. (Ufunuo 21-27) kwa hivyo katika marejeo ya pili, Yesu Kristo atakuja si kutuokoa katika dhambi zetu au kutakaza mawazo yetu kutokana na uchafu, la, utakazo lazima ufanyike hivi sasa, kabla Yesu hajarejea tena iwapo tutataka kumfuata atakaporudi kutuchukua pamoja naye. (1 Wathesalonike 5:17; Waefeso 1:4, 5:27) Ufunuo (7:14; 14; 1-5) Yesu alikufa kwa ajili yetu, damu yake ilimwagwa pale msalabani Kalivali kwa ajili yako na mimi. Hata hivyo, ni yeye aaminiye ambaye hatapotea bali atapata uzima wa milele. Yohana 3:16, Hebu tukubali toleo hili la neema na wokovu sasa na tumkubali ili tuishi maisha mapya.

Uwe tayari siku zote:

Hebu tujaribu wakati wote kufanya, mapenzi ya Mungu na mawazo yetu yaelekezwe mbinguni. Ndivyo tutakavyo songa mbele kutoka ushindi huu hadi ushindi mwingine katika maisha ya ukristo. Katika pambano kuu la mwisho, wale wanaozishika amri za Mungu na kuwa na imani ya Yesu hawatakubali alama ya mnyama, lakini kupitia kwa rehema za Mungu, watapokea muhuri wa Mungu katika vipaji vya nyuso zao. (Ufunuo 13:6, 14:9-10 Ezekiel 9:4, Ufunuo 7:2-4 22:14). Maombi yetu ni kwamba ziku zote uwe tayari. Ndivyo tutakavyotembea pamoja na Yesu, Mwokozi wa ulimwengu hadi makao ya mbinguni; wakati u karibu atakaporudi pamoja na malaika kuwakusanya pamoja wamwaminio. 1 Wathesalonika 4:15-17. Tunatarajia kukutana pale.

Ni mimi wako Mpendwa Abel and Bente Strusknes


[Back to the Main Page!]


This page belongs to Abel Struksnes. For more information contact Christian Information Service, Bente & Abel Struksnes, Vestrumsbygda 26, 2879 Odnes, Norway or send me an e-mail at abels@online.no