[Back to the Main Page!]

Sisi tuko vitani!

Sasa je! Tutashindaje na hatufai ushindi!

Je, wewe wajihizi kuwa hufai, mwenye hofu, bila nguvu na mpotevu! Na kama wajihizi hivyo tungependa kukupa wewe faraja na matumaini! Maneno yake Yesu yanakuelekea wewe; "Njoni kwangu ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha." Mathayo 11:28.

UPENDO UNAODHIHIRIKA!

Je,umewahi kufikiri kuhusu upendo wa ajabu ambao Yesu ametudhihilishia sisi?- kukuokoa wewe na sisi? "kitabu kidogo tu cha Bibilia "Kinasema hivi "kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa mwanawe pekee ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele." Johana 3:16.Mmoja wapo wa wanafunzi wa wa Yesu ambaye ni Yohana alipata kuelewa juu ya huo upendo wa Yesu na kwa hivyo akaandika hivi : " Hili ndilo pendo si kwamba sisi tuliyempenda Mungu, mbali kwamba yeye alitupenda sisi akamtuma Mwanawe kuwa kipatanisho kwa dhambi kwetu"1 Yohana 4: 10

JE! YESU AWEZAJE KUTUOKOA SISI?

Lakini, ni vipi Yesu anaweza kutuokoa? Yeye alikuja ili aendeleze penye Adamu alishindwa.

Yesu aliwezaje kufanya haya, ili hali yeye akiwa ni Mungu? Paulo anasema hivi, "iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu" ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho; bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu, tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba. Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia jina lile lipitalo kila jina ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya Nchi, na kila ulimi ukiri ya kuwa Yesu Kristo ni Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba Mungu ." (wafilipi 2: 5-11)

Naye Yohana anatuambia kwa njia hii: "Hapo mwanzo kulikuwako neno, naye neno alikuwako kwa Mungu, naye neno alikuwa Mungu. Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu. Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika ——— Naye neno alifanyika mwili, akakaa kwetu nasi tukauona utukufu wake utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba, amejaa neema na kweli.: Johana 1:1-3, 14.

Haya ni mambo magumu kuelewa; maandiko yanaelezea yesu kama "Neno". Ni Yesu aliyekuja na mwili kama binadamu. Naye Paulo ana dhibitisha kwa maneno haya "Basi, kwa kuwa watoto wameshiriki damu na mwili, yeye naye vivyo hivyo alishiriki hayo ili kwa njia ya mauti, yaani, ibilisi," (Waebrania 2:14). Penginepo Paulo anaandika na kusema, "Mungu alimtuma mwanawe katika mfano wa mwili ulio wa dhambi," Warumi 8:3. ili atuokoe sisi, Yesu Kristo ilimpasa kushinda penye Adamu alipata kushindwa Adamu (Mwanadamu) kwa kutenda dhambi. Yesu alijifaa utu wetu akawa kama sisi, Ila hali akiwa ni Mungu, alionekana kuwa mwanadamu. Mtu mdhaifu.

Ni kwa njia hii pekee aliweza kutuokoa sisi. Paulo anaelezea kazi na pabambano lake Kristo kwa maneno haya: "Hivyo ilimpasa kufananishwa na ndugu zake katika mambo yote, apate kuwa kuhani mkuu mwenye rehema, mwaminifu katika mambo ya Mungu, ili afanye suluhu kwa dhambi za watu wake. Na kwa kuwa mwenyewe aliteswa alipojaribiwa, aweza kuwasaidia wao wanaojaribiwa. "Waebrania 2:17,18 "kwa kuwa hamna kuhani mkuu asiyeweza kuchukuana nasi katika mambo yote ya udhaifu; bali yeye alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote, bila kufanya dhambi. Basi na mkikaribia kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji."Waebrania 4:15-16.

Yesu aliishi maisha yasiyo na dhambi. Baada ya kuzaliwa ndani ya holi ya ng'ombe mjini Bethlehemu, naye shetani kupitia Herode, akajaribu kumuua. (Mathayo 2:7-23). Alijaribiwa na shetani(Ibilisi) atende dhambi (Mathayo 4:1-11) mafarisanyo na waandishi walimjaribu, na wakajaribu kumzingizia mambo ya uongo. Alijaribiwa sana kwa njia zote. Alitandikwa kwa mijerendi, kutusiwa, kupigwa na kutemewa mate.Wakavika taji la miiba kichwani, na mwishowe wakamsulubisha msalabani kama mvunja sheria, ingawaje hakukosa kwa jambo lolote. Hapo msalabani Kalwali, alitoa uhai wake kwa ajiri yangu na wewe au sisi. Kitambo kidogo alitoa sauti ya kilio akisema "yote yameisha," na akakata roho. Ushindi ukapatikana. Baadaye kidogo, wakamchoma ubavuni kwa mkuki, na damu ikatoka na maji, dhihirisho kwamba alikuwa amekufa. Alimwaga damu yake kwa ajili yetu . Alikufa kwa ajili yetu, na ndipo sisi tuishi milele.

Hebu fikiria kujitolea kwake kwa njia ya upendo! Alionyesha alitujali sisi. Si Yatulazimu na basi sisi tudhihirishe shukrani zetu kwake, kwa kupokea kipawa cha wokovu?

KUPITIA KWA MIJEREDI YAKE SISI TUMEPONA

Yesu alikuwa na marafiki wengi, lakini na maadui wengi pia. "Alidharauliwa na kukataliwa na watu, mtu wa huzuni nyingi, ajuaye sikitiko; na kama mtu ambaye watu humficha nyuso zao. Alidharauliwa na kukataliwa na watu, mtu wa huzuni nyingi, ajuaye sikitiko na kama mtu ambaye watu humficha nyuso zao, alidharauliwa wala hatukumhesabu kuwa kitu. Hakika ameyachukuwa masikitiko yetu , amejitwika huzuni zetu, lakini tulimdhania yakuwa amepigwa , amepigwa na Mungu na kutezwa.Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu alichumbuliwa kwa maovu yetu.Adhbu ya amani yetu ilikuwa juu yake na kwa kupigwa kwake sisi tumepona. Isaya 53:3-5

Ni kwa nini Yesu aliyapitia haya yote? Unaweza kujiuliza, Kwa kweli Bibilia inasema hivi "dhambi ni uasi", na pia "mshahara wa dhambi ni mauti" (1 Yohana 3:4, Warumi 6:23). Zaidi ya hayo Bibilia inasema "wote wamefanya dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu" (Warumi 3:23). Hapa tuko ndani ya meli moja. Kwa nje, sisi tumehukumiwa kifo, kwa sababu zote tumekosa . Ni kwa sababu tumekosa, Yesu alikuja kutuokoa ili tusipotee milele.

DHAMIRI ZETU NA MVUTANO KATI YA MWILI NA ROHO

Hata Ingawa mengi yameharibika katika sayari ya dunia, bado twaweza kuyaona mengi ya maumbile ya Mungu. Maua mengi mazuri, miti, ndege wa angani, wanyama na pia binadamu. Binadamu pamoja na wanyama wamevikwa urembo, hekima, macho, masikio, mapua, midomo na hisia. Kupitia kwa haya, tunaweza kufurahia utukufu wa uumbaji. Ni lazima tufudishe mawazo kutambua uzuri wa uumbaji. Hili laweza kuinua maisha. Tambua ya kwamba tuna adui, anayeitwa shetani na ibilisi - yeye ndiye hutujaribu tuyatende mambo yale mabaya. Yeye hutujaribu kupitia kwa mawazo yetu. Anajua kuwa sisi hupenda kutawaliwa na tamaa za mwili, na kutenda dhambi. Na ndipo yeye hutaka sisi tuone, tusiokie, tuonje kuwa na hisia zinazotuongoza kwa dhambi. Hutudanganya kupitia hisia zetu ili kutenda dhambi. Hutushikilia mkno ili tutende kinyume na uumbaji na hata Amri za Mungu.

Tangu muumba kuanzisha Amri kumi, (Kutoka 20:3-17) kama mwongozo kwa binadamu, shetani, ambaye hupigana na Mungu, hutumia mbinu zote kutuletea mvuto ili tuvunje Amri za Mungu. Mungu anataka tuzishike amri zake naye shetani huwa kinyume cha Mungu. Mvutano kati ya mwili wetu na roho unaendelea kila siku, kila dakika, kwa hakika kila seconde. Na hivi ndivyo Paulo anaelezea.

"Basi nasema, enendeni kwa roho wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili kwa sababu mwili hutamani ukishindana na roho, na roho kushindana na mwili kwa maana hizizi zimepingana hata hamwezi kufanya mnayotaka. Lakini mkiongozwa na roho, hampo chini ya sheria".

MWILI NA ROHO-NI NGUVU MBILI ZINAZOPIGANA

"Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayo fanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyo kwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo, hawatauridhi ufalme wa Mungu.

Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi, juu ya mambo kama hayo hakuna sheria. Na hao walio wa Kristo Yesu wameusulibisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake. Tukiishi kwa Roho, na tuenende kwa Roho tusijisifu bure tukichokozana na kuhusudiana." Wagalatia 5: 16-25.

Uwezo tunaohitaji sisi wote

Sisi zote tumeumbwa tukiwa na uwezo wa mawazo ya kukata kauli zetu katika uamuzi wa maisha. Katika ndani ya akili zetu mnao uwezo wa kuchagua, kuwaza na kulinganisha, na kuwa na maono mazuri katika mawazo yetu. Tukiwa tunaelewa hayo, na kwa hakika tukatumia nia zetu wenyewe twaweza kufanya maamuzi yetu, bila kuongozwa na dhamiri zetu, ama watu wengine au hali. Mungu alituumba hivyo. lakini anataka tushirikiane pamoja naye. Ni wakati tunapoelewa mapenzi ya Mungu, ndiposa tutafanya uamuzi ulio wa busara sana katika maisha. Tuweza kumuomba Mungu atusaidie sisi kuchangua yote yanayolingana na mapenzi yake. Hayo yatatusaidia kusimama wima na kushinda majaribu ya shetani. Sisi tukifanya maamuzi yetu ya kibinafsi bila ya kupata ushauri kutoka kwa Mungu, kwa mara

nyingi tutafanya maamuzi ambayo yatatupotosha baadaye. Kwa hivyo,kazi yetu, ni kuambatanisha nia zetu kwa upande wa Yesu Kristo.kuzamisha nia zetu na zile za Mungu,tunaposhusha nia zetu katika nia yake, njia zake tu , zikiwa ndizo zafaa,Roho mtakatifu ataingia ndani ya maisha na kufanya ndani yetu "kunia na kutenda yalio mapenzi ya Mungu"Wafilipi 2: 13.

Wakati wowote sisi tunapokataa kutojitii, na kuamua kuambatana na mapenzi ya Mungu, sisi tumeshikanishwa na nguvu ambazo zimepita nguvu zote. Tunapokea uwezo kutoka kwa Mungu ambao unatushikanisha na nguvu zake, ambayo kwa hayo tutaishi maisha mapya _ maisha ya imani.

Ni msaada gani utakuwa wetu katika pambano dhidi yetu na shetani? Tayari hapo numa tumekwisha ongelea kidogo tu juu yake; lakini tutayaangalia kwa kindani zaidi. Wakati Yesu alipo paa akaenda mbinguni, alisema "lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajia juu yenu Roho mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu". Penginepo Yesu alisema "lakini huyo msaidizi, huyo Roho mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia.". La mwisho Yesu aliwaahidi yafuatayo "lakini yeye atakapokuja, huyo roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena na mambo yajayo atawapasha habari yake". Matendo1:8, Yohana 14:26 Yohana 16:13 . Roho mtakatifu, mmoja kati ya Uungu utatu, atatupa nguvu kuwa mashahidi wa Yesu. Atatusaidia kuelewa ukweli wa neno lake Mungu, na kuishi kulingana na mapenzi ya Mungu. Kwa njia hii tutapata nguvu za kushinda majaribu ya shetani, ambaye hatuyawezi kushinda kwa uwezo wetu.

Je, Kila mmoja aweza kufurahia kwa njia zake mwenyewe?

Wengine hufikiri eti imani yetu ina msingi wa hisia" wengine husema, "kila mtu anafurahishwa na mwelekeo wake mwenyewe. Ingawaje Bibilia inasema, "kuna Bwana mmoja, imani moja na ubatizo mmoja", (Waefeso 4:5) Yesu aliye muumbaji, anasema "mimi ndimi njia, na kweli, na uzima: hakuna awezaye kuja kwa Baba bila mimi" (Yohana 14:16)

Hivyo basi, sisi hatufurahishwi na njia zetu. Basi itatulazimu kufuata nyayo zake Yesu, ambaye ndiye njia. Sisi hatutaendeshwa na hisia zetu, "lakini tufuate njia aliyo tuwekea, ambayo tunaipata kwa kusoma neno la Mungu. Mafundisho mengi na makanisa ya dini zimejengwa chini ya mafundisho fulani au mistari kadhaa katika Bibilia. (Wakolosai 1:17). Hakuna mwingine anayeweza kutupa maisha ya baadaye na matumaini, ambayo yatatupatia uzima wa milele. Ni kwa njia pekee ya kumpokea Kristo kwa imani nakusema "ndio kwa neema yake ya wokovu tunaweza kupokea wokovu". Lazima ukate kauli hii sasa! Uchague uzima au mauti. Bibilia inasema: "mshahara wa dhambi ni mauti, bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu." (Warumi 6:23)

Muda mfupi tu kabla ya kufa kwa Yoshua kiongozi wa Israeli, aliwaambia watu hivi, lazima wachague Ni nani watakaye mtumikia kama miungu ya misri na ya waamareki au Bwana. Na akatoa ushuhuda huu; "mimi na nyumba yangu tutamtumikia Bwana" (Joshua 24:15) Hebu na kila mmoja wetu afanye uamuzi kumfuata Yesu Kristo sasa! Na tutapita kutoka mauti hadi uzimani, ndiposa tutakuwa na lengo la kweli la maisha yenye matumaini ya baadaye.

Jinsi ya kutupilia mbali huu mzigo mkubwa

Kwa kusema tu Ndiyo kwa Yesu, ina maana kwamba atatusaidia kushinda uzito wote wa dhambi katika maisha yetu. Yesu alikuja kutuokoa kutoka kwa dhambi (Mathayo 1:21). Waona wakati wowote tunapokuwa na dhambi ambayo haijatubiwa katika maisha yetu, sisi tu bado ni watumwa wa dhambi. Bibilia inasema, "yeye atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi" (Yohana 8:34)

Sisi huwa kama tumeshikwa na kamba. Shetani anatutawala na hatuwezi kuokolewa tukiwa katika hali hii, kwa sababu hakuna chochote kichafu kitaingia ufalme wa Mungu (Ufunuo 21:27). Katika njia hii ya upotovu, ni lazima tumuombe Mungu ili atukomboe. Ni Yesu pekee awazaye kutukomboa. Anaweza kuikata minyororo ya dhambi na ni wakati tunapoanza kukata minyororo ya dhambi ili tuwekwe huru ndipo pambano kamili linaanza. Roho mtakatifu anapoamsha dhamiri ya mtu, kwa njia mmoja au nyingine binadamu hutambua dhambi zake, nguvu zake, uovu wake, uchungu unaosababishwa na dhambi na hapo sasa huansa kuiona dhambi kwa mach mengine ya kuichukia. Hapo tutaelewa ya kwamba dhambi ilitutenganisha na Mungu na sisi ni watumwa wa dhambi; kwa jinsi hiyo tunapoendelea kuelewa vile hatuna nguvu na ya kuwa mwelekeo wetu siyo safi,na mioyo yetu ni yenye ouvu, tutaona maisha yetu yamekuwa ya kujitumikia na tunatamani sana kuwekwa huru. Basi tutakuwaje na mapatano na mapenzi ya Mungu?

Hitaji letu ni kuwa na amani - baraka za Mungu ni amani na upendo. Amani hii fedha haiwezi kugarimia; hata kupitia kwa bidii au hekima yetu. Hatuwezi kuipata kwa juhudi zetu. Hata hivyo Mungu ametupea kama Zawadi, "bila pesa na dhamana yoyote" (Isaya 55:1). Baraka hizi ni zako, ikiwa utaonyesha mikono yako na kuipokea. "haya, njoni tusemezane, asema Bwana. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu." Isaya 1:18. kama itakuwa ndio mwelekeo wetu, Yesu anasema, "Nami nitawapa ninyi moyo mpya, nami nitatia moyo wa jiwe uliomo ndani ya mwili wenu, nami nitawapa moyo wa nyama".(Ezekieli 36: 26)

VAZI JIPYA - LIZILOHITAJIKA!

Lengo letu dhambi ni lazima iondolewe kabisa. Tunahitajika kupeana dhambi zetu zote kwake Yesu, ndipo aweze kupatanisha dhambi zetu ili kuwezesha sisi kuokolewa. "Sasa, Yoshua alikuwa amevaa nguo chafu sana, naye alikuwa akisimama mbele ya malaika, na akajibu na akawaambia wale waliosimama mbele yake "akasema, mvueni nguo hizi zenye uchafu. Kisha akamwambia yeye, tazama, nimekuondolea uovu wako, nami nitakuvika mavazi ya thamani nyingi." (Zekaria 3:34)

Kinyume na hayo yatuonyesha; wale watakao kataa kutubu makosa yao, wale walio na kiburi kujinyenyekeza mbele za Bwana, basi hao Mungu hatawasamehe, mshahara wa dhambi ni mauti. Dhambi lazima iondolewe ndani yetu, kabla sisi kuhesabiwa wenye haki.

Katika kitabu cha Luka 15, Yesu aelezea mifano mitatu jinsi ya anavyo watafuta wale wamepotea mbali na Mungu katika mfano wake wa mwisho , anaelezea kuhusu "mwana aliitisha urithi wake , na kufanya hivyo a kaondoka nyumbani akatumia vibaya mali yake yote na mwishowe akamalizia lula na nguruwe. Ni kweli biblia yasema alitamani kula na nguruwe. Baada ya siku nyingi akarudiwa na fahamu zake na akafamu ya kuwa katika njia

yake hamna matumaini ya baadaye.Akaamua aende nyumbani kwa baba na akchukua hatua kwa uamuzi wake mwenyewe .akatoka akaenda nyumbani kasha huyo mwana akiwa bado mbali na nyumbani , baba yake akamuona kwa mbali, akiwa mchafu ,na amerararukiwa.Wakati baba ye amuona jinsi alivyo akamhurumia.akamkimbilia akamkumbatia akambusu na yule mwana akamwambia bambaye mimi nimekosa mbele ya mbingu na mbele yako na sisitahili kamwe kuitwa mwana wako, lakini baba yake akaambia wale watumishi wake , leteni lile vazi nzuri mmvarishe na mmtie na petemkononi na viatu miguuni na mlete ndama yule aliyenonamkamchinje nasi tule na kufurahi .Kwa kuwa huyu mwanangu alikuwaamekufa naye amefufuka, alikuwa amepotea naye ameonekana. Wakaanza kufurahia"Luka 15:21-24

Katika hadithi hii, kuvalishwa kunaakilishwa na vazi la la haki ya Kristo, kwanza, mwana ni lazima awe na nguo zile zake chafu kasha akavuliwa na kupeawa nguo mpya ya kuvaa. Kwa njia hiyo hiyo, mwenye dhambi hupokea vazi la Kristo kwa njia ya neema kupitia kwa imani. Wakati arudiapona kutarajia wokovu unaopatikana kwa Yesu Kristo.

Sasa swali ni hili, Je, tutazidi kuishi maisha ya dhambi, ya kufa na umasikini-Kuishia katika chakula cha kiroho cha nguruwe, au tutakubali kukumbatiwa na mkono wa Mungu wa furaha unaowapokea wenye dhambi wote watubuo? Uchaguzi ni wako, uchaguzi ni wangu, lakini yafaa tufanye uamuzi, hatuna faida kwa kupata malipo ya nguruwe! Lazima tuchukuwe hatua, lazima tuende kwa Yesu na tupokee kipawa cha wokovu na uzima wa milele.

Wokovu—Kwa Masharti

Hebu sisi wakati tunapo kuwa katika mapabano makali, tutafakali baadhi ya ahadi za Mungu: "Tukiziungama dhambi zetu, yeye ni mwanifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote." 1 Yohana 1:9. "Afichaye dhambi zake hatafanikiwa; bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema". Mithali 28:13 kama tunavyoona, ni lazima wokovu upeanwe katika masharti fulani. Yesu amefanya yote ili aweze kutuokoa na ni wajibu wako na sisi kuukubali au kuukataa wokovu. Wakati Mfalme Daudi alitambua ametenda dhambi, alisema, "Nimefanyia Bwana dhambi" (2 Samweli 12:13). Alirudi akaelezea jambo hilo; "Nalikujulisha dhambi yangu wala sikuuficha upotovu wangu nalisema nitayakiri maasi yangu kwa Bwana nawe ukanisamehe upotovuwa dhambi yanguHata Eliya alipoona kuwa hapana jawabu katika vinywa vya watu hao watatu, hasira zake ziliwaka ——"Ps 32:5.

Hivyo ndivyo Yesu alivyo, atamsamehe yeyote atakayetubu, na kupeana dhambi zake na kuachana na tabia zake za upotovu. Jambo hili likitendeka, kutakuwa na mabandiliko ndani yake. Paulo anaelezea jambo hili katika maneno haya; "Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya" (2 wakorintho 5:17). Mawazo yako yanabadilishwa kwa sababu Roho mtakatifu ameingia katika maisha yako.

Sisi tunahitaji mabadiliko ya maisha yetu kutoka kwa mwanzilishi wa uwezo wote, kupitia kwa Roho mtakatifu. Naomba wote wakubali mwito huu! Kuna heka heka nyingi, binadamu wako katika harakati nyingi na kwa sababu dunia inazidi kufanya maovu na mambo yasiyo mpendeza Mungu, na mabadiliko haya yatatubadilisha sisi, tusipo utafuta mkono wake Bwana na tuanze kutembea naye leo.

MSAMAHA

Yesu anasema katika ombi la Bwana, "utusamehe deni zetu kama tunavyo wasamehe wadeni wetu." (Mathayo 6:12). Pia katika waraka wa Yakobo anasema; "ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, mpate kuponywa. Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii." (Yakobo 5:16). Hili linatuonyesha ikiwa mmoja wetu amemkosea rafiki au jirani yake, ni lazima atubu hizo dhambi kwa hao na, ni lazima kwa hiari wakubali kumsamehe. Ikiwa umekosa hadharani utahitaji toba ya hadharani, Makosa tunayotendeana yahitaji kutubiwa kwa aliyekosewa . Msamaha wa mwisho utapatikana kutoka kwa Mungu kupitia Yesu Kristo. Lazima tuweke dhambi zetu zote kwake Yesu, ndipo aweze kuitakasa! Kuoshwa kwa moyo wako ni kitu cha dhamana kubwa, kwa kuwa Yesu anasema——"Heri wenye moyo safi; maana hao watamwuona Mungu". (Mathayo 5:8) zaidi Yohana anasema, "Na ndani yake hakitaingia kamwe cho chote kilicho kinyonge, wala yeye afanyaye machukizo na uongo bali wale walioandikwa katika kitabu cha uzima cha mwana kondoo.. (Ufunuo 21:27).

KAZI YA ROHO MTAKATIFU

Sisi tutafikiaje kuwa na uamuzi wa kutubu dhambi zetu? Roho mtakatifu anazidi kutuita tujinyenyekeshe mbele za Mungu (Wafilipi 2:13). Jambo hili linatupa uwezo wa haraka wakutokataa. Tunatakiwa kujinyenyekesha na kusalimisha mapenzi ya mioyo yetu na kuzitubu dhambi zetu. Basi Yesu atabeba lawama zetu. Neema yake kwa imani, tunafanywa wenye haki bila ya sisi kutenda lolote nzuri.

Mungu Baba atatuhesabia sisi ni wenye haki, kwa kuwa haki ya Yesu tumehesabiwa kuwa ni yetu. Nabii Isaiah anaelezea msamaha huo hivi; "Nitafurahia sana katika Bwana, nafsi yangu itashangilia katika Mungu wangu, maana amenivikwa mavazi ya wokovu, amenifunika vazi la haki, kama bwana harusi ajipambavyo kwa kilemba cha maua, na kama bibi arusi ajipambavyo kwa vyombo vya dhahabu." Isaya 61:10. Pia Paulo anaelezea vile vile. "Basi tukiisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani, na tuwe na amani kwa Mungu, kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo", (Warumi 5:1) uamuzi na imani hii hatupaswi kuikataa, kama tunahitaji wokovu. "Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake; (Yohana 1:12)

KIBURI

Kwa rafiki mpendwa, usikubali kiburi kiwe kikwazo cha kutozipeleka dhambi zako kwa Yesu. Fungua moyo wako kabisa kwake bila kujibakishia cho chote. Ni afadhali utubu dhambi zako sasa, kuliko kuwaachia watakaookolewa kutoka kuchunguza maisha yako na kuona dhambi zako za siri na zile zilizo wazi wakati waliookoka watakapofika mbinguni, na kuungana ili kuhukumu wasiomcha Mungu. Na wataziona rekodi za waliopotea, na sababu za kupotea kwao. (Ufunuo 20:4). Waona huna lolote lakupoteza, kwa kuziweka dhambi zako zote kwake Yesu. Utapata faida kwa kufanya vile. "wote wajao kwangu", Yesu anasema mimi sitawatupa (Yohana 6:37). Hakuna dhambi ambayo ukitubu kwa moyo wako wote, yeye atashindwa kukusamehe. Yeye ana upendo mwingi ili atusamehe. Hata hivyo, twahitaji kunyenyekea na kutubu dhambi zetu. Hebu fanya hivyo sasa! Usikatae useme kesho au siku nyingine ndio utafanya hivyo. Unaweza kupumzika sasa hapa, na kutengeneza maisha na

mwelekeo wa maisha mapya. Ikunje mikono yako na umumwagie yote kwake Yesu Kristo. Hebu fanya hivyo e kwa imani, bila kuwa na mashaka. Utafunguliwa na kuwa huru, huru kutoka kwa minyororo ya dhambi,kwa sababu " mwana akikuweka huru utakuwa huru kwelikweli (Johana 8:36) hebu fanya uamuzi wako sasa. Jambo hili likifanyika Yesu anasema, "Amani yangu ndio ninayowachia; siyo kama ulimwengu uwapao, ndio niwapao" (Yohana 14:27) sisi tunahitaji amani hiyo! Ulimwengu hauwezi kutupa, lakini Yesu ameweza.

UBATIZO WA IMANI

Imeandikwa, "yeye aaminiye na kubatizwa ataokoka" (Marko 16:16). Pia Bibilia inasema "amani inakuja kwa kusikia na kusikia kupitia neno la Mungu", (Warumi 10:17). Ingawaje hatuwezi kumwona Yesu, ni lazima tuamini yeye aliye chanzo cha historia na majira (B.C A.D). yeye ndiye katikati ya yote yalio katika Bibilia. Ni katika yeye tu tunaweza kuokolewa. Ingawaje hatumwoni leo, amejifunua kupitia kwa neno la Mungu.

Tangu sasa, "imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana". (Waebrania 11:1). Ni Yesu Kristo ambaye anaweza kutuokoa katika dhambi. Yatupasa kumwamini yeye Yesu mwenyewe aliyesema:, "mimi ndimi njia, na kweli, na uzima, mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi, "Yohana 14:6". Pia imeandikwa hivi —— "wala hakuna wokovu katika mwingine yeyote kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo." (Matendo 4:12) Budha au Mohammed au Papa hawezi kutuokoa. Hawa wote ni viumbe wenye kukosea.

Ni muumba pekee, Yesu Kristo, ambaye aliishi bila kutenda dhambi, anaweza kuokoa kabisa wote wajao kwake kwa imani. Wewe waamini hivyo? Wewe wataka kukata kauli kabisa umwaamini Yesu Kristo, na umfuate, umtii na ufunuo wake katika Bibilia; ndani ya habari njema tutapata amri kumi za Mungu, lakini haijalishi gharama zake? Ikiwa vile, hatua ifuatayo ni kujiandaa kwa umbatizo.

Imani na matendo huenda pamoja. Yakobo anaiweka hivi,"Lakini mtu asema wewe unayo imani nmi ninayo matendo ,nionyeshe imani pasipo matendo nami nitakuonyesha imni yangu kwa njia ya matendoYakobo 2:18-26 " Paulo asema hivi "lkwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zetu, ni kipawa cha Mungu." Wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu. Kwa maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo," (Waefeso 2:8-10) kwa kila ambaye amempokea Yesu Kristo kuwa mwokozi wa maisha yake, itakuwa jambo la kawaida la kimaumbile, kudhihirisha imani kwa matendo na ubatizo ni moja wapo wa kitendo cha imani.

KABLA YA UBATIZO: NI LAZIMA UYAFAHAMU YAFUATAYO:

Neno "BATISO" au ubatizo, limetokana na neno la kigriki "baptismo", lilichotumiwa na watengeza viuma. Maana yake ni kutumbukiza cho chote ndani ya maji, hadi kifunikwe kabisa. Kwa mfano mtegenezaji huyu akiwa na kipande cha chuma, na ataka kiwe kwa muundo mwingine kwa aina yake. Hivyo basi atakitumbukiza kile kipande hadi kifunikwe na maji kabisa. Kwa mfano huo huo, wale ambao wako katika darasa la ubatizo, huzikwa ndani ya maji hadi huyu mtu afunikwe mwili wote na maji. Kwa njia ya ubatizo, mfano unapatikana wa kudhihirisha kupokelewa kwa mauti yake Yesu, kuzikwa na ufufuo wake

kwa mauti yake Yesu. Zaidi ya hayo, ubatizo unamaanisha, utazika uzito wako wa dhamiri iliyo kushitaki ndani ya maji na unafufuliwa katika upya wa maisha pamoja na Kristo. Maandiko yafuatayo yanatoa ushahidi huo. "Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake, basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatiso , katika mauti yake kusudi kama Kristo alivyofufuka wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima." (Warumi 6:3-4) "mfano wa mambo hayo ni ubatizo, unaowaokoa ninyi pia siku hizi; (siyo kuwekea mbali uchafu wa mwili, bali jibu la dhamiri safi mbele za Mungu), kwa kufufuka kwake Yesu Kristo." (1 Peter 3:21).

Kama wewe, katika maisha ya kila siku utaingia mkataba na mtu yeyote, ni jambo la muhimu kujua mambo ambayo yanaleta mapatano, kabla kutia sahihi katika huo mkataba. Pia ndivyo kulivyo kabla ya mkataba wa ubatizo. Kabla ya ubatizo, unatakiwa kuutumia muda wako mwingi ukichunguza na kutafuta neno la Mungu, kukaa katika maombi ndipo uweze kuelewa maana ya mkataba wako. Na ndipo kuna maana ya kuzungumzia "ubatizo wa imani", au ubatizo wa watu wazima." kabla ya ubatizo ni lazima ufikilie kauli yako na kuchagua kumwachia Mungu akubadilishe na uombe nguvu za kumfuata Yesu ziku zote. (1 Petero 2:21). Ubatizo ni dhihirisho la kubadilika ambao umepatikana ndani yako.

UBATIZO WA WATOTO WACHANGA

Kama vile tumeona na kumalizia, hakuna ambaye anafaa kubatizwa kabla ya kuamini, mtoto mchanga ambaye amepokea matone kadhaa usoni au kwa kichwa chake, yaliyo nyunyizwa na mhubiri, au padre, sio ubatizo ulio katika Bibilia. Hujaweza kufunzwa na kujua lililo kweli au mbaya (Heb 5:13-14). Ujumbe wa Yesu wa kutuokoa, kutoka katika dhambi, haujaeleweka vilivyo. Hivyo, hana imani yake mwenyewe. Kwa kuwa Bibilia inasema, "yeye aminiye na kubatizwa ataokoka"(Marko 16:16) na pia, "imani huja kwa kusikia na kusikia huja kwa neno la Kristo" (Warumi 10:17) ubatizo lazima ufanyike tu baada ya mhusika kumpokea Yesu Kristo. Kuwamiminia watoto wachanga maji, siyo ubatizo kamwe, lakini ni mtindo wa watu wanaojiona wao ni wazuri. Hivyo kama huo wa watoto wachanga, lazima wabatizwe jinsi ya Bibilia.

KUKUBALIKA

Kanisa la katoliki lilianzisha ibada hii ya kukubalika katika enzi ya kumi na tatu (13th century). Inajulikana vyema kwamba, hakukuwa na mtindo huu wa watoto wadogo kubalika au watu wazima ndani ya kanisa kati ya walio mwamini Yesu Kristo kama mwokozi wa maisha yao. Jambo hilo linatuonyesha eti kukubalika huku, haina maana yoyote. Kabla Yesu kupaa mbinguni aliwafundisha mitume wake, akawambia walihubiri neno, pia ametuamuru sisi. (Mathayo 28:18-20) na ubatizo wa watoto wachanga, na ibada ya kukubalika hayakuwepo katika mafundisho yake. Haya ni mafundisho yasio ya Bibilia.

BAADHI YA MIFANO YA UBATIZO

Kuna mifano mingi ya ubatizo katika Bibilia. "Wakati Filipo alihumbiria injili ya Yesu kwa yule mhabashi mkushi, mhabashi alimwambia Filipo, tazama hapa kuna maji, ni nini basi kitanizuia mimi kubatizwa? akaamuru lile gari lizimame wakateremka wote wawili majini Philipo na yule towashi naye akambatiza.Matendo 8:26-38".

Philipo alipoihubiri injili kule Samaria, wengi waliupokea ujumbe. Bibilia inazidi kutuambia mazao ya mahubiri ya Filipo. "lakini walipomwamini Philipo, akizihubiri habari njema za ufalme wa Mungu, na jina lake Yesu Kristo wakabatizwa, wanaume na wanawake." Matendo 8:12 .

Na baada tu ya pentakote Petro na wanafunzi wengine walitokea wakisema "Basi nyumba ya Wairaeli na wajue ya kwamba Mungu amemfanya Yesu huyo mliyesulubisha kuwa Bwana na Kristo.Walipoyasikia hayo , wachomwa mioyo yao, wakamwabia petro na mitume wengine , tutendeje ndugu zetu? Petro akawaambia, tubuni mkabatizwe kwa jina la Yesu Kristo mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho mtakatifu"Matendo 2: 37-38

Vile vile Yohana mubatizaji alipotokea jagwani, aliwahubiria watu kwa kilio: "Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia ——— naye akawabatiza katika mto wa Yordani, huku wakiziungama dhambi zao." (Mathayo 3:1-6) Tunaona vyema kuwa ubatizo unatokana na mtu kutubu dhambi zake, na mtu mwenyewe kupokea ujumbe kumhusu Yesu Kristo kama mwokozi wa imani.

Bibilia inasema, kuna "Bwana mmoja," (Waeteso 4:5). Kwa hivyo, ubatizo wa bibilia ni ubatizo wa imani, ambapo muumini anazikwa ndani ya maji na Kristo. Iwapo unatalajia ubatizo huu, ni lazima ufuate nyayo zake Kristo. Yeye alizikwa mto Yordan, ingawaje haikuwa ni lazima afanye vile, lakini alifanya vile kuwa mfano kwetu, ndiposa tutembee katika hatua zake. (Mathayo 3:1-17) na (Petro 2:21)

Rafiki mpendwa, Bibilia inaonyesha wazi wazi kuwa, ubatizo wa imani, ni wa maana kubwa. Imeandikwa; "yeye aaminiye na kubatizwa ataokoka (Marko 16:16). Mara tu tunapoipokea imani ya Yesu, imani iliyokuwa ya kunyenyekea, Yesu aliyokuwa nayo, basi sisi tu tayari kwa ubatizo. Yakobo 4:17; inasema "yeye ajuaye kutenda wema, walakini hatendi, kwake yeye ni dhambi. "Hata katika ubatizo ni hivyo hivyo. Ikiwa wewe kupitia neno la Mungu unaweza kutuambia ubatizo wa imani ni wa kweli, na ujabatizwa katika huu ubatizo, unatakiwa umtafute mhubiri au mchungaji anaye ihubiri imani ya Yesu Kristo ndipo jambo hili liweze kufanyika. Yesu alimwambia Nikodemu maneno yaliyomsumbua katika mawazo yake; "Amin, amin, nakuambia, mtu asipozaliwa mara ya pili hawezi kuuona ufalme wa Mungu. (Yohana 3:3-6). Historia hii inatuambia, eti Roho mtakatifu bila ya kusita, hutuvuta tumkumbali Yesu, na kumfuata. Yesu anailezea hivi "upepo huvuma upendako, na sauti yake waisikia, lakini hujui unakotoka wala unakokwenda; kadhalika na hali yake kila mtu aliyezaliwa kwa Roho mtakatifu katika moyo wa binadamu anafananishwa na upepo, kuwa huwezi kuona kamwe. Lakini kazi zake huonekana vyema. Hutenda kazi kwa nguvu na kufanya upya maisha, kazi ambazo hakuna awezaye kuziona, huleta uhai upya katika moyo; huumba mfano wa Mungu katika binadamu. Hebu na tuyafungue maisha yetu kwake Mungu na uwezo wake. Na basi maisha yetu yote yatabadilika kabisa kuanzia hapo tutakuwa watumishi kuliko kuwa vingozi, tutakuwa wenye huruma kuliko kuwa wasio na huruma, tutakuwa wenye upendo kuliko kuwa wenye chuki, tutakuwa marafiki kuliko kuwa wenye kupenda vita na tungeendelea. Hivi ndivyo Roho mtakatifu alivyo, anafanya kazi ndani ytu kwa knia na kutenda mapenzi ya Mungu (Filipo 2:13). Kwa rafiki mpendwa, usikatae, mwito wa roho mtakatifu, na umkaribishe lakini mkaribishe aingie maishani mwako. Jambo Fulani la furaha sana liingia maishani mwako

Hivyo ndivyo, tunavyo kuwa mashahidi wazuri wake Yesu mwana wa Mungu.

MAISHA NDANI YA KRISTO

Mara tu tunapoamua kumfuata Kristo, na tumebatizwa katika njia ifaayo ya Bibilia, tutaendelea kuishi ndani ya Kristo na kuendanisha naye popote aendako. Hapa hapana ghalama yoyote, yakuwa tunaye adui, shetani, anayejaribu kutuangusha na majaribu ya kutufanya kutenda mambo maovu. Tusipo shikamanishwa imara katika Kristo, tusipokuwa na mshikamano imara naye, tutakubaliana na mujaribu wetu kwa majaribu yake. Yakobo ana haya yakusema; "Heri mtu astahimiliye majaribu, kwa sababu akiisha kukubalika ataipokea. Mtu ajaribiwapo, asiseme, nimejaribiwa na Mungu; maana Mungu hawezi kujaribiwa na maovu, wala yeye mwenyewe hamjaribu mtu. Lakini kila mmoja hujaribiwa na tamaa na kudanganywa. Halafu ile tamaa ikiisha kuchukua mimba huzaa dhambi, na ile dhambi ikiisha kukoma huzaa mauti" (Yakobo 1:12-15)

Katika utangulizi tuliandika kuhusu vita dhidi ya mwili na Roho. Mwili ni sehemu mmoja yetu. Shetani hutujaribu kupitia mawazo yetu, lakini hatutaruhusu mwili ututawale.

Tutafuata sauti ya Mungu, ushauri wake na uongozi wake. Muumbaji anayajua yale yanayofaa viumbe vyake, na amri kumi zilianzishwa ili tukae na furaha katika Mungu pamoja na wenzetu. Amri hizi fupi kumi, inatakiwa sisi tujifunze mioyoni mwetu kama zilivyoandikwa kutoka 20:3-17. Tunapokuwa na umoja na amri za Mungu, tuko na ushirika naye, aliyetuumba sisi.

Vita kali dhidi ya ubinafsi ndio vita kuu imewahi kuwepo. Kusalimisha ubinafsi, kukata kauri kumfuata mapenzi ya Mungu kabisa, na kujinyenyekesha kwa moyo, kudhidirisha upendo, urafiki, na matunda mengi mema" ni kati ya mambo hatuwezi kuyatenda kupitia uwezo wetu. Walakini tukiwa na nguvu zake mwenyezi Mungu katika maisha, tunaweza kupata ushindi hata katika sehemu hiyo. Maisha matakatifu na tabia ya Kristo ni mfano mzuri jinsi tunavyoweza kushinda ubinafsi. Imani yake kwa baba wa Mbinguni haikuwa na mipaka. Utiifu wake na kujipeana kwake havikuwa na vizuizi walakini alikuwa kamili. Hakuja kutumikiwa, bali kutumikia wengine. Hakuja ili mapenzi yake yafanyike, lakini mapenzi ya Baba, aliye mtuma yeye. Katika yote alijipeana kwake, yeye ambaye hukumu yake ni ya haki. Yesu anasema —————"siwezi lolote kwa uwezo wangu"(Yohana 5:30). Mungu anaweza na anataka kuwapa watumishi wake, uwezo wowote wanaouhitaji, hata ikiwa ni maarifa kuhusu jambo lolote. Yeye atawatimizia jukumu la hali yeyote kwao wanao weka tumaini lao kwake.

Sasa tutatumia mifano kadhaa kutoka kwa uumbaji unaolezea kukua kwa Mkristo: ukipanda mbegu shambani, mmea huo utaendelea kukua, ikiwa mbegu hiyo itapata maji ya kutosha joto na jua, jinsi mbegu inavyomeaya hili hufunua wazi mwanzo wa maisha ya kiroho. Maisha ya kikristo huendanisha sabamba na mambo yaliyo katika maumbile: hawezi kuwa na uhai bila ya kukua. Vile vile ni lazima kila mche ukue au ufe. Jinsi mche unavyokuwa kimya kimya bila ya kutambuliwa, pia ndivyo maisha yako ya ukristo yanavyokuwa. Maisha yako yanaweza kuwa kamili katika hatua zako zote za kukua: ili mpango wa Mungu kwetu uweze kufaulu, itatulazimu tuendelee. Utakazo ni kazi ya maisha. Katika kila wajibu, tutapata ujuzi na kuzidi katika maarifa. Tutapata nguvu za kuyafanya majukumu yoyote na tutakuwa katika majukumu yanayo tukabili. Na tutaendelea sasa kuwazua jinsi mkristo anakuwa katika kristo. Kama ilivyo na mmea, hata wewe unakuwa hatua kwa hatua. Mmea hukua kwa kupokea vitu vyenye kutengezwa na Mungu ili kuukuza. Huichimbia mizizi yake chini ya mchanga. Huupokea mwangaza wa jua na pia kunyeshewa na manyunyu ya mvua au umande.

Hupokea pia hewa inayo tupa uhai. Hivi ndivyo, mkristo hukuwa, wakiwa na ushirika na Mungu. Wakati tunapotambua kushindwa kwetu, ni wajibu wetu kutumia kila uwajibikaji tunayopewa ndipo tuwe na uzoefu wa kindani. Kama jinsi yake mumea unapo ichimbia mizizi yake chini ya mchanga, ni lazima hata sisi tuwe na mizizi ndani ya Kristo. Kama jinsi mimea inapata mwangaza, umande na mvua hata sisi lazima tupokee Roho mtakatifu katika mioyoni mwetu.

Bibilia inaelezea Yesu akiwa mtoto mchanga katika maneno machache. "Yule mtoto akakua, akaongezeka nguvu, amejaa hekima, na neema ya Mungu ilikuwa juu yake——naye Yesu akazidi kuendelea katika hekima na kimo, akimpendeza Mungu na wanadamu." (Luka 2:40,52).

Mfalme Suleimani mwenye hekima, anaelezea kwa undani ni maarifa na hekima ipi: "mwanangu, kama ukiyakubali maneno yangu, na kuyaweka akiba maagizo yangu; Hata ukatega sikio lako kusikia hekima, ukauelekeza moyo wako upate ufahamu; ukiutafutia kama fedha, na kutafutia kama hazina iliyositirika; ndipo utakapofahamu kumcha Bwana, na kupata kumjua Mungu.

Kwa kuwa Bwana huwapa watu hekima; kinywani mwake hutoka maarifa na ufahamu, (Methali 2:1-6). Yesu alipokea maarifa na hekima kutoka katika neno la Mungu. Pia hata sisi lazima tuwe na uwajibikaji wa kila siku kutafuta kwa maombi na kulichunguza neno la Mungu. Jambo hili litatuongeza maarifa katika Mungu, na kutusaidia sana katika maisha yetu kama wakristo.

Ni ndani ya Bibilia tunapata maelezo sahihi, kuwa ni jinsi ngani tutakuwa ndani ya Kristo. Kulingana na neno lake; "kaeni ndani yangu, nami ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa peke yake, lisipokaa ndani yangu ya mzabibu; kadhalika nanyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote." (Yohana 15:4-5)

Jinsi matawi hayawezi kukua, na kuzaa matunda, yakiwa yametenganishwa na mti mwenyewe, pia hata sisi hatuwezi kuishi maisha ya Mungu bila Kristo. Twajua vyema kuwa sisi kuishi bila Kristo, tunakuwa matawi yanayo katwa kwa kutozaa. Haya yanaweza kutupata sisi, ikiwa hatutaendelea kuwa na uhusiano na Kristo - maisha yetu ya kiroho yatakufa. Baada ya kifo cha kiroho, tutakosa uwezo wa kushinda majaribu, kuwa katika neema na utakatifu. Lakini tukiendelea kuwa ndani ya Kristo, tutakuwa na kuendelea kuwa wenye furaha. Sisi tukiywa kutoka kwake; sisi hatutadhofika au kutokua na mazao, walakini tutakuwa kama mti uliopandwa kando ya mto ulio na maji mengi. Wengi mwanzoni hupokea wokovu katika Yesu Kristo, lakini hujaribu kuishi maisha matakatifu kwa bidii yao wenyewe. Jaribu kama hilo halina mazao kamwe. Tulisoma maneno kama hayo sekondi kadhaa zilizo pita; "bila mimi hamwezi chochote" kukua kwetu kwa neema, furaha yetu, mambo mazuri tunayoweza kufanya, yote yanategemea kushikamana kwetu na Kristo. Ni kwa njia yakuwa na uhusiano wa kila siku naye, kila saa, hata kila sekondi kukaa ndani yake, ndio tunaweza kukua katika neema. Siyo tu kuwa katika mawazo yetu kila asubuhi, lakini ni kuwa ndani yetu wakati wetu wote. Basi tutakuwa kama mbegu na bila shaka kuwa mazao ambayo yako tayari kuvunwa wakati Yesu atarudi." (Ufunuo 14:13-15; 1 Th 4:15-17).

Penginepo, waweza kujiuliza "mimi nitawezaje kuishi ndani ya Kristo?" Utaishi jinsi tu vile ulivyo mpokea. Bibilia inasema _ "basi kama mlivyompokea Kristo Yesu, Bwana,

enendeni vivyo hivyo katika yeye…..(Wakolosai 2:6) sasa mwenye dhambi ataishi kwa imani. (Waebrania 10:30). Ulijipeana kwa Mungu ndiposa uwe wake kabisa, uweze kumtumikia, kumtii, na uliweza kumpokea kama Mwokozi wa maisha yako. Haukuweza kwa jinsi yeyote kuleta upatanisho na dhambi zako, au kubadili moyo wako au mafikara yako, Yesu alifanya haya kwa imani, umekuwa mali ya Kristo, na kwa imani, utaendelea kukua katika yeye kwa kupokea na kupeana. Lazima uyatoe yote - Moyo wako mapenzi yako, utumishi wako, kujisalimisha kwake na kutii amri zake. Kwa njia sambamba, ni lazima umpokee Kristo, aliye mwanzo wa Baraka zote. Mkubalie aishi katika moyo wako na awe uwezo na nguvu zako, awe haki, msaidizi wa maisha yako yote, ndipo upokee uwezo wa kuishi na kutii.

Yesu anasema "ikiwa mwanipenda mtazishika amri zangu" (Yohana 14:15). Yohana, mtume aliyependwa sana, anaelezea hivi; "katika hili twajua kwamba twawapenda watoto wa Mungu, tumpedapo Mungu, na kuzishika amri zake, wala amri zake si nzito"(1 Yohana 5:2,3). Wengi husema kuwa "ni kuhubiri watu waitii sheria. Walakini mambo hayo ni mafunzo ya Bibilia. Walakini ikiwa sisi kwa uwezo wetu bila kufanikiwa tutajaribu kutii sheria, hivyo basi sisi tutakuwa wenye kutunza au kujaribu kuiweka sheria. Na tukisha jua yale Kristo ametufanyia ili aweze kutuokoa, tutayafikiria sana mambo mepesi sana yalio andikwa katika amri kumi, ambayo Mungu alianzisha ili tuwe na uhusiano kamili na binadamu wenzetu na Mungu pia. Hatutaweza kushika sheria kwa uwezo wetu, walakini roho mtakatifu akiingia katika maisha yetu, basi tutakuwa na nguvu zinazo hitajika kutunza amri kumi za Mungu, kama ilivyo katika kutoka 20:3-7. je wewe unaamini haya?

Wewe unaamini yakuwa yesu anauwezo kuliko shetani? Wewe unaamini Yesu anaposema, "nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani?" (Mathayo 28:18). Atagawa nguvu zake zingine? Kabla hajapaa kwenda mbinguni, Yesu aliwaambia mitume wake; "lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu roho mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi. "Mitume 1:8 Paulo anaelezea hivi "Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu ila Mungu ni mwaminifu, ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili." (1 Wakorintho 10:13) Petero na mitume walisema——"Na sisi tumashahidi wa mambo haya, pamoja na roho mtakatifu ambaye Mungu amewapa wote wamtiio. (Matendo 5:32) katika mahubiri mlimani Yesu alisema; "si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni." (Mathayo 7:21). Zaidi ya hayo, "—— naye alipokwisha kukamilisha, akawa sababu ya wokovu wa milele kwa watu wote wanaomtii." (Waebramia 5:9) maandiko haya yanatuambia Mungu ametuahidia roho kutenda mapenzi yake, na ni Mungu anayeamua eti ni furani nitakayempa huyo roho wake. Hebu fikiria chanzo cha uweza ambao utapewa wenye kushirikiana na Mungu.

Katika siku ya Pentekosti, mitume walinyunyiziwa kwa kipimo kikubwa cha uweza wa roho mtakatifu. Waihubiri injili kwa uwezo mkubwa, nayo kazi ya Mungu ikaharakishwa kwa uwezo mwingi. Katika hizi siku za mwisho, watu wa Mungu watapokea huyo Roho ili waende kuenezwa ujumbe wa malaika wa tatu, sana sana malaika huyo wa tatu (Ufunuo 14:12) ukipelekana na ujumbe wa TOKENI BABELI(ufunuo 18:4) wakati ni huu wakujiandaa kupokea "mvua wa masika" ya roho mtakatifu. Huu ndio wakati wa kujinyenyekesha mbele za Mungu na tutambue dhambi zetu, na tujiweke wakfu kwake

upande wake Yesu ndio tuweze kupokea baraka na tuwe na sehemu katika kazi ya kufunga historia ya ulimwengu. Sisi tusipo chagua kumfuata Yesu kabisa bila ya kujibakishia, Roho mtakatifu atawashukia wale walio karibu nasi lakini siyo juu yetu.

Hapo mbeleni tuliona kuwa Yesu ni mwenye haki, na wote wampokeao kama mwokozi wao kwa imani watahesabiwa wenye haki kwa ajili yake. Pia tuliona, kuwa tukiwa na nguvu za roho mtakatifu watatenda haki. Tutaendelea kusoma mistari mingine katika maandiko kuhusu mambo haya. Paulo anaandika haya "Bali katika kila taifa mtu amchaye na kutenda haki hukubaliwa na yeye."(Mitume 10:35). Zaidi ya hayo Paulo anaelezea ukweli huu. "kwa sababu sio wale waisikiao sheria walio wenye haki mbele za Mungu, bali ni wale waitendao sheria watakaohesabiwa haki." (1 Yohana 2:13). Maandiko mengine yasema "watoto wadogo, mtu na asiwadanganye; atendaye haka yuna haki, kama yeye alivyo na haki, (1 Yohana 3:7) zaidi sana "kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao wake wakaa ndani yake; wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa kutokana na Mungu." (Yohana 3:9) Yesu alimwambia Nicodemu "Yesu akajibu, Amin, Amin, nakwambia, mtu asipozaliwa kwa maji na kwa roho, hawezi kuingia ufalme wa Mungu." (Yohana 3:5).

Ni Roho mtakatifu awezaye kutupea uwezo wa kuishi maisha matakatifu, hatuna jambo lolote tunaweza kujisifu sisi wenyewe. Utukufu uwe kwa Mungu kwa kila ushindi na msaada! Sasa hatuwezi kuingia katika ufalme wa Mungu bila ya kupokea haki yake Yesu, ambayo hatukufaa kuipata, ila tu katika neema kwa njia ya imani. Matunda ya kupokea haki ya Kristo ni kuwa Roho mtakatifu huja na kuishi ndani yetu, na huwa msaada wetu sisi kutenda haki. Anatusaidia kutunza Amri za Mungu. Mmowapo wa maandiko katika Bibilia inasema "Heri wazifuao nguo zao, wawe na amri kuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa milango yake" (Ufunuo 22:14)

Maandiko yanajielezea vyema yenyewe. Imani yako itamulikwa na matendo yako. Kuhusu haya, Yakobo anasema; "maana kama vile mwili pasipo roho umekufa, vivyo hivyo na imani pasipo matendo imekufa." (Yakobo 2:26)

Yafuatayo yamesemwa kuhusu wataookolewa kabla ya Yesu kurudi dunia-ni "nikamwambia Bwana wangu, wajua wewe, akaniambia, hao ndio wanatoka katika dhiki ile iliyo kuu, nao wamefua mavazi yao na kuyafanya meupe katika damu ya mwana kondoo. (Ufunuo 7:14) nikiongezea ….. "naye amepewa kuvikwa kitani nzuri, hiyo ni matendo ya haki ya watakatifu.(Ufunuo 19:8)

Wakati Yohana alipofundisha kuhusu kukubalika na ubatizo, aliwaambia wale walio fikilia kuwa walikuwa na hekima kutoka kwa Mungu; "Basi zaeni matunda yapasayo toba;" (mathayo 3:8). Yesu hataki tu tuwe wenye kulisikia neno, bali lakini hata tuwe wenye kulitenda. (Yakobo 1:22) kwa kuwa Roho mtakatifu yuko katika maisha yetu, tutapokea nguvu za upendo, urafiki, wenye kujali wengine, kusaidia na wenye huruma na mengineo. Matunda ya roho mtakatifu yatadhihirishwa katika maisha ya Yesu. Tutafanana na yeye zaidi na zaidi katika tabia. Tutakuwa tukitembea katika njia ya utakatifu, Yesu ametupa sisi mfano ili tufuate mfano wake." (1 Petero 2:22)

Kristo anataka mengi kutoka kwetu, walakini kwa uwezo wake, hatua kwa hatua tutazidi kufanana na yeye. Tunaweza kujiona kuwa wakamilifu, lakini kumebaki sehemu furani ya kukua (Mathayo 5:48) Petero anasema haya "…… kama watoto wa kutii msijifananishe na

tamaa zenu za kwanza, za ujinga wenu, bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi wenu wote, kwa maana imeandikwa, mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu." (1 Petero 1:14-16)

Kitambo kidogo kabla ya wana wa Israeli kuingia inchi ya ahadi kanaani, Yoshua aliwahutubia watu…. "Basi Yoshua akawaita hao watu kumi na wawili, aliokuwa amewaweka tayari tangu hapo, katika wana wa Israeli, kila kabila mtu mmoja, naye Yoshua akawaambia, haya piteni ninyi mtangulie mbele ya sanduku la Bwana, Mungu wenu, mwende pale katikati ya Yorodani, mkatwae kila mtu wenu jiwe moja begani mwake, kwa kadiri ya hesabu ya kabila za wana wa Israeli", (Yoshua 4:4,5). Dalili za yakati zinaonyesha vyema kuwa Yesu Kristo, mwokozi wa ulimwengu, hivi karibuni atakuja ulimwengu. Tumefika sasa mpaka-ni ya kuingia kanaani ya mbinguni, na tunaomba kwa haraka sana tujitakase, kwa kuwa tunaenda kukutana na Bwana wa mabwana na mfalme wa wafalme.

Sisi hatuwezi kujitakasa sisi wenyewe walakini kwa kujipeana kwa Mungu kila siku, na Roho mtakatifu kuwa anafanya kazi ndani yetu na kutuwezesha kuishi maisha yalio lingana na mapenzi ya Mungu- wazi kabisa ni lazima tuwe na roho safi ndiposa tuweze kumwona Mungu. Petero anaandika, "lakini, kama ilivyo ahadi yake, mnatazamia mbingu mpya na nchi mpya, ambayo haki yakaa ndani yake." (2 Petero 3:13-14). Mahubiri katika mlima wa mizeituni, Yesu anasema, "Heri wenye moyo safi, maana hao watamwona Mungu." (Mathayo 5:8)

Kwa hivyo, kabla ya Yesu kurudi mara ya pili, ni lazima tupitie pambano na vita kubwa. Bila shaka tuko vitani, walakini ni vita vya kiroho. Ni vita kati ya mwili na Roho, kati ya shetani na Mungu, vita ya kumawazo na kiroho huifanya hii vita kuwa wazi. Bibilia inafafanua mapambano hayo hivi;

1. Maana ingawa tunaendelea katika mwili, hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili;(maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome;) tukiangusha mawazo na kile kitu kilichoinuka, kujiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo.(2 Korintho 10:3-5)

2. Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga zile za shetani. Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama. Basi simameni, hali mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani, na kufungiwa miguu utayari tupatao kwa injili ya amani, zaidi ya yote mkiitwa ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwuovu, tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa roho ambao ni neno la Mungu; kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote, (waeteso 6:11-18)

3. "Joka akamkasirikia yule mwanamke, akaenda zake afanye vita juu ya wazao wake waliosalia, wazishikao amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu;(Rev 12:17)

4. Tabia ya wafuasi wa Mungu-ambao ni kama tu wengine wote watalazimishwa kuipokea chapa ya mnyama katika siku hizi za Mwisho hapa ndipo penye subira ya watakatifu, hao wazishikao amri za Mungu, na imani ya Yesu. (Ufunuo 14:12)

5. Katika kitabu cha mwisho wa Biblilia, Ufunuo, Yohana aliona katika jonzi ushindi wa watu wengi tena nikaona kitu kama mfano wa bahari ya kioo iliyochangamana na moto, na wale wenye kushinda, watokao kwa yule mnyama, na sanamu yake, na wamesimama kando-kando ya hiyo bahari ya kioo, wenye vinubi vya Mungu." (Ufunuo 15:2)

6. Biblia inaeleza hali itakavyo kuwa wakati wa mwisho katika kundi hili kisha nikaona, na tazama huyo mwana-kondoo amesimama juu ya mlima sayuni, na watu mia na arobaini na nne elfu pamoja naye, wenye jina lake na jina la Baba yake limeandikwa katika vipaji vya nyuso zao. Nami nikasikia sauti mbinguni kama sauti ya maji mengi, na kama sauti ya radi kuu. Na hiyo sauti niliyoisikia ilikuwa kama sauti ya wapiga vinubi, wakavipiga vinubi vyao; na kuimba wimbo mpya mbele ya kile kiti cha enzi, na mbele ya wale wenye uhai wane, na walewazee; wale hapana mtu aliyeweza kujifunza wimbo ule, ila wale mia na arobaini na nne elfu, walionunuliwa katika neti. Hawa ndio wasiotiwa unajisi pamoja na wanawake, kwa maana ni birika. Hawa ndio wamfuatao mwana-kondoo. Na katika vinywa vyao haukuonekana uongo. Maana hawana mawaa. Bibilia tena inasema watakao faulu ni hao wazishikao amri za Mungu, na imani ya Yesu.(Ufunuo 14:12)

Kwa uwazi kabisa,basi Masalio ya watu wa Mungu wataokolewa (Isaya10:20-2,Mika 2: 12 Ufunuo 12 :17 Warumi 11 :5 Warumi 9:27)Basi Biblia yasema wazi eti ni wale tu watakao shinda wale watakao zishika amri za ungu na imani ya Yesu( Ufunuo 12: 14) Kwa hivyo swali la kuchunguza moyo ni hili,, Kwa uwezo wa neema ya Yesu. Je, utatunza amri za mungu na imani ya yesu? Wokovu ni jambo lako binafsi. Tutapotea au kuokoleawa kibinafsi si kama kundi au makanisa. Isipokuwa umeyapeana maisha yako kabisa kwa Mwito wa Yesu ni huu:

Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakuwa pamoja naye, na yeye pamoja nami. Yeye ashindaye, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi (Ufunuo 3:20-21)

Basi sasa, unakawilia nini? Simama, ubatizwe, ukaoshe dhambi zako, ukiliitia jina lake. (matendo 22:16)

Si katika siku hiyo watasema, tazama, huyu ndiye Mungu wetu, ndiye tuliyemngojea atusaidie; huyu ndiye BWANA tuliyemngoja, na tushangilie na kuufurahia wokovu wake. (Isaiya 25:4)

UWE SHAHIDI MTENDAJI

Tukishagudua jinsi Yesu amefanya "kutuokoa NA TUMESHA ISHIA MAISHA YAKE TUTATAKA TUSHIRIKI SANA FURAHA pamoja na habari njema na wengine pia mwajiri wetu Yesu Kristo asema hivi :

Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. Basi enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na mwana na roho mtakatifu, na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari. (Mathayo 28:18-20)

Pia tume hizwa sana tuupeleke ujumbe wa wokovu kwa wale tunaokutana naoYesu mwenyewe ni nuru ya dunia (Yohana 8:12)huelezea jambo hili zaidi:

Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji hauwezi kusitirika ukiwa juu ya mlima. Wala watu hawawashi taa na kuiweka chini ya pishi, bali juu ya kiango, nayo yawaongoza wote waliomo nyumbani. Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni. (Mathayo 5:14-16)

Kwa sababu tunaishi nyakati za mwisho. Tuko na ujumbe wa kipekee kwa wanadamu. Tunapata ujumbe huu katika kitabu cha ufunuo 14:6-12) na fungu la 18, mstari wa nne. Ni ujumbe wa wokovu na onyo ambalo litajulikana duniani na watu wote. Ujumbe wa siku zetu. Mungu atahakikisha utaenda kote, na wengi ambao wamepata upendo wake Kristo tayari wanaendelea kueneza ujumbe huu kupitia kwa redio, runinga(Tv), video, fazi, utandawazi, ujumbe wa simu tangatangi, CDs, gasseti, vitabu, vijitabu na makaratasi, mahumbiri ya wazi barabarani, na pia mikutano mingi ya aina yeyote. Kunao kazi inayoendelezwa na kundi maalum, na hakuna awezaye kuwasimamisha. Wewe utahakikisha eti umejiunga nalo, kwa kuwa wako na mwamusho mkubwa na wako tayari kumfanyia Bwana kazi. Zaidi ya yote Mungu atampa Roho wake kwa wanaomtii. (Mitume 5:32) kulingana na Bibilia, kazi itamalizika kwa haraka sana (Warumi 9:28), kama vile uchungu umjiavyo mwenye mimba. (Wathesalonike 5:3). Tumefikia kiwango Fulani, tukiona ushahidi kwamba kazi inaendelea kumalizika, mbele ya machoni petu. Walakini tusije tukawasahau watu wa kawaida wanao fanya kazi ya maana sana. Wao ndio huwatembelea watu nyumba kwa nyumba, au kufanya mikutano majumbani na kufikia kwenye utangazaji haufiki. Itakuwa ni vyema kama wenye kuupeleka ujumbe huu na onyo hili kwa wengine. Lakini ni sasa tunatakiwa kuwa wenye bidii. Udhihirishe eti unawajali wengine. Onyesha wazi kuwa eti utawasaidia wengine waweze kuepuka ufalme wa giza, hadi kwenye matarajio, kuwa na maisha ya baandaye mema, na uzima wa milele. Hebu na Mungu aende pamoja nawe!.

Ni mimi wako Mpendwa Abel and Bente Strusknes


[Back to the Main Page!]


This page belongs to Abel Struksnes. For more information contact Christian Information Service, Bente & Abel Struksnes, Vestrumsbygda 26, 2879 Odnes, Norway or send me an e-mail at abels@online.no