Vita na misukosuko, vurugu na mauaji, njaa na dhiki,
Vibunga, ghalika, matetemeko ya ardhi...haya si matukio mapya.
Hata hivyo, kizazi kilichoko leo kinakabiliana na changa moto mpya na ngumu; nazo ni matatizo ya kimazingara, uhandisi wa kinasaba, mabadiliko katika hali ya anga, magojwa yanayo husiana na chakula, na kadhalika. Wengi wetu pia tutaweza kutambua ya kwamba jamii yetu inajitenga na maadili fulani ya kitabia ambayo ni ya kimsingi
Wengi wamebaki huku wakijihisi kuwa wadogo na wanyonge, lakini je, si ingetupasa sis kujiuliza swali hili: Haya yote yatendeka kwa nini.
Kunayo sababu ya mabadiliko haya. Habari njema ni kwamba kunalo pia suluhisho.
Hatuzungumzii ile aina ya utatuzi ambayo siku hizi hupendekezwa na wanasiasa au viongozi wa kidini. Historia yaonyesha kuwa mara nyingi, walio wengi ndio hukosea, na pia, japokuwa kumefanywa mikataba mingi ya amani, masikilizo ya kuushirikiana pamoja na mipango yenye makusudi mema, hali kadhalika tamaa ya uongozi na ile tamaa idumuyo ndani ya moyo wa binadamu, hali yote hayatatoweka.
Yale yanayoendelea ni mapambano kati ya mema na mabaya, lakini yatakoma. Nyuma ya ukweli huu unaohusu misukosuko, kunao mpango unaotekelezwa.
Kitabu cha vitabu, yaani Bibilia, kinalo jambo la kusema kuhusu hali ya maisha ilivyo. Hasa ina kuongelesha wewe unayetafuta maelezo kamili wewe unayetaka kuyajua mambo yajayo.
Kufikia sasa,unabii wa biblia haujawahi kufeli. Kwa hivyo, twaamini kuwa unabii wa siku za mwisho utatimia pia.
Katika kitabu cha Ufunuo, twaupata mfululizo wa unabii unaoendelea kutimia sasa. Tutauangalia unabii huu kwa undani.
Katika kitabu cha Mwisho cha Biblia, yaani ufunuo, twaupata mfululizo wa unabii unaotuarifu mengi kuhusu historia, kuzihusu nyakati zetu, na pia kuzihusu siku zijazo hivi karibuni. Hapo pia twazipata jumbe tatu za kipekee kabisa ambazo zatufaa sana leo, na ambazo yatupasa tuzitilie maanani zaidi.
Waweza kuusoma ujumbe wa kwanza katika ukurasa unaofuata.
Yasema kuwa jumbe tatu hizi zapeanwa na malaika. Neno la kiyunani litumikalo kumaanisha malaika ni "angelon", maana yake mjumbe. Hivyo basi malaika hawa watatu husimamia waume na wake watendao kazi kulingana na mapenzi ya Mungu, na ambao watapeana ujumbe huu, ambao ni "injili ya milele" wa ulimwengu, kwa nguvu zao zote.
Injili Ya Milele
Je, "injili ya milele" ni nini? Jawabu limeelezwa kwa kinaganaga kwenye Biblia, katika injili ya Yohana 3:16 Hapo husema hivi;
"Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa mwana wake wa pekee, ili kila amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele "(Yohana 3:16)
Sote twaifahamu hadithi ya Biblia kuhusu Adamu na Hawa, ambao walikosa kutii na kulila tunda lililo katazwa, walikuwa tayari wamelipokea onyo, na walijua ya kwamba wangefariki nyuma ya hadithi hii inayoonekana kuwa rahisi, umefichika mkosi ambao tayari umewafikia binadamu wote, Biblia yahakikisha kuwa mshahara wa dhambi ni mauti (Warumi 6:23), na hapa huzungumzia mauti ya milele, Mungu, ambaye ndiye muumbaji wetu, ndiye chanzo cha uhai wote, hivyo basi wakati mababu zetu walipoamua kuyapuuza maonyo ya Mungu, walimwacha yeye ambaye ndiyeuhai. Lakini Mungu humpenda binadamu.
Yeye aliamua kujitwalia hukumu ya kifo inayotufaa juu yake. Alimtuma mwanawe, Yesu Kristo, ambaye alikuwa tayari kuyapitia mateso badala yetu sisi.
Japo Yesu alikuwa ni Mungu, alikuja kama binadamu (Yohana 1:13,14 na Wafilipi 2:5-8). Akiwa kama binadamu, ingempasa ajaribiwe kwa njia zote kama vile sisi. Na kwa vile angeichukua nafasi yetu, ingekuwa tu ni kwa kuishi maisha ya haki, pasipo dhambi, ili aweze kujitwalia adhabu yetu bila yake mwenyewe kuwa na hatia. Kristo aliyashinda majaribu YOTE kupitia kwa nguvu za Mungu (Wahibirania 2:17-18)
Ni yeye pekee aliyeyatenda haya.(Warumi 3:23)Hatimaye, aliutoa uhai wake msalabani ili atuweke huru wewe na mimi kutokana na mauti ya milele. Husema hivi:
"Naam, kadiri ya sheria karibu kila kitu chaweza kutakaswa kwa damu, na
dhambi nazo zaondolewa tu ikiwa damuimemwagwa"(Waebrania 9:22)
Kwa hivyo, ni juu yako wewe nami tulipokee toleo hili la Kristo kwa imani. Kama wajiona kuwa ni mwenye dhambi, waweza kujiondolea mzigo huo wa dhambi kwa kumjia Kristo. Biblia yasema:
"Lakini tukiziungama dhambi zetu, basi, Mungu ni mwaminifu na mwadilifu, naye atatusamehe dhambi zetu na kututakasa uovu wote" (1 Yohana 1:9)
Kila mmoja wetu anayekubali kuhesabiwa haki kwa imani ataokolewa. Je, sihizo ni habari njema?
Mcheni mungu na kumtukuza
Lakini maisha hayakomi wakati tunasema NDIYO kwa Yesu. Hapo, maisha yetu pamoja na Kristo huanza. Ndipo itakapoonekana maishani mwetu kuwa tumepitia kwenye mabadiliko. Biblia yasema kuwa tutabadilishwa kwa kuwa na mageuzi kamili ya nia (Warumi 12:2). Haya ndiyo yanayotendeka pale tusemapo NDIYO kwa Yesu, Roho mtakatifu akishaingia mioyoni mwetu. Hapo ndipo tutakapoyafuata maagizo ya Mungu, wala sio njia zetu wenyewe, huku tukiwezeshwa na Roho mtakatifu. Hatimaye sifa za kitabia kama vile upendo, furaha, amani, wema na urafiki zitajitokeza maishani mwetu, badala ya chuki, hasira na tamaa (Wagalatia 5:16-26).Jambo hili hatuwezi kulitimiza peke yetu, bali ni kwa msaada wa Mungu. Kwa hivyo, maana yake kumtukuza Mungu ni kushuhudia tabia yake ndani ya maisha yetu, na kwa njia hii kumfanya ajulikane kwa wale wanaotuzunguka.Yesu ametupa mfano, na sasa ni juu yetu, - huku tukisaidiwa na Mungu kuiendeleza kazi yake kwa kuidhihirisha tabia yake katika maisha yetu na mafundisho yetu (1 Petero 2:21, na Waefeso 3:10).
Kuishi pamoja na Kristo na kudhihirisha tabia yake maishani mwetu hushirikisha mambo
mengi. Yesu asema hivi:
"Mtu awaye yeyote akitaka kunifuata, lazima ajikane mwenyewe, auchukue msalaba wake, anifuate mimi". Na pia "Mkinipenda mtazishika sheria zangu" (Mathayo 16:24, na Yohana 14:15)
Mtu aliyempokea Yesu kwa imani watafurahia kuzifuata amri zake. Amri za Mungu ametupa amri hizi kumi ili tufahamu jinsi tutakavyoimarisha uhusiano wetu na Mungu, hali kadhalika sisi kwa sisi. Katika barua ya kwanza ya Yohana, twajaribiwa hivi:
"Tukizitii amri za Mungu, basi, tunaweza kuwa na hakika kwamba tunamjua. Mtu akisema kwamba anamjua, lakini hazitii amri zake, basi mtu huyo ni mwongo, na ukweli haumo ndani yake. Lakini mtu yeyote anaye shika neno la Mungu, huyo ndiye aliye na upendo kamili wa mungu ndani yake. Hivi ndivyo tunavyoweza kuwa na hakika kwamba anaungana naye; mtu yeyote anayesema kwamba ameungana na Mungu, anapashwa kuishi kama alivyoishi Yesu Kristo."(1 Yohana 2:3-6)
Kwa hivyo, kumwogopa Mungu humaanisha pia humtii Mungu.
Tukishaelewa kwa undani yale yote ambayo Mungu ameyatoa kafara ili kutuokoa sisi, itakuwa ni furaha kwetu kuzifuata amri za Mungu. Kuwa chini ya sheria hakutakuwa tena ni utumwa, bali tutatii kutokana na upendo pamoja na shukrani kwa Mungu aliyetupenda kwanza.
Yesu alipokuwa akipaa mbinguni, aliwaambia wanafunzi wake:
"Lakini wakati roho mtakatifu atakapowashukieni nyinyi, mtapokea nguvu." (matendo 1:8)
Nguvu hizo hizo twaweza kuzipata pia. Kwa hivyo, kama vile ingempasa Yesu kupewa nguvu za kuzishinda dhambi na Mungu, vivyo hivyo nasi pia twaweza kuyashinda majaribu yote yanoyotukabili (Yohana 5: 30 na 1 Wakorintho 10: 13). Mfuasi wa Kristo atakuwa sio tu msikilizaji wa neno, mbali pia mtendaji. Imani ya kweli hudhihilishwa kwa vitendo. Maisha au vitendo huambatana na mapenzi ya Mungu. (Yohana 1:22 na 2:14-26, pia 1 yohana 2:29)
Biblia yadhihilisha kuwa roho mtakatifu atapeanwa kwa wale wanaomtii Mungu (Matendo 5:32), na kuwa Roho Mtakatifu ndiye atuwezeshaye kuishi bila kutenda dhambi. Biblia yaahidi hivi:
Kila aliye mtoto waMungu hatendi dhambi, maana anayo hali ya kimungu ndani yake: hawezi kutenda dhambi kwa sababu yeye ni mtoto wa Mungu. (1 Yohana 3:9, na 2 Petero 1:4)
Tukishaiamini ahadi hii, tutapata kuwa twaupokea usaidizi wa kulishinda kila jaribu litakalotukabili.
Twatumai kuwa utaupata uzoefu huu unaohusu kushirikiana kwa nguvu za kibinadamu na za kiungu, kwani hili ni jambo ambalo yatupasa sisi sote kulifanya ili tumheshimu Mungu katika shughuli zetu mbali mbali maishani.
"Lakini" huenda utauliza, "ikiwa utausahau msaada wa Mungu na kuanguka majaribuni, la
kufanya ni nini?" Basi hapo, sisi ndio tutakaokuwa tumeusahau msaada wake, wala si yeye. Hapo litakuwa
ni jambo la muhimu kwetu sisi kumrejea Yesu na kushikamana naye. Atakuwa tayari zaidi kutupokea
na kumsamehe kila mwenye dhambi anayetubu. Roho Mtakatifu atatutembelea ili atusaidie
kuzikubali dhambi zetu, kuzitubu, kuomba msamaha na kuupokea wokovu wa yesu Kristo tena. Kama
Biblia inavyosema:
"Watoto wangu, ninawaandikieni mambo haya, kusudi msitende dhambi. Lakini, ikijatokea mtu akatenda dhambi, tunaye mmoja ambaye hutuombea kwa Baba, ndiye yesu kristo aliye mwadilifu kabisa. Kristo ndiye sadaka iondoayo dhambi zetu; wala si dhambi zetu sisi tu, bali pia dhambi za ulimwengu wote." (1 Yohana 2: 1-2)
Haya yamekuwa ni maneno ya kuchangamsha. Ikiwa wewe ni mmoja wao, yakupasa ujue kuwa yesu huwa tayari kukupokea wakati wowote. Lakini hamna njia nyingine ya wokovu. Ni lazima sisi zote tupitie kwa Yesu ili tuokolewe. Hivyo basi Yesu asema:
"Mimi ni njia, na ukweli na uhai. Hakuna awezaye kuenda kwa Baba ila kwa kupitia kwangu," (Yohana 14:6)
Kwa hivyo, kuihubiri "injili ya milele" na "kumheshimu Mungu" hujumuisha siyo tu kumpokea Yesu kama mwokozi wetu binafsi wakati mmoja fulani maishani, mbali pia tutayaishi maisha yetu tukiwa pamoja na kristo, na kuidhihirisa tabia yake maishani mwetu. Tunaposhirikiana na nguvu za mbingu kwa jinsi hii, basi tutaupokea msaada tunaouhitaji ili kuwa mshahidi walio hai kwake, na kwa neema yake tutakuwa tayari wakati Yesu atakuja hivi karibuni kuwachukuwa walio wake.
Biblia pia yatuhimiza tumheshimu Mungu kwa miili yetu. Katika 1 Wakorintho 6:19, husema:
"Je, hamjui kwamba miili yenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, ambaye mlipokea kutoka kwa Mungu? Nyinyi basi, si mali yenuwenyewe. (1 Wakorintho 6: 19-20)
Je, si hili ni jambo la kutuamsha mawazo, ya kuwa miili yetu yalinganiswa na hekalu?
Katika agano la kale, hekalu lilikuwa wakfu kwa Mungu. Kadri tuwezavyo, na huku tukiwezeswa na
Mungu, ni lazima tujaribu kuutunza mwili huu wa kupendeza ambao Mungu ametupa. Ni lazima
tuzirudie tiba za kiasili: yaani hewa safi, mwanga wa jua, mazoezi ya viungo, chakula chenye afya bora,
usafi, usingizi na pumziko la kutosha, na kumtengemea Mungu.
Hapo tutakuwa na maisha bora ya kimwili, kimawazo na kiroho.
Kule kuutunza mwili vyema kadri tuwezaavyo ni njia moja pia ya kumtukuza Muumbaji wetu, jambo ambalo yampasa kila mfuasiwa wa Kristo kulizingatia.
Sasa tutaitazama sehemu ya pili ya ujumbe huu wa kwanza, ambao leo wafaa kutangazwa kwa sauti ya juu.
Saa Ya Hukumu Yake Imefika
Biblia yasema kuwa kabla ya kurudi kwake Yesu Kristo, itakuwa tayari imeamuliwa ni akina nani watakaookolewa na watakaopotea. Kusema kweli, sisi ndio tunaoamua ni kikundi gani tutakachojiunga nacho. Biblia yatuambia ya kwamba Yesu leo ni kuhani mkuu katika hekalu ya mbinguni, ambapo anatufanyia upatanisho mbele za Mungu. Ili tuweze kuielewa huduma anayotufanyia huko, tumeupokea mfano ambao tunaweza kuutafakari: nalo ndilo hekalu la hapa duniani, ambalo habari zake twaweza kuzisoma kwenya Agano Jipya. Paulo huiita "nakala au kivuli cha mambo ya mbinguni (Waebrania 8:5). Ulikuwa tu ni mfano mdogo wa hekalu ya mbinguni. Waweza kuyasoma haya katika aya ya 8 na 9 ya Waebrania.
Katika chumba cha kwanza cha hekalu ya duniani kuhani alihudumu kila siku. Chumba hiki kilijulikana kama "pahali patakatifu" (Walawii 4). Mwishoni mwa mwaka wa hekalu-yaani mara moja kwa mwaka-katika "Siku kuu ya Upatanisho," kuhani alienda kwenye chumba cha pili; yaani "Pahali Patakatifu Mno," (Waebrania 9:7). Katika huduma ya hekalu wakati wa Agano la kale, walikuwa wameshazihamisha dhambi zao kwa mfano (kupitia kwenye damu ya mnyama anayetolewa kafara) hadi kwenye hekalu. Katika siku hii ya kipekee; yaani "Siku kuu ya Upatanisho", ilibidi hekalu lisafishwe kutokana na zile dhambi zilizohamishiwa huko. Ilikuwa ni siku ya hukumu. (Hebu soma Walawii 4 na 16). Dhambi ilisafishwa kwa njia ya mfano toka ndani ya hekalu, na muda usio mrefu baadaye wangeweza kuiadhimisha sikukuu iliyofuata, ambayo ndiyo sikukuu ya Tabenakulo. Sikukuu ya Tabenakulo ilikuwa ni sherehe ilyojumuisha hali ya furaha na kutoa shukrani.
Kwa vile huduma ya hekaluni wakati wa Agano la kale ilikuwa ni mfano tu wa yale ambayo Yesu angeyafanya baadaye katika hekalu ya mbinguni, ni jambo dhahiri kuwa lazima pia kutakuwepo na siku ya hukumu kabla ya "sikukuu ya furaha" ambayo itafanyika pale Yesu atakapoungana na watu wake.
Nabii Daniel atujulisha kuhusu hii siku ya hukumu huku "kusafishwa" au kuhesabiwa haki kwa hekalu ya Mbinguni.
Katika kitabu cha Danieli, aya ya 8, fungu la 14, twaambiwa kuwa wakati ambapo tendo hili la hukumu lingeanza ulikua tayari umeshapangwa.
Haya yaambatana na kichwa chetu "saa ya hukumu Yake imewadia" Je, "saa" muda huu wa kipekee utafika lini? Danieli aliarifiwa kuwa siku 2300 zingepita kwanza; kisha hukumu hii ingeaza.
Kwa lugha ya kinabii, siku moja mwaka mmoja (Ezekiel 4:6), kwa hivyo hapa twauzungumzia muda mrefu unaojumuisha miaka 2300.
Baadaye kidogo katika kitabu cha Daniel, twapata kujua ni wakati gani unabii huu ungeanzia (soma Daniel 9:25) nayo historia yatuarifu zaidi kuwa tukio ambalo lingeudhibitisha mwanzo huu lilifanyika wakati wa kupukutika kwa majani, mnamo mwaka wa 457 BC.
Hivyo basi tukihesabu miaka 2300 toka wakati huo (bila kuhesabu mwaka wa sifuri), twafikia kati ya miaka ya 1840. Kulingana na unabii, ni wakati huu ambapo "sikukuu ya upatanisho" ingeanza huko mbinguni.
Biblia yasema kuwa hukumu itaanza kwa wale waliojitolea kuwa wana wa Mungu. (1 Petero 4:17). Majina yao yatachunguzwa, nayo maisha yao yatajaribiwa kwa mujibu wa mwanga utokao kwenye sheria ya Mungu ambayo hupatikana kwenye chumba cha pili cha hekalu, yaani "pahali patakatifu mno" (waebrania 9:3-4).
Wakati wa Agano la kale, ili walazimu kuziungama dhambi zote kabla ya sikukuu ya upatanisho, ili waweze kupatanisha.
Vivyo hivyo, yatupasa nasi kuzianika dhambi zetu zote mbele za Mungu, ili Yesu atupatanishe. Wakati ambapo "siku ya hukumu" itakwisha huko mbinguni, nao muda wetu wa neema utakuwa umekwisha.
Haya yatatokea muda kidogo kabla ya kurudi kwake Yesu kama bwana na mwokozi wetu. Damu ya Yesu itakuwa imeweza kuwasafisha wale tu ambao watakuwa wameomba wapewe, yaani wale walioupokea msamaha kupitia kwa Yesu Kristo. Wengine wote watapotea. Japo Yesu alitamani kuwaokoa pia, hawa kuipokea zawadi ya wokovu. Siku moja watakuwa wame chelewa, na japo Mungu atawalilia, hata hivyo ili kuzingatia haki itawalazimu wahukumiwe kulingana na matendo yao.
Imeandikwa kuwa hao watateketezwa kwa moto na salfa (Ufunuo 20: 12 na 21:8).
Yesu sasa yu mbinguni (Yohana 14:1-3, na Matendo 1:8-11). Yesu ndiye mkombozi na mwokozi, lakini pia ndiye hakimu. Yeye ndiye huamua ni nani atakayeokolewa na ni nani atakayepotea. Kwa hivyo wajua ya kwamba hukumu itapitishwa kwa haki. Njia moja tu ya kupitia kwenye hukumu hii ni kuziezeka dhambi zetu juu ya Yesu.
Hakuna ajuaye ni lini Yesu ataimaliza hiyo huduma yake ya kuitekeleza hukumu kama kuhani mkuu huko hekalluni. Hapana pia ajuaye ni lini uhai wake utakoma. Kwa hivyo, hatuna muda wa kupoteza. Siku ya neema ni sasa. Sasa ndio Mungu anapokuita unyenyekee na kuziweka dhambi zako zote miguuni pake Yesu.
"Yeye anijiaye mimi, sitamtupa nje kamwe" asema Yesu. (Yohana 6:37)
Yeye yu hivyo. Waweza kumjia wakati wowote. Atakupokea na kukupa amani, yaani amani yake, amani na usalama ambazo dunia kamwe haiwezi kukupa! (Yohana 6:37), Je, ungependa kulikubali toleo hili? Ni juu yako, lakini yakupasa ujue kuwa kamwe hautajuta ikiwa utajibu NDIYO kwa hili toleo, kumbuka maneno ya Biblia.
"Basi ikiwa mwana atakufanya huru, utakuwa huru kwa kweli" (Yohana 8:36) na "popote Roho wa Bwana alipo, kunao uhuru". (2 Wakorintho 3:17).
Hebu na tu siwe watumwa wa kumtumikia shetani pamoja na ule mzigo wa dhambi ulioko maishani mwetu. Lakini, huku tukisaidiwa na Mungu, hebu na tuzikate kamba ili tuwe huru ndani ya Kristo. Hapo tutakuwa tumehama toka mautini hadi uzimani. Hebu na tuikate kauli hii sasa, ikiwa ingali siku ya neema. (mengine zaidi kuhusu ujumbe huu yapatikana kwenye kitabu kiitwacho "Vita Kuu").
sehemu ya mwisho ya ujumbe huu wa kwanza ambao sasa utatangazwa kwa sauti kuu, ya sema:
Mcheni Yeye Aliyeiumba Mbingu Na Nchi, Na Bahari, Na Chemchemi Za Maji
Biblia yatuambia ya kwamba Mungu aliziumba mbingu na nchi, bahari na vyote vilivyomo kwa siku sita, akastarehe siku ya saba. Naye Mungu akaibariki siku ya saba, akaitakasa (Mwanzo 2:1-3), katika amri ya nne kwenye Biblia, kutoka sura ya 20 mafungu ya 8-11, twaipata amri kuhusu siku ya kustarehe. Hapo twayapata mawaidha hayo ya kumcha muumbaji. Siku ya pumziko ambayo Biblia huita Sabato, imetengwa ili sisi tuweze kupata nafasi ya kumwabudu, kumwinua na kunjua mwumbaji wetu kwa njia ya kipekee. Tutamjua Mungu vyema zaidi kwa kulisoma Neno lake na pia kwa kuutafakari uumbaji wake. Japokuwa uumbaji huu sasa waendelea kuharibiwa, bado kunavyo vitu vingi vya kupendeza vinavyotuzingira. Kadri tunavyoendelea kujifundisha mengi zaidi kuhusu uumbaji wa Mungu, ndivyo tutakavyozidi kumtamani muumbaji.
Bila shaka kunavyo vitu vingi vya kupendeza kwenye uumbaji hivi kwamba mtu hupata yamempumbaza kabisa.
Hebu litazame ua, au mdudu, na mbwa, au binadamu, vyote vimeundwa vyema na ifaavyo.
Ni jambo la kuhuzunisha ya kwamba watu wengine wameanza kuwa na tashwishi kama kweli mungu ndiye muumba. Mnamo karne ya 19, Charles Darwin alilitangaza pendekezo lake kuhusu chanzo cha viumbe.
Kwa bahati mbaya, wengi wameiamini nadharia hii ya kibinadamu ya mageuko kutoka sahili kuwa tata, ambayo mara kwa mara hujipenyeza kwenye vitabu na majarida mengine yanayo somwa shuleni na vyuoni.
Hebu tusimwinue binadamu na nadharia zake za kupotosha zinazohusu mwanzo wa uhai, bali tumwinue na kumsujudu muumbaji alieumba siku sita na kustarehe siku ya saba miaka 6000 iliyopita.
Ametuumbia sisi vitu vipendezavyo ajabu. Ikiwa bado unayo mashaka kama kweli Mungu ndiye muumba, hebu yafumbe macho yako kwa siku nzima ili uelewe jinsi macho yako husaidia katika yote uyatendayo. Kwa njia hii, twaona kuna viungo vyetu vyote ni muhimu kwetu kwa kuyafanya mambo ifaavyo. Hatimaye, hebu na tumshukuru Mungu/ Yesu Kristo kwa uhai wetu. Biblia yasema hivi:
"Yeye alikuwako kabla ya vitu vyote; vyote huendelea kuwako kwa uwezo wake." (Wakolosai 1:17, Yohana 1:1-3,14 na mwanzo 1:26).
Kama kila mtu angalipata nafasi ya kumsujudu Mungu katika ile siku ambayo yeye aliitenga ili itumiwe kwa utakatifu, hakungekuwa na watu wenye nadharia ya mageuzi na wale wasioamini kwamba kuna Mungu. Mungu anao utajiri wa mibaraka kwa wale wanaomsujudu kwa Roho na kweli.
Ujumbe wa pili"Malaika wa pili alimfuata huyo wa kwanza akisema, Ameanguka! Naam, Babuloni mkuu ameanguka! Babuloni ambaye aliwapa mataifa yote wainywe divai yake divai kali ya uzinzi wake" Ufunuo 14:8
Ameaguka, Babuloni Ameaguka
Ni nani "Babuloni", "Babuloni Mkuu" na "Kahaba"?
Katika Ufunuo sura ya 17, "kahaba" ameelezwa. Anazo sifa nyingi zilizoelezwa, hivyo itakuwa ni rahisi kumtambua. Usikiapo jambo hili mara ya kwanza, huenda ukaichukulia hii kuwa ni lugha kali, lakini hata hivyo: alama zote za kutambulisha katika Biblia zaingiana na Kanisa Katoliki. Bila shaka kunao washiriki wengi wa kanisa hili ambao ni wazuri, wasio na hatia, na si kusudi letu kuwanasa. Lakini twajihisi kuwa tunao mwito wa kuwaonya wao, pamoja na wengineo dhidi ya mfumo huo, hali kadhalika mafundisho ambayo mfumo umejengwa juu yake. Usuli ya onyo hili ni amri ya Biblia, na pia ya kwamba hatuwezi, hali kadhalika kwa sababu ishara na alama za kumtambua yule "Kahaba" kwa mujibu wa biblia zaingiana na utawala huu (Ufunuo 17:5).
Mojawapo ya ishara hizi ni:
Alikuwa ameandikwa juu ya paji la uso wake jina la fumbo: "Babuloni mkuu, mama wa wazinzi na wa mambo yote ya kuchukiza sana duniani" (Ufunuo 17:5)
Kanisa katoliki hujiita mama wamakanisa. Katika barua waliotumiwa maaskofu wote wa ulimwengu, Cardinal Joseph Ratzinger aliandika hivi:
"Yapasa izidi kueleweka waziwazi ya kwamba kanisa moja lilio takatifu, la kikatoliki na la mitume linalozaa dunia nzima, hilo sio dada bali ni mama wa makanisa yote" (Daily telegraph, September 4, 2000).
Matangazo ya aina hii huchangia kuhakikisha ya kwamba kanisa katoliki ndilo linalo utimiza unabii wa Ufunuo 17:5.
Ujumbe wa pili umeelezea pia hali ya kuogofya katika ulimwengu wa kidini. Biblia ya funua kuwa yule "kahaba" au "Babeli Mkuu", ata utongoza ulimwengu kupitia kwenye mafundisho yake yasiyo ya kibiblia, yaani ule mvinyo wake unaolevya. Pengine udanganyifu mkuu sana ambao kanisa katoliki imewahi kuufanya kwa miaka mingi ni kule kuzibadilisha amri kumi za Mungu kama tuzisomavyo katika Kutoka aya ya 20, mafungu ya 3-17. Kwa bahati mbaya, makanisa ya Lutheri yamezikubali amri hizi bandia kwenye katekisimu zao, nao wamewatongoza watu kwa amri hizi bandia. (Tutayajadili haya baadaye chini ya kichwa hiki. "Mhuri wa Mungu na alama ya mnyama").
Mvinyo wa Babeli Unaolevya
Kanisa katoliki, yaani yule "kahaba" (Ufunuo 17:5)pia limeyatanguliza mafundisho mengine mengi yasiyo ya Biblia, kama vile ibada ya Bikira Mariamu, Hali kadhalika fundisho la kutokufa kwa Roho ya binadamu, ambalo pia hupatikana kati ya mafundisho ya Kizazi Kipya na ya wanaoamini katika kuwasiliana na mapepo. Leo hii, makanisa kadhaa wameyakubali mafundisho yanayohusu mawasiliano ya mapepo. Imani hii ya mizimu huyafungulia mlango mapepo yatakayo kupoteza, kwa mafundisho ambayo chanzo chake ni zile nguvu za uovu. Adhari za malaika waovu zitaendelea kubainika katika makanisa tofauti tunapokaribia mwisho wa nyakati (Kumbukumbu 18:10-12, na 2 Wathesalonike 2:9).Soma zaidi kuhusu haya kwenye kijitabu kiitwacho "Vizuka vya Mariamu".
* Komunyo
Kanisa katoliki hufundisha kuwa mkate na divai hubadilika na kuwa mwili na damu ya Yesu hasa, wakati ambapo kuhani huviinua na kuvibariki, na ya kwamba wao humtoa kafara ("humwua) Yesu upya walao mkate na kunywa divai. Kwa hivyo hujulikana kama kafara ya misa takatifu. Hii ni mojawapo ya ibada zinazoudhi ambazo kanisa katoliki imezitanguliza. Kinyume na hayo, Biblia husema kuwa Yesu alitolewa kafara mara moja, na kwamba komunyo utakuwa ni ukumbusho wa yale aliyoyatenda Yesu ili atuokoe (Waebrania 9:24-28 na/ Wakorintho 11:23-26)
Kunazo ishara nyingi zinazoonyesha kuwa waprotestanti walioasi pia wata ikubali komunyo hii ya kikatoliki hivi karibuni.
* Maazimio Ya Pamoja
Tumetaja kwa kifupi baadhi ya udangnyifu (au mvinyo unaolevya) ambao umepenya kidogo kidogo na kuingia ndani ya makanisa mengine. Lilikuwa ni jambo la kusikitisha pale shirikisho la Walutheri Duniani na Kanisa Katoliki, mnamo Octomba 31, 2000, walipatia sahihi azimio la pamoja kuhusu mafundisho yanayo angazia kuhesabiwa haki. Washiriki wengi katika kanisa la Kirutheri hata hawana habari ni yapi yaliyokusudiwa kwenye makubaliano haya, kwani uamuzi huu uliafikiwa na viongozi wenye uwezo katika makanisa hayo kufuatia mikutano ya wanachama bila ya watu kujua. Azimio hili pamoja husema, baadhi ya mambo mengine, ya kwamba sisi ni wenye dhambi, na wakati huohuo watakatifu. Lakini Biblia yasema kuwa bora tuwe tumeikubali haki ya Yesu, sisi sio wenye dhambi tena, bali sisi ni wenye haki (1 Yohana 1:9).
Isitoshe, kama tungalikuwa wenye dhambi saa zote, hakuna mtu ambaye angeokolewa. Kwani Biblia yasema kuwa hakuna kichafu kitakachoingia kwenye ufalme wa Mungu, naye Yesu alikuja kumwokoa binadamu toka dhambini, bali sio ndani ya dhambi (Ufunuo 21:27 na Mathayo 1:21).
* Haki Kupitia Kwenye Sakaramenti?
"Azimio la Pamoja" pia husema kuwa waumini wanayo haki kabisa, kwa sababu Mungu huwasamehe kupitia kwenye neno na sakaramenti. Lakini, hatuwezi kuupokea msamaha na kuwa wenye haki kutokana na matendo yetu (yaani sakaramenti). Huu ni ukatoliki, na chanzo chake lilikuwa ni Baraza la Trent mnamo karne ya 16. Kwa nini Walutheri wanarudi Roma kuhusu swala hili muhimu? Ubatizo na komunyo, ambazo ni baadhi ya hizo waziitazo sakaramenti, ni mifano tu. Hatufai kutia chochote kati yetu na Kristo ili eti tujiokoe au tuipate haki. Ni pale tu tuendapo kwa Yesu Kristo kuzipeleka dhambi zetu ambapo hufanywa wenye haki.
* Kuwanyunyizia maji watoto wachanga
Hilo "Azimio la Pamoja" kadhalika husema kuwa "ni kwa kusikia na kuamini ambapo mtu huhesabiwa haki kupitia ubatizo" Twajua ya kwamba ni kwa kuwanyunyizia watoto wachanga maji vichwani ambapo wao hupata tikiti ya kuingia kwenye makanisa ya Kikatoliki na ya Kilutheri. Lakini mtoto hawezi kuamini chochote akiwa peke yake. Pia, haifai watu wengine kuamini jambo kwa niaba yako. Biblia yasema Kuwa imani huja baada ya Neno la Mungu kuhubiriwa, na kuwa yeyote ambaye
huamini na kubatizwa ataokolewa (Warumi 10: 17 na Mariko 16: 16). Ubatizo ni agano njema la dhamari kati ya Mungu na binadamu (1 Peter 3: 21), lakini mtoto mchanga hawezi kuelewa maana ya angano hilo. Itambidi mtu yeyote kwanza kuisikia Injili , kisha aamue ikiwa ataingia kwenye mkataba huu wa dhamili pamoja na Mungu au la. Isitoshe ubatizo wa Bibilia ni kuzikwa ndani ya maji, ambapo mtu huyazika maisha ya zamani kwa mfano tu, na kufufuka katika maisha mapya pamoja na Yesu Kristo (Warumi 6: 3- 6).
* Charta oecumenica
"Azimio La Pamoja" ni hati ya kutatanisha, wala sio "asema Bwana ". Hivi majuzi, mashirika makubwa ya Kikatoliki na Kilutheri huko Uropa, nao ndio CEC (yaani Kongamano la Makanisa ya Uropa) na CCEE (Kongamano la Maaskofu wa Kikatoliki huko Uropa), wote walikusanyika pamoja ili kuiandaa hati ya pamoja iitwayo Charta Oecumenica . kwa mambo mengi, hati hii yafanana sana na ile mipango iliyofanywa na kanisa Katoliki pamoja na kundi la Wajesuti mnamo 1995. (yaani Toka kwenye Kongamano la Wajesuti 1995). Kumbukumbu za mkutano huu zaonyesha kuwa hao watajitahidi kuyaunganisha makanisa. Tena wanataka muungano huu uwe chini ya Kanisa Katoliki. Katika Charta Oecumenica, karibu umerudiwa mpango huo huo. Yasema hivi "Hadi pale tutakapolifikia lengo letu ambaloni Ushirikiano mkamilifu wa kanisa, twakusudia kufanya kazi pamoja katika mambo yale yasiyohusisha kuhitilafiana kwingi kwa imani ambako kwaweza kutu lazimu kutenda mambo katika hali ya kutengana ". ili kuyaafikia haya, wataingia katika MAJADILIANO pamoja makanisa yale mengine, ambapo hayo makanisa yatawajulisha kuhusu imani zao. Baadaye, watajaribu kuyakusanya yale wanayoyaamini kwa pamoja, na kuyaepuka yale yanayohushisha mabishano. Lakini mfuasi wa kweli wa Yesu huuchukua huo ukweli unotatanisha, na kumwomba Mungu amsaidie kuingiana na mapenzi ya Mungu katika nyanja zote.
Hiyo Charta Ecumenica pia itafanya kazi ili "kuyakuza masomo ya ki-ekumeni katika elimu ya Kikristo na katika mafunzo ya thiologia na katika elimu ya juu". Je, tutawezaje kuwakinga vijana wetu dhidi ya ushawishi huu mkuu wenye asili ya ki-ekumeni na kikatoliki?
Charta Oecumenica yapendekeza "Uinjilisti wa pamoja huko Uropa" na hawatahubiriwa ili "kuwaiba " watu toka kwenye makanisa mengine. Ikiwa mbinu hii itafuatwa, uhuru wa kuhubiri na kuwaita watu watoke "Babeli" utatoweka. Yatupasha kuonya vikali kuhusu haya! Charta Oecumenica itauhatarisha uhuru wa kuabudu! Twaelekea katika nyakati ngumu kabisa! Ni dhahiri kwamba hawa wanayapendelea makundi yaliyo makubwa katika Ukristo, ndiposa husema kuwa ni jambo la muhimu kutofautisha kati ya madhehebu na makanisa. Hebu badala yake na tujiunge naye Paulo, ambaye aliifuata njia waliyoitaja kuwa ni dhehebu (Matendo 24:14), badala yetu kuwaachilia hawa wenye madaraka kutufunganisha na mpango wao wa kiekumeni na kikatoliki (soma zaidi kuhusu jambo hili kwenye kijitabu kiitwacho Charta Oecumenica).
Mabinti Wa Makahba
Hapa twona kuwa makanisa ya Kilutheri pamoja na makanisa mengine ambao hufanya makubalioano na kutia sahihi kwenye maazimio ya pamoja na kanisa Katoliki, na ambao huyashikilia mafundisho ya uongo kuhusu mambo muhimu, wamekuwa "Mabinti wa Makahaba", kama Biblia inavyoelezea katika Ufunuo 17:5.
Twayapata maneno "Babeli" na "Mnara wa Babeli" katika kitabu cha Mwanzo, sura ya 10 na 11. Nimrod alikuwa ni mtawala, na ni chini ya utawala wake ambapo waliunjenga ule Mnara wa Babeli. Hapo mwanzo, "Babeli" ilikuwa na maana sawa na ile hali ya uasi dhidi ya mamlaka ya Mungu. Binadamu aliutwaa uongozi uliokuwa wa Mungu pekee. Kwa jinsi hii, "Babeli" akawa mama wa dini zote bandia, nayo dini yao ni hii iliyofundisha ya kwamba wangeokolewa kupitia kwa matendo yao wenyewe. Kulikuwa na utovu wa uungu, kujitwalia mamlaka na hali ya kuchanganyikiwa. Ndiposa twalinganisha "Babeli" na kuchanganyikiwa. Neno "Babeli" humaanisha kuchanganyikiwa.
Mji wa Babeli, uliokuwepo miaka 600 kabla ya Kristo, pia ulikuwa na aina kama hizi za uasi na kuchanganyikiwa. "Utawala wa dunia" huu uliwadhulumu watu wa Mungu, nay Biblia huwaamuru watu wa nyakati hizo hivi:
"Kimbieni kutoka Babuloni, kila mtu naayaokoe maisha yake! Msiangamizwe katika adhabu yake, maana huu ndio wakati wa Mungu wa kulipa kisasi, Anaiadhibu Babuloni kama inavyostahili" na pia "Tulijaribu kuuponya Babuloni, lakini hawezi kupoanywa " (Yelemia 51: 6 + 9).
Katika maneno haya "Umeanguka, Babuloni umeanguka" (Ufunuo 14: 8) "Babuloni" imetumika kama mfano. Huzungumzia juu ya makanisa ambayo wakati mmoja yaliufahamu ukweli, lakini sasa yameanguka. Ni dhihirisho la utovu wa kiroho ambao tayari umefanyika miongoni mwa wakristo. Mungu anawashtaki na kuwakemea wakristo hawa walioasi. Makanisa ya Kilutheri ni kielelezo kamili cha haya. Martin Luther aliongoza kwenye matengenezo makuu zaidi dhidi ya nguvu za upapa katika wakati wake, lakini leo kanisa la Lutheri limeshirikiana na Roma katika maswala kadhaa muhimu. Tayari tumetoa mifano kadhaa, lakini hivi karibuni utaona jinsi uasi huo ulivyoenea kwa upana. Hivyo basi Babuloni yaelezea vile kusanyiko bandia ambalo litaongoza wakati wa dunia hii. Kusanyiko hili bandia la Kibabuloni ndilo kanisa Katoliki, kwani linalo alama za kutabulisha sawa na zile ilizokuwa nazo Babuloni ya kale. Makanisa ya Kilutheri yamekuwa yakifanana na "Babuloni" hatua kwa hatua, hadi sasa wamekuwa sehemu ya "Babuloni" Biblia yaashiria kuwa mwanguko huo utakuwa mkuu, kwa kanisa Kikatoliki na pia kwa Walutheri . Hali kadhalika kwa wale wote wafuatao njia hiyo hiyo . Yatadhihirishwa hivi karibuni.
Japokuwa makanisa ya kibabeli yamekumbwa na giza la kiroho na pia kutengana na
Mungu, sehemu kubwa y a wafuasi wa Kristo wapatikana mumo humo. Wengi wao bado
hawajayafumbua macho yao ili kuufahamu ukweli huu wa nyakati hizi. Kunao wachache wasioridhika,
ambao wanatumaini kuona mwangaza zaidi. Hawa wanaitafuta sana sura ya Kristo kwenye
makanisa wanayohudhuria, bila mafanikio. Huku makanisa haya yakiendelea kutanga mbali na ukweli,
na kujifunganisha na ulimwengu, polepole, hatua kwa hatua, tofauti kati ya vikundi hivi viwili
itaendelea kudhihirika. Hatimaye kutakuwa na utengo kamili. Wakati unakaribia ambapo wao
wampendao Mungu zaidi ya mengine yote hawataweza tena kushiriki pamoja na wale walio na ...
"mfano wa uungu lakini pasipo nguvu zake" (2 Ti. 3:5)
Shauri la Biblia kwetu, sisi katika nyakati hizi za mwisho ni wazi kabisa:
TOKENI NDANI YAKE, WATUWANGU (Ufu. 18. 1-4)
Umoja Ndani Ya Kristo
Harakati za ekumeni hujaribu, kupitia kwenye maafikiano na utawala wa wengi, kuyafanya makubaliano kuhusu maswala kadhaa ambayo hayahusishi mabishano mengi, na kuyaacha yale ambayo yanaleta ubishi. Hata hivyo, Biblia yasema kwamba neno la Mungu ndilo linalofaa kutuonyesha njia. Ni kwa namna hiyo tu ambapo tutaufikia ule wa kweli.
Biblia hupendekeza umoja, lakini umoja huu ni lazima uwe umejegwa juu ya msingi dhabiti wa Biblia na sharti kuwe na umoja ndani ya Kristo.
Yesu huuelezea namna hii:
"kusudi wote kitu kimoja kama vile wewe baba, ulivyo ndani yangu, nami ndani yako, ili wawe kitu kimoja ndani yetu" (Yohana 17: 21-23)
Watoto wote wa Mungu watasimama pamoja ili kuafikia umoja ndani na pamoja na Kristo. Umoja utafika kulingana na kile kipimo alichokiweka Mungu, ambavyo mara nyingi haviwi juu ya msingi wa "asema Bwana "
Tokeni Babeli
Biblia huelezea hali ya mambo yatakavyokuwa nyakati za mwisho hivi:
"maana mataifa yote yalileweshwa kwa divai kali ya uzinzi wake, nao wafalme wa dunia wamefanya uzinzi naye, nao wafanya biashara wa dunia wametajirika kutokana na anasa zake zisiso na kipimo " (Ufunuo 18: 13)
Hii ni hali ya kutatanisha, hata hivyo kunayo nuru gizani. Mungu angali ana watu wake huko " Babuloni, " nao wataipokea changamoto kubwa hasa nyakati hizi za mwisho. Kundi fulani litaibuka, ambalo lafananishwa na malaika. Nao litazitangaza dhambi za " babeli " kwa sauti kuu. Ujumbe wenyewe ni:
"Ondokeni kwake, watu wangu, ili mshirikiane naye katika dhambi zake, msije mkaipata adhabu yake" (Ufunuo 18:4)
Tangazo hili, pamoja na ule " ujumbe wa malaika wa tatu, " ndilo onyo la mwisho kwa wanadamu. Iwapo wewe hujichukulia kwa sehemu ya watu wa Mungu, yakupasa ulikubali onyo hili, ukajiepushe na ushawishi wa e kumeni.
Hatimaye hatautazama ule ujumbe wa mwisho ambao wanuiwa kutangazwa sasa hivi , yaani muda mfupi kabla ya kuisha kwa wakati tuliopewa wa rehema na kabla ya kurudi kwa Yesu.
Ujumbe wa tatu"Na malaika wa tatu aliwafuata hao wawili akisema kwa sauti kubwa, " yeyote anayemwabudu yule mnyama na sanamu yake na kukubali kutiwa alama yake juu ya paji la uso wake au juu ya mkono wake, yeye mwenyewe atakunywa divai ya ghadhabu ya Mungu ambayo imemiminwa katika kikombe cha gharabu yake bila kuchanganywa na maji. Mtu huyo atateseka ndani ya kuchanganywa na maji. Mtu huyo atateseka ndani yamoto wa madini ya kiberiti mbele ya malaika watakatifu na mbele ya mwana kondoo. Moshi wa moto unaowatesa hupanda juu milele na milele. Watu hao waliomwabudu huyo mnyama na sanamu yake na kutiwa alama ya jina lake, hawatakuwa na nafuu yeyote usiku na mchana. Hapa ndipo penye subira wa watakatifu wale wazishikao amri za Mungu, na imani ya Yesu. " Ufunuo 14: 9 12
Mhuri wa Mungu au Alama ya Mnyama
"Alama ya mnyama " ama " alama ya Mungu " ndilo chaguo litakalokuwepo nyakati za mwisho. Lahusu uamuzi kati ya kumtii Mungu au binadamu. Mungu ametukabidhi muhuri au alama yake ndani ya ile amri yake inayohusu siku ya kustarehe. Muhuri hushirukisha jina la mpaji wa sheria, madaraka yake na hatimaye milki yake, amri inayohusu siku ya kustarehe yasema hivi:
"Ikumbuke siku ya sabato ukaitakase, siku sita fanya kazi na utende mambo yako
yote. Lakini siku ya saba ni sabato ya mwenyeji Mungu, Mungu wako, siku
hiyo usifanye kazi yeyote, wewe wala mwanao, wala binti yako, wala mtumwa wako,
wala watumishi wako wa kike, wala mnyama wako wa kufungwa wala mgeni aliye
nyumbani mwako, maana kwa siku sita mimi mwenyeji Mungu niliziumba mbingu na
dunia, bahari na vyote vilivyomo, kisha nikapumzika siku ya saba,kwa hiyo mimi
mwenyeji Mungu niliibariki siku yasabato, nikaitakasa. ( kutoka 20:8-11 )
Hapa yasema kuwa jina la mpaji wa sheria ni " Bwana " na madaraka ya huyu mpaji wa sheria ni yule " aliyeumba " (yaani muubaji ) nayo milki ya utawala wake ni " mbingu na nchi na bahari, na vyote vilivyomo." Kanisa Katoliki limekiondoa kifungu hiki cha maneno kutoka kwenye amri kwa majibu wa katekisimu yaani, kifungu kinachodhihirisha kuwa Mungu ndiye mtunzi wa sheria kimeondolewa.
Wakishafanya hivyo, wanajitwalia uhuru kwa kujifanya watunzi wa sheria wenyewe, kisha wakazibadili amri na kuzifanya kama tunavyoona kwenye katekisimu yao.
Nabii Daniel aliwahi kuandika kuhusu kuibuka kwa dini fulani (Daniel 7:25). Japokuwa upapa umeshautimiza unabii huu tayari kwa kule kuzibadili amri kumi za Mungu kwa mjibu wa katekisimu, hata hivyo amri za Mungu zingali halali. Yesu asema hivi:
"Msidhani kuwa nimekuja kutangua sheria na mafundisho ya mnabii. Sikuja kutangua bali kutimiza. Kweli nawambieni, mpaka hapo mbingu na dunia zitakapopita, hakuna hata nukta moja au sehemu ndogo kabisa ya sheria itakayoondolewa, mpaka yote yametimia. (Mathayo 5: 17-18)
Kanisa katoliki limeondoa sio tu sehemu kubwa ya lile fungu linalozungumziasiku ya pumziko katika amri, bali pia maneno yanayotuamuru kumwabudu Mungu katika siku ya saba kulingana na Biblia. Wala sio jumapili, ambayo Biblia huitaja kuwa siku ya kwanza juma. Kwa bahati mbaya, kanisa la Kilutheri limekuwa likizifuata nyayo za kanisa katoliki. Hivyo basi waweza tu kukipata kifungu kifupi cha maneno kifuatacho ndani ya katekisimu ya Lutheri "itakase siku ya pumziko". Hapa haujajurishwa ni gani siku ya pumziko bandia, aliyoianzisha binadamu, wala sio iku ya kustarehe ya Biblia.
Mageuzi siku ya pumziko toka sabato hadi jumapili yalifanyika zaidi ya miaka elfu kabla ya waleashujaa au matengenezo. Leo hii, wachache tu wafahamu kuhusu undanganyifu huu, na wengi hutunza jumapili kama siku ya pumziko pasipo nia mbaya, huku wakiamini kuwa hiyo ndiyo siku ya starehe kulingana na Biblia. Lakini hapa ndipo makuhani na wachungaji wamewahadaa watu, huku wakikataa kulihubiri Neno kwa uzazi na usafi jinsi lilivyo kwenye maandiko matakatifu.
Sabato ni Siku Gani?
"Lakini siku ya saba ni gani kulingana na Biblia? " huenda utauliza. Kuambatana na kifo cha Yesu, na mazishi, na kufufuka kwake, Biblia huitaja siku aliyofariki Yesu kuwa "siku maandalizi" au "siku inayoitangulia sabato". Pia hujulikana na wengi kama Ijumaa njema, siku ambayo Yesu alifufuka toka kabulini huitwa siku ya kwanza ya Juma, yaani Jumapili kwa lugha ya kisasa. Siku iliyokatikati ya hizi mbili huitwa "sabato" "siku ya saba" yani Jumamosi. Yesu, aliye Bwana wa sabato, alipumzika kaburini mnamo Jumamosi, kisha akafufuka kuikabili siku mpya ya kazi, yaani Jumapili kwa hivyo jumapili kulingana na Biblia ndiyo siku ya mwanzo wa zile siku sita za kazi katika juma.
Katika Biblia, siku huanzia machweo hadi machweo (Mwanzo 1: 14-19, Walawii 23:23, Nehemia 13:16-21, Luka 23: 54-56). Hivyo basi siku ya saba kulingana na Biblia, yaani sabato, huanzia machweo Ijumaa na kumalizika machweo jumamosi.
Leo hii, kanisa katoliki pamoja na baadhi yamakanisa ya Kiprotestanti huita jumapili " siku ya Bwana " (15,58:13) kwa hivyo " siku ya Bwana " siyo jumapili, bali ni sabato.
Diies Domini
Papa Yohana Paulo wa pili , katika barua yake ya uchungaji "Dies Domini" ya Mai 1998, ametambua ya kwamba sabato ndiyo siku asili ya pumziko ya Mungu, lakini asema, bila ya kuona haya, ya kuwa "Wakristo, ambao wameitwa ili kutangaza uhuru uliyoshindaniwa na damu ya Kristo, walihisi kuwa wanayo mamlaka ya kuihamisha maana ya sabato hadi kwenye siku ya ufufuo" Papa pia anauzungumzia "utajiri wa kiroho na wa kiuchungaji uliomo ndani ya jumapili, kama ilivyokabidhiwa kwetu na utamaduni." Papa asema kuwa walihisi kuwa wanayo mamlaka ya kuyatekeleza mabadiliko haya, na pia aanakubali ya kuwa kuwepo kwa jumapili kama siku ya pumziko kutokana na utamaduni.
"Jumapili ni ya wakatoliki, na pendekezo lao eti kuwa itakaswe laweza tu kutetewa kuambatana na imani ya kikatoliki." (The Catholic Press, Sydney, Australia, August 1900)
Sasa ni dhahiri kuwa zile ishara zote zilizotolewa na Biblia za kumtambua Mpinga Kristo, iloisemekana pia vivyo hivyo katika lile azimio liitwalo "Augsburg Confession of Belief." ukurasa 5: 39
Tumeona jinsi kanisa katoliki lililouondoa ule mhuri wa Mungu au alama yake toka kwenye amri zake, kama isemavyo katika katekisimu yao, na ya kwamba wao huendelea kusema, kwenye jumbe zao mbali
mbali, ya kuwa jumapili ndiyo alama yao ya mamlaka, na kuwa wengi wao huyatambua mamlaka ya kanisa lao hili kwa kule kuitakasa Jumapili (H.F. Thomas, chancellor of Cardinal Gibbons, and the Donay Catechism, P, 59)
Komunyo Na Utunzaji Wa Jumapili
Katika ile baruayake ya uchugaji itwayo Dies Domini, Papa Yohana Paulo wa pili anawahimiza makasisi kupeana komunyo ya kikatoliki kila jumapili. Maana yake ni kuwa aliwaambia watuwazitangulize tamaduni mbili zisizo za Kibiblia kwa pamoja, nazo twaweza kuona waziwazi jinsi mambo yanavyoendelea kukomaa, kama vile papa asemavyo katika barua yake iliyochapishwa mnamo Mai 28, 1998, ya kuwa mtu awaye yeyote atakayekataa kuzitumikia sera za kikatoliki, "ataadhibiwa kama mwasi."Maneno haya ni sawa na upepo mwovu uvumao toka enzi za kale. Lakini usiwe na hofu. Yeyote anayeongozwa na Kristo, anaye mmoja aliye mwenye nguvu zaidi kwa upande wake, naye atawapa watoto wake nguvu tosha za kushinda, japo watakabiliana na vitisho pamoja na mateso.
Hesabu Ya Mnyama
Katika kijitabu kiitwacho, "Watch out for the power Elite and the Global Union!" twazipata alama 16 za kumtabulisha "mnyama." Alama zote hizi zaingiana na kanisa katoliki, hali kadhalika ile hesabu ya mnyama, yaani 666. Biblia yasema kuwa hii ni NAMBARI YA MTU FULANI, wala sio namba ya tarakimu fulani zenye mafumbo. Wale wanaopendekeza kuwa alama ya mnyama ni mfumo watarakimu hizo wanawapotosha watu. Hayo hayana uhusiano wowote na alama ya mnyama. Hata hivyo, yawezekana kuwa mfumo huo unaohusisha nguvu za umeme huenda ukatumiwa kwa kuwatabulisha watu, na kuhakikisha kuwa wale wanaokataa kuipokea alama hiyo ya mnyama hataweza kununua wala kuuza.
Lakini hebu tuirejelee namba ya mnyama Biblia yasema kuwa hiini namba ya mtu fulani. Naye ni nani?
Papa wote huwa na jina fulani la heshima, nalo ndilo VICARIUS FILII DEI, maana yake " mwakilishi wa mwana Mungu " hapa duniani. (soma Our Sunday Visitor, Catholic Weekly, Bureua of Investigation, Hunington, India 18th April 1915 ). Herufi za Kilatini huwa na maana fulani ya tarakimu, hivyo basi ukizilinganisha herufi hizi na hizo numerali, utapata 666. ( V na U = 5, I = 1, C = 100, A = 0, R = 0, S = 0, L = 50, D = 500, E = 0, ). Jumla ni 666.
"Hesabu ya mnyama," "alama ya mnyama" na "sanamu ya mnyama," hizi ni alama tatu tu miongoni mwa zingine nyingi zitumikazo kutambua huyo " mnyama. " Alama zote lazima ziingiano utawala fulani, nazo huingiana na utawala wa Upapa. Luther na mashujaa wengine wa matengenezo hawakukosa pale waliposema kuwa "Papa anazo alama zinazo mtabulisha mpinga Kristo,"
Kweney Kipaji Au Mkono
Biblia yasema kuwa alama ya mnyama itapokelewa kwenye kipaji au mkono. Yasema hivi:
"Naye awalazimisha wote, wadogo kwa wakubwa, matajiri na maskini, watu huru na watumwa, watiwe alama juu ya mikono yao ya kulia au ya juu ya paji za nyuso zao, na pia mtu yeyote asiweze kununua au kuuza kitu isipokuwa tu mtu aliyetiwa alama hiyo, au jina la yule mnyama, au tarakimu ya jina hilo. (ufunuo 13: 16 17)
Hapa Biblia yajielezea yenyewe, huku ikisema kuwa kipaji chahusiana na kichwa pamoja na mawazo, nao mkono wahusiana na matendo (soma kumbukumbu 6:6-9 na kutoka 13: 8-10)
Wakati wa alama ya mnyama ukishawadia, wale ambao watakuwa wameshaambiwa na kuelewa haya yote, lakini wakachagua mawazoni, mwao kuitunza amri ya upapa ya jumapili, wataipokea vipajini mwao. Wale watakaoipokea alama mikononi mwao, hudhihirisha kwa mikono na matendo
chaguo lao ni lipi. Hufanya kazi siku ya sabato ya Bwana, huku wakiipumzisha mikono yao siku ya sabato bandia, wote wawili hawa huipokea " alama ya mnyama"
Kwa kifupi, kuipokea alama ya mnyama maana yake ni kwamba mtu huyo amefanta uamuzi sawa na ule alioufanya yule MNYAMA, na atazitetea hisia hizo hizo hizo japo zapingana na neno la Mungu.
Japokuwa watu wengi wanaipokea ishara hii ya utiifu kwa utawala wa kidunia na njia hiyo hupokea " alama ya mnyama " kipo kikundi idogo cha watu waliochagua kumtumikia Mungu, na kumkubali awe mtawala wao, hivyo basi wameupokea " mhuri wa Mungu ."
Kwa wale watakapoikea "alama ya mnyama ," onyo hii latolewa toka mbinguni:
"yeyote anayemwabudu yule mnyama na sanamu yake na kukubali kutiwa alama yake juu ya pajila uso wake au juu ya mkono wake, yeye mwenyewe atakunywa divai ya ghadhabu ya Mungu ambayo imeminwa katika kikombe cha ghadhabu yake bila kuchanganywa na maji."(ufunuo 14 : 910)
"Lakini hakuna atakayeangukiwa na ghadhabu ya Mungu hadi pale ukweli utakapokatiliwa baada ya kusukumiwa kwenye mawazo dhamiri yake. Wapo wengi ambao bado hawajapata nafasi ya kuusikiliza ukweli huu wa kipekee kuhusu nyakati hizi. Jukumu la kuitii amri ya nne haijawahi kufikishwa kwao katika ile nuru kufikishwa kwao katika ile nuru ya kweli. Yeye asomaye kila moyo, achunguzaye nia zote, hatamwachilia yeyote anayetamani kuujua ukweli kudanganywa kuhusu pambano hili. Amri hii hawapasi kusukumia watiu kwa njia ya upofu. Kila mmoja atapata nuru tosha ili aweze kufanya uamuzi baada ya kutafakali kwa makini" ( The Great Controversy; p, 605 )
Kwa bahati mbaya, watu wengi zaidi watashindwa pale wakapobanwa na serikali hadi waipokee alama ya mnyama, huku wakiogopa kupoteza kazi zao au kuishi bila chakula na nguo. Lakini mfuasi halisi wa Kristo atakuwa na hakikisho ya kuwa Mungu atamuwezesha kupitia kwenye hatari wakati itakapowadia.
Utachagua Utawala Gani?
Katika kijitabu hiki, umepewa nafasi ya kuchagua ni mtawala gani utakaomfuata Yesu aliyesimamisha sabato (Jumamosi ) au upapa, ambao hupendekeza kuitakaza jumapili, kuhusu jambo hili, tutatoa maelezo zaidi.Yesu alihusika kwenye uumbaji Biblia yasema "vitu vyote viliumbwa na yeye" (Yohana 1 : 1-3, 14 ). Alishiriki katika kuisimamisha sabato, nayo Biblia husema ya kwamba Yesu ndiye Bwana wa sabato (Mariko 2 : 28 ). Kwa hivyo, kama angalihitajika mtu wa kuibadilisha sabato, bila shaka angalikuwa ni Yesu. Lakini je, waweza kulipata neno hata moja kutoka kinywani mwa Yesu linalotushauri kuacha kuitunza sabato na kwanza kuitunza Jumapili kama siku ya kustarehe ? Tulishasoma hapo awali ya kwamba hakuna herufi hata moja itakayotolewa kwenye sheria. Biblia pia husema kuwa .
"Yesu kristo ni yule yule jana, leo na milele." (Waebrania 13: 8)
Hapa twaambiwa kuwa amri za Mungu zingali za simama, ikiwemo amri za sabato.
Kwa hivyo swali ni hili; utamchagua mtawala gani ; wale wanaoifuata amri ya kibinadamu pamoja na jumapili kama siku ya pumziko, au Mungu na siku yake ya pumziko ambayo ni sabato (yaani jumamosi).
Biblia yasema kuwa jibu lako kwa swali hili litakuwa ndilo jaribio la mwisho nyakati za mwisho je, utamwabudu Mungu na kumtii kwa kuitunza sabato? ( ufunuo 13:15-17 na 14: 9 12).
Kila mtu atafanya uamuzi baada ya kufafanuliwa mambo haya. Kijitabu hiki chanuia kukusaidia kufanya uamuzi huu, lakini waweza kusoma zaidi kuhusu swala hili kwenye kitabu kiitwacho "Vita Kuu" au kikaratasi kiitwacho "Uhuru Hatarini." Hivyo basi sabato itakuwa ndilo jaribio kuu la uaminifu, kwani pambano lenyewe lahusu swala la ukweli na ibada. Watu wakishatiwa kwenye jaribio
hilo la mwisho. Msitari utachorwa kati ya wale wamchao Mungu na wale hapana. Kuisherehekea sabato bandia kulinganana sheria za nchi, lakini kinyume na amri ya nne litakuwa ni tangazo la utiifu kwa utawala unaopingana na Mungu ni tangazo la utiifu kwa muumbaji. Huku kundi moja likiikubali alama ya utiifu kwa tawala za dunia, kundi lingine huchagua alama ya utiifu kwa utawala wa Mungu, hivyo basi wataupokea "mhuri wa Mungu"
Mhuri Wa Mungu Kipajini Mwako
Ijapokuwa alama inayoonekana ya Mungu imo ndani ya ile amri yake inayohusu siku ya pumziko, japo Mungu asema kuwa sabato itakuwa ni ishara kati yake na watu wake (Ezekieli 20: 12, 20) twaelewa pia ya kwamba mhuri watakaoupokea watoto wa Mungu vipajini mwao muda tu kabla ya mwisho wa ule msukosuko wa dunia, utakuwa ni mhuri wa aina ya kipekee. Mhuri huu utatiwa juu ya waaminifu watakaonusurika na kuibuka washindi katika vita dhidi ya "alama ya mnyama."
"Mhuri wa Mungu" ni ishara ya kwamba Mungu hupendekezwa na watoto wake. Biblia yasema kuwa wale wanaotubu na kumwamini kristo wameahidiwa Roho mtakatifu kama mhuri. Mwamini anaye Roho mtakatifu kama mhuri maishani mwake bora tu awe anaishi karibu na kristo na kuyatenda mapenzi yake. (Waefeso 1: 13 na Matendo 5: 32 ).
Lakini sasa tutaangalia kule kutiwa mhuri kutakaofanywa na malaika wa Mungu muda kidogo kabla ya kurudi kwa Yesu. Biblia yasema kuwa malaika wa Mungu atautia "mhuri wa Mungu" vipajini mwa wale wanaolia na kuomboleza kwa ajili ya machukizo yanayopatikana na kutendwa miongoni mwa wale wanaojidai kuwa viongozi wa kiroho wa watu wa Mungu. "mhuri wa Mungu" ukiwepo kipajini ni ishara ambayo ni malaika pekee (wala si binadamu) wanaoweza kuiona (Ezekiel 9: 4) "mhuri wa Mungu "ukiweopo kipajini humaanisha ile hali ya kutosheka ndani ya ukweli, kimawazona pia kiroho hivi kwamba watoto wa Mungu hawawezi kutikisika (ufunuo 14: 1- 6 )
Wale ambao hawajitegemei, bali hujinyenyekeza mbele za Mungu, ambao kwa nguvu za Roho mtakatifu huishi kulingana na mapenzi ya Mungu, huwa wameshaipokea chapa ya mbinguni huku wakijiandaa kuupokea " mhuri wa Mungu " au chapa ya kukubaliki, watapewa wale tu walio na Roho wa Mungu, nao kwa jinsi hiiwatatiwa nguvu Rohoni hivi kwamba hawataweza kutikisika. Hakuna atakayewadhuru wakati wa yale mapigo, nao wameshajiandaa kuwa na kristo wakati ajapo kuwachukua wafuasi wake.
Kisha Biblia hutufunulia ya kwamba hiyo "alama ya mnyama" itaonekana kabla ya kumalizika kwa muda wa rehema, na pia kabla ya kurudi kwa Yesu (ufunuo 13:11-6) Twasoma kuhusu wale ambao
"Walimshinda yule mnyama na sanamu yake, na alama yake, na tarakimu ya jina lake. Hao walikuwa wamesimama kando ya hiyo bahari ya kioo, wakiwa na vinubi walivyopewa na Mungu" (ufunuo 15: 2)
Yohana pia aliweza kuwaona hao walioibuka washindi dhidi ya alama ya mnyama; huku wakiwa wamesimama mbele ya kiti cha enzi cha Yesu kilichoko mbinguni (ufunuo 4 :2 na 7: 9) WALIIBUKA WASHINDI hii yamaanisha kuwa hapo mbeleni walikuwa katika pambano fulani hivyo basi wateule watakaokuwa bado hai arudipo Yesu watakuwa wamesharipitia lile jaribio kuu linalohusu "alama ya mnyama".
"Mhuri wa Mungu" au "alama ya mnyama" hii ndilo litakalokuwa jaribio kuu litakaloamua mwisho wa kila mmoja wetu. Huu ndio mtihani ambao itawabidi masalio wa Mungu kuupita kabla yao kutiwa ule mhuri. Wote watakaodhihirisha utiifu wao kwa kuitunza sheria ya Mungu, na watakaokataa kuipokea ile sabato bandia (yaani jumapili watakuwa wamejitikia chini ya bendera ya Mungu, na wataipokea " mhuri wa Mungu aliye hai. "Wale watakaoionea haya ile kweli itakayo kwa Mungu, na watakao ikubali ile sabato ya Jumapili, wataipokea ishara ya mnyama
Sasa ndio wakati wa kujiandaa. " mhuri wa Mungu " kamwe hautatiwa kwenye kipaji cha mke au mume aliye mchafu kamwe hautatiwa kipajini mwa mume au mke aliye na tamaa, au aupendaye ulimwengu. Wala hautatiwa vipajini mwa waume au wake walio na ndimi za uongo au roho zenye hila. Wote watakaoupokea muhuri huo nisharti wawe bila kosa mbele za Mungu kama vile watu ambao wazo lao kuu ni mbingu.
Harakati Za Kuipendeza Jumpapili Zimeanza
Kunazo harakati za kuipendekeza jumapili zinazoendelea duniani kote. Papa Yohana Paulo wa pili atailazimisha jumapili kama siku ya kustarehe vikundi vikuu vya kidini, kama vile "The Christian Coalition," vyatuambia ya kwamba ni lazima tuzirudie zile amri kumi za Mungu. Katika muungano wa Uropa (EU), Waprotestanti na Wakatoliki wanajaribu kuyatafuta maswala ambayo wote wanaweza kukubaliana, moja wapo likiwa ni kuichukulia jumapili kama siku ya pumziko. Huko Uropa muungano wa madhehebu, yaani CEC, wananuia kuyaunganisha makanisa yote pamoja kulingana na mpangilio wa kikatoliki, na jumapili itatiliwa mkazo kama siku ya pumziko kwa watu wote, wakati Herald V alipowekwa taji kama mfalme wa Norway, alitaka sherehe ya kumbariki ifanyike mnamo siku ya jumapili ili siku hiyo ya jumapili itiliwe mkazo kama siku ya kupumzika. Makasisi na makuhani wanatamani sherehe za jmapili zifufuliwe. Wengine wanataka harakati zinazohusu watu wote wa kuitetea siku hii iwe ya pumziko, huku wengine wakipendekeza adhabu kali kwa wale watakao haribu amani ya siku hiyo takatifu.
Twaona pia jinsi makasisi na wachungaji wanavyojiunga vya wafanya kazi, mashirika
yakulinda mazingira, hali kadhalika matawa mbalimbali ya biashara na viwanda, ili waweze kuilinda jumapili
na kuifanya kuwa siku tofauti na zinginezo katika juma. Nia zao huenda ni nzuri, kwani ni jambo
la busara kutoka kuifanya siku ya pumziko kuwa ni ya kuridhisha. Kwa kweli yafaa tustarehe,
tupumzike na tuweze kuburudika kiroho na pia kimwili. Lakini kama ingelihitajika wakristo kuipendekeza
siku ya pumziko, yafaa iwe ni ile siku ambayo muumbaji ameitakasa na kuibariki, yaani sabato, siku
ya saba ya jumaa kulingana na Biblia. Isitoshe haifai mtu yeyote alazimishwe kuitunza siku ya
pumziko ambayo serikali imeamua. Kuitakaza siku ya pumziko ni kwa hiari, wala si lazima. Lakini
Biblia yasema kuwa uhuru wa kuabudu utadharauliwa katika swala hili. Hata sasa tayari twayaona
matayarisho ya vikwazo kama hivyo vya kidini.
Alama Ya Mnyama Itafika Hivi Karibuni
Jaribio kuhusu " alama ya mnyama " litafika pale jumapili itakapo simamishwa kimabavu, na kwa amri, kama siku ya kupumzika, jambo ambalo laweza kufanyika hivi karibuni.
Hata hivyo, kwa vile sasa twajua kuhusu undanganyifu uliofanywa dhidi ya siku ya pumziko, yatupasa pia tufanye uamuzi leo (Yakobo 4 : 17 ). Ni jambo la muhimu kwetu sisi leo kujitia kabisa kwenye upande wa Yesu kuhusu swala hili, ili Roho mtakatifu awe mwenye kuutia nguvu tunapokabiliana na majaribu yaliyo mbele yetu ambayo yahitaji uamuzi.
Masalio Watavumilia Watazitunza Amri Za Mungu Na Mafundisho Ya Yesu
Biblia yawaelezea wale ambao hawataikubali sabato bandia ya kibinadamu jinsi hii;
"Hapa ndipo penye subira ya watakatifu, wale wazishikao amri za Mungu, na imani ya Yesu" (Ufunuo 14 : 12)
Kwa hivyo, hebu na tuzijue amri za Mungu pamoja na yale yote aliyoyaamini Yesu.
Biblia yadhihirisha wazi kuwa litakuwepo pambano kali la kiroho mnamo siku za mwisho kabla ya kurudi kwa Yesu wale ambao hawataikubali alama ya mnyama watafinyiliwa toka pande zote. Yasemekana ya kwamba hawataweza kununua wala kuuza, na kuwa amri itatolewa ili wauawe (Ufunuo
13: 15 16). Dunia yote itaustaajabia upapa ( yaani mnyama ) na hata kumfuata, lakini masalio wa Mungu walio waaminifu hawatawezwa na mvuto huo, Biblia yasema kuwa hawa hawakujinajisi na wanawake (yaani makanisa, 2 Wakoritho 11:2), kwani wao ni kama bikira. Kwa kifupi, hawaupokei " mvinyo wa Babuloni unaolevya," lakini hutangaza, kwa sauti safi, ule "ujumbe wa malaika watatu," na pia huionyesha tabia ya Mungu maishani mwao. Hawauachilii ubinafsi wao uongoze, bali huifuata njia ya Mungu huku wakiongozwa na Roho mtakatifu, kuhusu hawa yasemekana..
"Hawa ndio wamfuatao mwana kondoo (Yesu) popote aendapo " "Na katika vinywa vyao hapakupatikana hila; kwani wao husimama mbele ya kiti cha enzi cha Mungu bila kosa lolote." (Ufunuo 14: 1 5)
Hao wameyatakasa maisha yao kwa ajili ya kristo, na wameshampokea Roho mtakatifu ili awe chanzo cha nguvu zinazohitajika maishani mwao, ili waweze kuishi kwa njia ya haki mbele ya Mungu na binadamu.
Yasema kuwa hawa hawana kosa lolote. Vivyo hivyo ilisemekana kuwahusu wana kondoo katika enzi za angano la kale. Hawa walikuwa wamlenga kristo ambaye pia alikuwa hana kosa. Ikiwa Roho mtakatifu yu ndani yetu, sisi pia twaweza kuidhihirisha tabia ya kristo maishani mwetu, wala hatutatenda dhambi kamwe. Hebu tuelewane hapa. Twaweza kuyatenda haya si kwa nguvu zetu wenyewe, bali ni kupitia kwa nguvu za Mungu ambaye hufanya kazi ndani yetu huku akitusaidia kuishi kulingana na mapenzi ya Mungu (1 Petero 1: 14 16 na Wafilipi 2:123). Hivyo basi Biblia yakuletea changamoto hii! Ikiwa wajihisi kuwa hufai mbele za Mungu, au iwe waogopa mambo yajayo, yakupasa uelewe ya kuwa Roho mtakatifu yuakuita uje kwa Yesu pamoja na huo mzigo wako wa dhambi, sasa! zitie dhambi zako miguuni pake Yesu katika maombi, ili kufanyie upatanishe na wale watu uliowaumisa, au waliokuumiza, kisha haki yake itakuwa ni yako. Hali kadhalika, yatupasa kuomba tupewe nguvu za Roho mtakatifu ili atuwezeshe kuendelea njiani pamoja na kristo, ili tuishi katika haki kwa mambo yote. Kwa neema ya Mungu, tutakuwa tayari wakati akija karibuni kuwachukua watu wake.
Sanamu Ya Mnyama
Kwa vile Upapa unaingiana na zile alama za kumtambulisha " mnyama " kulingana na Biblia, basi " sanamu ya mnyama " sharti iwe ni nakala ya mfumo huu.
Maana yake " sanamu ya mnyama " ni Uprotestanti ulioasi ambao hutokea wakati makanisa ya Kiprotestanti yanapoanza juhudi za kuishawishi serikali kuwalazimisha watu waufuate mtindo wao wa ibanda.
Huko Uropa, nchi nyingi zinalo kanisa fulani linalopendekezwa na serikali. Serikali na kanisa hufanya kazi pamoja. Kanisa hupata msaada kutoka kwa serikari ili kute keleze majukumu yake. Huu ni sawa na mfumo wa kikatoliki. Katika Enzi za katikati za Giza, tulikuwa mfano halisi jinsi kanisa katoliki lilivyotumia nguvu zake na kuwatesa watu wa imani zingine. Biblia yasema kuwa ukatili kama huo utarudishwa mnamo siku za mwisho. (Ufunuo 13: 11 18). Kwa vile katiba ya Marekani haina nafasi ya kanisa la kiserikali, ni vigumu kudhania ya kuwa hapo ndipo mfano wa ile serikali ya upapa itakaposimamishwa, lakini Biblia yadhihirisha kuwa hivi ndivyo mambo yatakavyotendeka. Wataitumia serikali ili kujisukumia sheria zao za kidini, hasa sheria zinazohusu utakasaji wa jumapili.
Lakini huenda utasema kuwa Marekani ni nchi ya uhuru wa kuabudu. Kweli, Biblia huielezea pia kama mwana kondoo aliye na pembe mbili lakini anenaye kama joka. Mwanzoni mwa historia yake, Marekani ilionekana kuwa nchi inayoutetea uhuru wa dini. Pembe za mwana kondoo husimamia ujana, bila hatia na upole ambazo zilikuwa ni sifa za Marekani wakati ambapo nchi hiyo ilianza kukua mnamo karne ya 18. Uprotestanti na Ujamhuri zilikuwa ndizo sera zilizokuwa msingi wa serikali. Uhuru wa dini ulidumishwa, hivi kwamba kila mmoja alikuwa huru kumwabudu Mungu kulingana na dhamira zake hata hivyo Biblia yaonyesha kuwa mtindo huu utabadilika katika nchi hiyo hadi mwishowe, itanena kama joka. Kwa kawaida, taifa hunena kupitia kwa bunge lake.
Wengi sasa wametambua kuwa bunge la Congress limeshaanza kupitisha sheria za kidini, kama vile HR 2431, sheria hii huipatia afisi mpya iliyoteuliwa mamlaka ya kuvichunguza vikundi vya kidini duniani kote. Wale ambao wanayatekeleza mateso ya kidini wataadhibiwa. Afisi hii itaamua maana ya mateso ya kidini. Kwa mfano je, kijitabu chaweza kusemekana kuwa kinawatesa wakatoliki.
Katiba ya marekani yasema kuwa kamwe hatutapitishwa sheria zinazohusu dini. Yasema hivi, "Bunge kamwe halitatengeneza sheria kuhusu utanguluzi wa dini, wala kuuzuia uhuru wa kuyatekeleza majukumu ya kidini." Ni kwa kulidharau hakikisho hili la uhuru ambapo utawala wa serikali utawasukumia watu sheria hizo za kidini. Utaratibu huu tayari umeanza, na mengine mengi yaja. Ndiyo, kwani Biblia yasema kuwa nguvu zote za upapa (mnyama wa kwanza) zitatumiwa na Marekani (mnyama wa pili) kwa niaba ya upapa. Wataitanguliza ile "sanamu ya mnyama." Hata sasa wameshaanza kufanya hivyo.
Marekani Itaongoza Katika Kulazimisha Utunzaji Wa Jumapili
Wengi watastaajabu watakapoiona Marekani ikiongoza katika kuitanguliza "alama ya mnyama" (shurutisho la kutunza jumapili) na kiisha baadaye nchi zinginezo zitafuata. Wale watakao wapinga mazimwi hawa (yaani Uprotestanti ulioasi na ukatoliki) na kukataa kuipokea ile "alama ya mnyama" watatiwa alama kama waasi ambao wanahatia ya kuleta misiba na majanga na pia kama wanaoivuruga amani duniani. Biblia yasema kuwa mnamo siku za mwisho amri zitatolewa ili watu hawa wauawe (ufunuo 13 : 11 16). Ni wakati huo ambapo Yesu kristo, aliye mwokozi wa dunia, atakaporudi kuwapa uhuru watu wake. (soma zaidi kuhusu "mnyama mfano wa mwana kondoo" katika kitabu cha Great Controversy kurasa 439 445)
Adhabu Kali
Biblia yadhihirisha wazi kuwa wale watakaoipokea " alama ya mnyama " watapata adhabu ya kuogofya. Biblia hutwambia wazi kuwa wale wanaoipokea hiyo " alama ya mnyama " watakuwa wa kwanza kupitia kwenye maumivu makali wakati wa yale "mapigo 7 " yatakayokuja baada ya muda wa rehema kuisha (ufunuo 15: 5 - 8) Biblia yasema hivi:
"Kisha nikasikia sauti kubwa kutoka hekaruni ikiwaambia wale malaika saba, "nendeni mkamwage mabakuli hayo saba ya ghadhabu ya Mungu duniani." Basi malaika wa kwanza akenda akamwaga bakuli yake juu ya nchi. Mara madoda mabaya na ya kuumiza sana yakawapata wote waliokuwa na alama ya yule mnyama na wale walioiabudu sanamu yake." (Ufunuo 16: 1-2)
Mapigo sita yanayofuata toka kwenye mabakuli ya hasira za Mungu yatawajia wale walioipokea " alama ya mnyama" huku watoto wa Mungu wakitembea huru (Ufunuo16: 1- 2) Leo hii, kila mtu hukabiliana na nguvu za shetani za uharibifu. Lakini watoto wa mungu, wanaotambuliwa na mungu, yaani "Mhuri wa mungu",hawatadhuriwa na yale "mapigo saba"ya mwisho, kama vile Waisraeli hawakudhuriwa na yale mapigo saba kabla yao kuondoka kwenye nchi ya Misri (kutoka 8:22).
Adhabu ya mwisho,tena baya sana kuwahi kuwajia wale walioipokea "alama ya mnyama'',ni pale ambapo shetani, pamoja na wote waliojitia kwenye upande wake ,watakapo tekelezwa kwa moto na madini ya kiberiti,Biblia yaelezea hivi:
"Lakini watu waoga, wasioamini, wapotevu, wauaji, wazinzi wachawi, waabudu sanamu na waongo wote, mahali, pao patakuwa ndani ya lileziwa liwakalo moto na madini ya kiberiti, hicho ndicho kifo cha pili" (Ufunuo21:8).
Wale wote waliompinga mungu watahukumiwa kulingana na matendo yao wakati huo, na watateketea kama vile nyasi wataharibiwa (Ufunuo20:11-15 na Malaki 4:1). Huu ndio uharibifu wa mwisho dhidi
ya maovu na wale wote waliokwenye upande wa uovu. Hatimaye mungu ataumba mbingu mpya ambapo haki tu itakayotawala, Nao mviringo huo waishia hapo. Binadamu ataishi peponi aliyoipoteza-yaani Edeni-pasipo dhambi tena,na ambapo binandamu aweza kunena na mungu uso kwa uso tena, kwani wakati huo atakuwa ameshaupokea mwili wa utakatifu (1wakorintho 15:50-54).
Hili ni jambo la kutazamia, nazo shida za hapa duniani hazitakuwa na umuhimu wowote zikilinganishwa na ule utukufu utakaowajia wateule. Hebu tuombe tupewe Roho Mtakatifu atusaidie kufika pale. Ishara za nyakati zaonysha kuwa saa hii haimo mbali.
Wateule Wataenda Mbinguni Kwanza
Yesu arudipo, wateule watainuliwa hewani na kupelekwa mbinguni. Haya yaelezwa hivi katika Biblia:
"Hili tunalo waambieni ni fundisho la bwana. Sisi tulio hai,ambao tutakuwa tumabaki wakati bwana atakapokuja, hakika hatutawatangulia wale waliokwisha fariki dunia, maana patatolewa amri, sauti ya malaika mkuu, sauti ya tarubeta ya mungu, naye bwana mwenyewe atashuka kutoka binguni. Ndipo wale waliokufa wakiwa wanamwamini kristo watafufuriwa kwanza. Kisha sisi tulio hai wakati huo tutakusanywa pamoja nao katika mawingu kumlaki Bwana hewani. Na hivyo tutakuwa daima pamoja na bwana." (soma 1 wathesalonika 4:15-17, wafilipi 3:20-21 na Yohana 4:1-3).
Wateule watanyakuliwa hewani pamoja ili wamlaki bwana.
Yesu hataikanyanga dunia wakati huo, lakini wateule watachukuliwa juu angani. Wataelekea Mbinguni (Ufunuo 12)
Biblia yasema kuwa wateule wataishi mbinguni kwa miaka 1000 (Ufunuo 20:4). Hiki kitakuwa ni kipindi cha raha takatifu, tukiwa pamoja na mwokozi wetu yesu, na pia wateule. Lakini pia utakuwa ni muda wa uzito. Biblia yafunua kuwa wateule watahukumu, watahakikisha kuwa wale wasiookolewa wapata hukumu ya haki, na kuwa Mungu ni wa haki.
Baanda ya miaka 1000, wale wasiookolewa watainuka toka makaburini yao na kuipokea hukumu yao ya mwisho. Watatupwa kwenye ziwa la moto lililoelezewa hapo awali.
Kumbuka usome kwa makini mchoro ulio hapo juu!
Mungu Ameshika Usukani
Japokuwa leo yaonekana kana kwamba watawala wa dunia wameiteka dunia, Mungu angali ameshika usukani. Katika wakati umfaao, ataingilia kati na kuwa weka huru watu wake, hata awafikishe pahali alipo yaani mbinguni (Yohana 14:1-3). Ndiposa Biblia huyaelezea matokeo ya pambano hili hivi:
"Kisha nikaona kitu kama bahari ya kioo, imechanganywa na moto. nikawaona pia wale watu waliomshinda yule mnyama na sanamu yake, na alama yake na tarakimu ya jina lake, wakawa wamesimama kando ya hiyo bahari ya kioo, wakiwa na vinubi walivyopewa na Mungu. Walikuwa wakiimba wimbo wa Musa, mtumishi wa Mungu na wa Mwanakondoo: "Bwana Mungu mwenye Nguvu, matendo yako ni makuu na ya ajabu mno! Ewe Mfalme wa watakatifu, njia zako ni za haki na za kweli!" (Ufunuo 15:2-3)
Ufunuo 17: 14 pia hutwambia kuhusu wale watakaoshinda: awe ni "mnyama" (yaani upapa) na washirika wake, au ni Mwanakondoo" (Yesu) na wale walio katika upande wake. Humalizia kwa kueleza namna hii:
"Hawa watapigana na mwana kondoo, lakini Mwanakondoo pamoja na wale aliowaita na kuwachagua ambao ni waaminifu, atawashida kwa sababu yeye ni Bwana wa mabwana na Mfalme." (Ufunuo 17:14).
Yesu pamoja na wale wanaosimama upande wake ndiye atakayeibuka mshindi katika pambano lililo mbele yetu. Wale waaminifu watakuwa na imani ya yesu. Kutokana na upendo wao kwa Mungu, na huku wakiwezeshwa na Roho Mtakatifu, watazitii amri zake, sio kwa kulazimishwa, bali ni kwa furaha. Biblia husema:
"Hivi ndivyo tunavyojua kwamba tunawapenda watoto wa mungu: Kwa kupenda Mungu na kuzitii amri zake. Na amri zake si ngumu. "(Yohana 5:2-3)
Nani Atakaye Kujiunga?
Wale malaika watatu wanaoutangaza ule "ujumbe wa malaika watatu" husimamia binadamu waliojitowa maisha yao kwa kristo. Watautangaza ujumbe huu na inayoeleweka, maana Roho Mtakatifu anashiriki. Je, si wewe pia ungependa kijiunga nasi katika kuutangaza "ujumbe wa malaika watatu?" Sasa wakati umewadia wa kufanya uamuzi huu.
Iwapo utajihisi kuwa umefungwa na minyororo ya shetani na pia watawala, mwombe Mungu aliye mbinguni akuweke huru. Biblia hutuhimiza:
"La! Mfungo ninaotaka mimi ni huu: kuwafungulia waliofungwa bila haki, kuziondoa kamba za utumwa, kuwaachilia huru wanaokandamizwa na kuuvunjilia mbali udhalimu wowote!" (Isaia 58:6)
Yatupasa wewe na mimi tuombe ili tupewe nguvu za kuivua mizigo yote ambayo dunia imetubebesha mabegani, iliyo pia kinyume na neno la Mungu, hali kadhalika sera zinazoambatana na neno hilo. Hujaribu kutufunga na kamba za maelfu ya amri za kibinandamu, hata kutuzuia tusiwe huru katika Bwana. Lakini uhuru wa kweli hupatikana pale tunapoanza kushirikiana na utawala wa mbingu ili tuuondoe mzigo wa dhambi. Twakumbushwa pia kuhusu maneno haya ya kutia nguvu kutoka kwa Biblia:
"Mwana akiwapeni uhuru, mtakuwa huru kweli." (Yohana 8:36). na "pale alipo roho wa Bwana kunao Uhuru" (2 Wakorintho 3:17)
Kwa vile twaishi nyakati za mwisho na muda wa rehemu u karibu kuisha, yatarajiwa kuwa watu wa Mungu watajitahidi kuwaokoa watu toka kwenye mitego aliyoitega shetani na kuwafungua macho ili wautambue ujumbe wa wokovu. Lakini Biblia hukiita kikundi cha waumini wa nyakati za mwisho "Laodikia" (Ufunuo 3:14-22) Laodikia sifa zake ni uzembe na uvuguvugu. Wengi wa wale ambao hujidai kuamini ujumbe wa malaika watatu ni waumini walio uvuguvugu, wasioonyesha hamu yoyote ya kuwaletea wengine ujumbe huu. Wao si moto au baridi. Hukaa katikati, huku wakijigamba kuwa hawahitaji chochote. Hawataki kuachana na ubinafsi wao. Hujihisi kuwa ni matajiri, wasiokosa chochote cha kiroho, lakini wao ni maskini, vipofu na uchi. Hawawezi kijitambua jinsi walivyo hasa. Je yawezekana kuwa wewe nami tu katika hali sawa na hiyo ya uvuguvugu?
Lakini hebu na tumshukuru Mungu! Yeye hutuonyesha njia ya kutoka kwenye hali hii isiyo na tumaini Hatujui kwa upendo wa moyoni na kutuhimiza tubadilike, tuipokee dawa ya macho anayotukabidhi (Ufunuo 3:18). Dawa hii ni Neno la Mungu likiongelesha dhamiri zetu kupitia kwa Roho Mtakatifu. Tukijipaka dawa hiyo, tutapokea nguvu za kiroho za kufanya uamuzi utakaotuwezesha kuyastamili mashambulio ya shetani yaliojaa ujanja, pia kuitambua dhambi na kujihisi kuwa kinyume nazo - kuuona ukweli na kuutii. Mabadiliko haya yakishatendeka, Mungu tatutumia tena, na tutakuwa na nguvu za kumshuhudia Mungu katika kazi hii ya mwisho.
Twatumai kuwa utayaweka wakfu maisha yako ili umtumikie Mungu, na ujiunge nasi katika kuutangaza "ujumbe wa malaika watatu" ndani ya maisha yako na katika mafundisho yako. Hili ndilo onyo la mwisho, hali kadhalika ujumbe wa neema kwa ulimwengu ulioanguka, nalo nijukumu la dhati na lenye uzito mwingi lililoezekwa mabegani mwetu. Yatupasa tuelewe ya kuwa twakaribia mwisho wa historia ya dunia hii. Muda wa rehema ukishapita na Yesu kurudi, hapana nafasi nyingine itakayopeanwa. Sasa ndio wakati ambao yatulazimu kuujibu inavyofaa ule mwito wa Roho Mtakatifu wa kumkabidhi mioyo na mawazo yetu.
Ni ombi letu kuwa watu wengi iwezekanavyo, wanaoyasoma maneno haya, watajihisi kuwa wameitwa washiriki katika kuueneza ujumbe huu wa malaika, huku wakijihesabu wemebahatika. Mavuno yako tayari, lakini wafanyi kazi ni wachache, naye Mungu atawatumia wale watakao kuyaweka maisha yao wakfu kwa ajili Yake.
Naomba wewe nami tuwe miongoni mwao!
Salamu za upendo toka kwa
Bente na Abel Struksnes