[Back to the Main Page!]

VIZUKA VYA MARIAMU
Je, ni ufunuo wa kiungu kwa kizazi cha mwisho au ni ulaghai ulio mkuu?

Leo hii maelfu ya watu wana safiri kuelekea Fatima (Ureno), ambapo kiumbe fulani kinacho semekana kuwa ndiye bikira mariamu, hujidhihirisha. Kiumbe hiki pia kimejidhihirisha katika sehemu zingine mbali mbali duniani. Watu wamekuwa wakikiita kiumbe hiki kwenye maombi yao, na mara kwa mara huyu "Mariamu" huwaongelesha, huku akiwapasha jumbe fulani…

"Mariamu" hujielezea kuwa nabii wa nyakati za mwisho katika kanisa la mwisho la masalio wa Mungu, huku akiwa ametumwa na Bwana kuutoa mwongozo wa kipekee kwa kanisa hilo lake katika siku hizi za mwisho. Tena husemekana kuwa yeye, kama mpatanishi wetu, humpelekea Mungu maombi ya watu wake, kwa hivyo yeye huchukuliwa kama mpatanishi kati ya Mungu na binadamu, hasa miogoni mwa wakatoliki.

"Mariamu" pia hubainisha kuwa maafa makubwa pamoja na adhabu nyingi zitauangukia ulimwengu, kwa mujibu wa nyakati ngumu zijazo. Yeye huwahimiza wafuasi wake kujificha chini ya ulinzi wake. Husema, "Huu ndio wakati wa kila mmoja kujificha ndani yangu, kwani mimi ndiye safina ya Agano Jipya".

Pia yeye hupasha ujumbe na unabii unaohusu siku zijazo, na kutuuliza tuyafuate mashauri yake, "Mimi nawafunulia kitabu kilichotiwa muhuri" asema, "ili siri iliyofichwa ndani ya kitabu hiki ifichuliwe".1

Msimamo wetu utakuwa upi?

Misemo hii kuhusu "Mariamu" ni ya kuogofya kweli! Lakini msimamo wetu sisi utakuwa ni gani pale tutakapokabiliana na maono haya? Je, hizi ndizo jumbe ambazo Bwana angetaka kukiarifu kizazi cha mwisho, ama huu ni uzushi tu ili kuupotoa ukweli?

Hebu tuigeukie Biblia, kwani hapa twauzungumzia ufunuo unaodaiwa kuwa watoka kwa Bwana. Bila shaka Mungu ana jambo la kusema kulihusu swala hili. Biblia yafunua waziwazi kuwa manabii wa uongo na pia wa ukweli watakuja siku za mwisho, hivyo basi twaulizwa kuigeukia "Sheria na ushuhuda" ili tuweze kuelewa ni yapi yaliyo ya ukweli, na yaliyo makosa. "Ndiposa kwa matunda yao mtawatambua", Biblia husema,"Msiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu".2

Kuna vipengele viwili muhimu ambavyo tutajaribu kuvichunguza, huku tukivithibitisha kwa neno la Mungu:

1. Je, huyo anayefunuliwa ni Mariamu mama ya Yesu kwa hakika? Je, bikira Mariamu amekufa au bado you hai?

2. Je, jumbe zake zaambatana na neno la Mungu?

Je, bikira Mariamu amekufa ama yu hai?

Hebu na tulichunguze swali letu la kwanza: Je, Biblia yasema chochote kuhusu kile kinachotendeka wakati mtu akifa? Hebu tuyapitie mafungu kadhaa kwa kifupi kutoka kwenye maandiko matakatifu:

"Kwa sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa, lakini wafu hawajui neno lolote, wala hawana ajira tena; maana kumbukumbu lao limesahauliwa… chochote mkono wako ukipatacho cha kufanya, kifanye kwa nguvu zako zote; maana uendako kaburini hakuna kazi, wala mbinu, wala ujuzi, wala hekima"

"Msiwatumainie wakuu wala mwana wa adamu, ambaye hakuna msaada kwake pumzi yake hutoka, huurudia udongo wake, siku hiyo mawazo yake hutoweka".

"Watu hawamsifu Bwana, naam wale wateremkao kwenye kimya. Basi sisi tutamsifu Bwana tangu wakati huu kuendelea hadi milele"3

Yapo mafungu mengine, hata hivyo Biblia tayari imeshatupatia picha safi, ukweli kwamba watu wakifa, hawaendi mbingini, wala kuzimu, bali wako makaburini mwao, huku wakigeuka kuwa udongo kwa taratibu. Mariamu pia alikuwa ni mwanadamu, hivyo basi hayo yalimpata pia : "wafu hawamsifu Bwana..."

Kwanza kabisa wakati wa ufufuo, ambao Biblia yatuarifu kuwa utafanyika kuambatana na kurudi kwa Kristo, wale waliomfuata Bwana kwa uaminifu watafufuliwa toka makaburini mwao na kuingia kwenye uzima wa milele. Biblia yaelezea hivi:

"Kwa kuwa twawaambieni haya kwa neno la Bwana, kwamba sisi tulio hai, tutakaosalia wakati wa kuja kwake Bwana, hakika hatutawatangulia wao waliokwisha kulala mauti. Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu, nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani, na hivyo tutakuwa pamoja n aBwana milele.4

Mizimu

Tukishauelewa ukweli huu, Biblia yatuonya vikali dhidi ya viumbe ambavyo hujitokeza kwa mfano wa watu walioaga dunia. Maonyesho haya huitwa imani ya mizimu, ambayo hujumuisha mafundisho ya kuwa nafsi haiwezi kufariki. Biblia imetupa shauri hili: "asipatikane kati yenu yeyote ambaye…. Ni mchawi, au awasilianaye na mapepo, wala mlozi, wala mwenye kukata kauli kwa mizimu na pepo au kutoka kwa wafu. Maana yeyote atendaye mambo haya ni chukizo kwa mwenyezi Mungu.5

Katika Biblia pia, tunao mfano jinsi yule mwovu hujidhihirisha kama mfu. Tunawaza kuhusu ule wakati ambapo sauli alikuwa akipigana vita na wafilisti. Alikuwa kamwacha Mungu, na kuenda kwa mchawi ili apate habari kuhusu matokeo ya vita hivyo. Sauli alifahamu kuwa ni haramu kumtembelea mlozi, lakini alikuwa katika hali ya kuata tamaa, kwa hivyo haidhuru alienda kumtembelea, huku amejivika mavazi ya kujigeuza. Kwa kulitii neno la huyo mchawi, yule mwovu alitokezea katika umbo la nabii Samueli, ambaye alikuwa kafariki miaka kadhaa kabla ya tukio hili. Kisha sanamu hii, iliyofanana na Samueli, iliuleta ujumbe kuhusu vita hivyo.3

Vivyo hivyo yule mwovu hata siku hizi hujidhihirisha kwa mfano wa watu waliofariki. Kwa hakika huwa ni ibilisi au malaika wake ambao huiga "Mariamu". Na habariwaziletazo zitaukaribia ukweli kiasi kwamba ni wale tu wanaoyafahamu maandiko, na walio na Roho Mtakatifu kama kiongozi wao, watakaoweza kutambua yaliyo ya kweli na yalio makosa.

Maandiko yasema kuwa siku za mwisho, shetani atafanya kazi kwa ari "kwa uweza wote na ishara na miujiza ya udanganyifu",6 kwa hivyo twaweza kuvitarajia vivuli zaidi vya "Mariamu" nyakati zijazo, na kwa huzuni twaona halaiki ya watu waliodanganyika (na pia watakaondanganyika siku zijazo), ambao wamenaswa na maonyesho haya ya pepo. Ulinzi wa kipekee dhidi ya udanganyifu huu unasao ni kushikamana na baba wetu wa mbinguni kwa ukaribu na ukweli, hali kadhalika kulifahamu neno la Mungu kwa undani.

Udanganyifu ulio mkuu zaidi?

Kila mara shetani atakuwa akijaribu kuiga unabii wa Biblia. Biblia husema waziwazi kuwa "shetani mwenyewe hujibadili na kuwa malaika wa nuru", na ya kwamba watatokea manabii wa uongo.6 Shetani afahamu vyema kuwa Yesu atarudi, na kama vile yeye (shetani) aonyeshavyo vivuli bandia vya Mariamu, vivyo hivyo ataiga kurudi kwa Kristo mara ya pili. Huu utakuwa ni udanganyfu sugu. Mwongo huyo atafanya iaminike kuwa Kristo tayari amerudi duniani. "Katika sehemu mbali mbali za dunia shetani atajidhihirisha miongoni mwa wanadamu kama kiumbe jalali kitoacho mwanga mwingi wa kupofusha, huku umbo lake likifanana na maelezo yaliyotolewa na Yohana kwenye kitabu cha Ufunuo kuhusu mwana wa Mungu.7 Nuru inayo mzingira yazidi nuru nyingine yoyote ambayo macho ya binadamu yamewahi kushuhudia. Mayowe ya ushindi yajaa hewani; "Kristo amewasili! Kristo amewasili!"

Watu wajiangusha kifudifudi mbele zake ili kusujudu, huku naye akiinua mikono yake na kuwatangazia mibaraka, kama vile Kristo alivyo wabariki wafuasi wake alipokuwa duniani. Sauti yake ni nyororo na iliyopimwa, inayosikika kama wimbo. Kwa sauti yenye upole na upendo mwingi, huhubiri baadhi ya ule ukweli wa mbingu, wenye neema, alioutamka mwokozi; huponya pia magonjwaa ya watu na kisha, huku akijitwwatia tabia ya Kristo, hudai kuwa aliibadilisha sabato akaifanya kuwa Jumapili, na kuwaamrisha watu wote waitakase siku hiyo aliyoibariki, hutangaza kuwa wale wanaoendelea kuitakasa siku ya saba wanalikufuru jina lake, kwani wanakataa kuwasikiza malaika waliotumwa kuleta nuru na ukweli.

Huu ndio udanganyifu wenye nguvu na unaokaribia kutawala kabisa. Kama wasamalia walio hadaiwa na Simon Magus, umati utaupokea uchawi huu kuanzia mdogo hadi mkubwa, huku wakisema: huu ni "uweza mkuu wa Mungu".7 Lakini watu wa Mungu hawatapotoshwa. Mafundisho ya huyu Kristo bandia hayaambatani na Biblia. Huyo atawatangazia baraka wale wanaomsujudu mnyama na sanamu yake, japokuwa hawa ndio wale wale watu ambao Biblia yatangaza kuwa wata mwagiwa divai ya ghadhabu zake Mungu isiyo changanywa na maji.

Isitoshe, shetani hana ruhusa ya kuiga namna ya kurudi kwa Kristo. Mwokozi aliwaonya watu wake dhidi ya udanganyifu kuhusu swala hili, na ametabiri kwa njia ya wazi kabiza kuhusu namna ya kurudi kwake mara ya pili. " Maana watatokea kina Kristo wa uongo na manabii wa uongo. Watafanya ishara kubwa na maajabu ya kuweza kuwapotosha ikiwezekana hata wateule wa Mungu… Basi, wakiwaambieni, `Tazameni, yuko jangwani; msiende huko; au `Tazameni, amejificha ndani,' msisandiki; maana, kama jile umeme uangazavyo toka mashariki hadi magharibi, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake mwana wa Mtu".6 Kuja kwa namna hii hakuna awezaye kuiga.

Ulimwengu mzima utajua na dunia yote itashuhudia

Ni wale tu wanafunzi wa maandiko waliomakinika na walio pokeakule kuupenda ukweli ambao wataepukana na udanganyifu huu ulio na uwezo mkuu kiasi cha kuushika ulimwengu mateka. Kupitia kwa ushuhuda wa Biblia, hawa watamtambua yule mdanganyifu akiwa amejivika mavazi yake ya kujificha.

Wote watafikiwa na wakati huu wa kujaribiwa. Kupitia kwenye kichungio hiki cha majaribu, Mkristo wa kweli atafunuliwa. Je, wakati huu watu wa Mungu watasimama imara juu ya neno lake kiasi kuwa hawawezi kuufuata ushahidi utokanao na hisia zao? Je, waufikiapo upeo wa mgogoro kama huo, wataweza kushikamana na Biblia, naam, Biblia pekee? Kama ikiwezekana, shetani atawazuilia ili wasipate kujiandaa kamili ili kusimama imara siku hiyo.

Atafanya mpango kabambe ili kuwafungia njia, kuwatega kwa kutumia mali za dunia hii, na kuwabebesha mizigo mizito yenye kuchosha mno, ili nyoyo zao zimilikiwe na shughuli za maisha haya, nayo siku hiyo ya kujaribiwa iwafikie kama mwizi" (Dondoo hili la kuvutia limetolewa kwenye kitabu kiitwacho "Vita Kuu," ambacho tutakitangaza mwisho wa ukurasa huu. Jitwalie kitabu hicho bila malipo, ili ukasome zaidi kuhusu vita hivyo vikuu!).

Kwa hakika twahitaji kujihadhari mno dhidi ya udanganyifu huu mkuu, ili nasi tusije tukanaswa. Biblia yasema kuwa "kama ikiwezekana, watawadanganya wateule pia". Kwa hivyo, tungependa kusizitiza jambo moja kuhusu pambano hili, ili tuupate ufahamu kamili ambao utatuwezesha kuivumilia mitego ya ibilisi.

Kristo atakaporundi ili kuwapeleka watu wake nyumbani hivi karibuni, nyayo zake hazitaikanyaga ardhi hii. Tulisema hapo awali ya kuwa wateule watachukuliwa mawinguni ili waende na Yesu mbinguni. Kabla ya kupaa mbinguni,4 Yesu alisema, "na kama nikienda kuwaandalia makao, basi nitarudi tena, niwapokee kwangu; ili nilipo, nanyi muwepo". Ni baada tu ya miaka 1000 (muda ambao wateule watakaa mbinguni) ambapo Yesu ataikanyaga ardhi tena, nao ndio wakati ambapo nyayo za Yesu zitaukanyaga mlima wa Mizetuni, mahali ambapo Yerusalemu mpya itasimamishwa. Hapo ndipo atakapo umba "mbingu mpya na ulimwengu mpya" zililizojaa haki.8

Muhuri wa mungu au alama ya mnyama?

Mafundisho ya "Mariamu" yanao ukweli mwingi lakini ukweli huu mara kwa mara huchanganywa na uongo, jambo ambalo hufanya kazi ya kuufichua udanganyifu huu kuwa kibarua kigumu. Ukweli wote uliopo ndani ya jumbe zake, pamoja na kule kule kujionyesha kwake kwa ajabu, hali kadhalika ile hali yake ya kipekee inayoashiria wema wake, yote haya yahitaji mtu awe na imani. Bila shaka ibilisi ataigeuza imani hii ili kujinufaisha mwenyewe, na hapo atayatanguliza mafundisho ya asili ya kikatoliki. Mojawapo ya mafundisho haya ambayo papa aliyopo sasa huyapendekeza hasa katika ile barua ya uchungaji "Dies Domini", Mai 31, 1998 ni kuhusu Jumapili kama siku ya kustarehe badala ya sabato, ambayo ndiyo siku ya saba kulingana na Biblia.

Yafaa ifahamike kwa watu wote ya kuwa upapa ndio uliozibadilisha amri za Mungu (katika katekisimu) hivi kwamba kwa njia nyingi, zimekuwa tofauti na zile amri kumi za Mungu kama zinavyopatikana kwenye kitabu cha kutoka 20:3-17. Biblia yasema kuwa twafaa kuitunza siku ya saba, yaani sabato, kama siku ya kustarehe. Pia husema kuwa Mungu ameibariki sikuhiyo na kuitakasa. Katika katekisimu husema tu: " I kumbuke siku takatifu ya sabato ukaitunze". Hivyo basi husema kuwa kanisa liliuhamisha utakatifu wa sabato hadi siku ya kwanza ya juma, ambayo ni Jumapili.19 Alama zote za kutambulisha ndani ya Biblia kuhusu mnyama "huingiana na upapa na kama tulivyo kwisha kuona, upapa husema kuwa wanayo alama fulani ya mamlaka yao; ambayo ni Jumapili kama siku ya kustarehe badala ya sabato. Kwa hivyo kuitunza Jumapili ndiyo alama ya upapa yaani "alama ya mnyama". Tukiitazama jambo hili kulingana na unabii wa Biblia, twafunuliwa waziwazi kuwa alama ya mnyama itasimamishwa kama jaribio mnamo siku za mwisho wa historia ya dunia hii. Biblia yasema kuwa wale watakaokataa kuipokea alama ya mnyama hawataruhusiwa kununua wala kuuza, na hatimaye watakabiliana na hukumu ya kifo ni katika kilele cha pambano hili ambapo yesu atarudi tena ili kuwaokoa watu wake.

Je, twafaa kumwabudu Mariamu"?

Tunapoitazama misemo ya "Mariamu" tuliyoitaja hapo awali huwa ni jambo la kuogofya tuonapo jinsi yeye anavyojiinua, na jinsi anavyo yavuta macho ya watu kijielekeza. Ule mwito wakujificha ndani yake na kumsujudu umeitikiwa na watu wengi. Wamezigeukia sanamu za bikira "Mariamu" ili kutafuta neema, na pia kumuliza awaombee kwa mwana na baba. Mara tu baada ya lile jaribio la kumwua papa Yohana Paulo wa pili, yeye alienda moja kwa moja hadi Fatima mnamo tarehe 2 Mai, 1982, na kuabudu mbele ya sanamu ya bikira Mariamu, huku akimshukuru kwa kuulinda uhai wake.

Ni jambo la huzuni kuona kuwa viongozi wa dunia wanawapasha watu ishara za udanganyifu, ambazo huwaelekeza watu mbali na ukweli wa Mungu. Sasa, tutadondoa sehemu kadhaa toka kwenye amri ya pili ya Biblia, ambazo kanisa katoliki imeondoa kulingana na katekisimu udanganyifu ambao tayari umekubalika miongoni mwa waprotestanti: "usijifanyie sanamu ya miungu wa uongo, au majini chini ya dunia… usiisujudie wala kuitumikia…"9 Japokuwa Biblia imeelezea hapa waziwazi, bado twamuona papa na wenzake wakingeukia "Mariamu" na sanamu za "Mariamu"

Je, "Mariamu" atakuwa mwokozi na mpatanishi wetu?

Wakatoliki pia wameanzisha kampeni kabambe, huku wakiitangaza imani mpya katika kanisa hilo la katoliki: kutangaza kuwa Mariamu ni mshiriki katika kuokoa, na pia ni mpatanishi katika neema yote, hali kadhalika ni mtetezi wa watu wa Mungu.10

Tukishaelewa hivi, tutaweza kuona waziwazi ya kwamba kunazo harakati ndani ya kanisa katoliki za kujaribu kumwinua "Mariamu" hadi pale atakapofikia kiwango sawa na Yesu Kristo. Kwa mujibu wa Biblia, "wapo watatu wanaoshuhudia huko mbinguni, yaani Baba, Neno (Kristo) na Roho Mtakatifu"11 ni mshrikishi katika kuokoa, na kuwa yeye ni mpatanishi. Basi yamaanisha kwamba hawa watatu wataongezeka na kuwa wanne, yaani Baba, Mama, Mwana na Roho. Wakati ambapo wakatoliki wanampa "Mariamu" cheo hiki cha mshrikishi katika kuokoa na mpatanishi apelekaye maombi kwa Mungu, pia mtetezi na kimbilio, huo huwa ni udanganyifu mkuu, na pia ni jaribio la kutwaa cheo cha Yesu Kristo kwa ujanja na ujasili! Yesu mwenyewe hulikataa waziwazi wazo la aina hiyo pale asemapo. "Mimi ndiye njia, ukweli a uzima: mtu haji kwa Baba ila kwa njia yangu mimi"11 Twaambiwa pia sababu iliyomfanya Yesu kuyasema haya. Ni kwa sababu kifo chake Yesu kiliifungua njia ifikayo kwenye kiti cha Mungu. Dhambi humtenganisha binadamu na Mungu, na wakati binadamu alipoasi, alihukumiwa kufa, kwani "Mshahara wa dhambi ni mauti". Lakini Mungu ameitenganiza njia ya kuepukana na haya: "kwa maana jinsi hii Mingu aliupenda ulimwengu, akamtoa mwana wake wa pekee, ili yeyote amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.11 "Tukimchagua Yesu kuwa kiongozi wa maisha yetu, atajitwalia dhambi zetu juu yake kwa mujibu wa kafara aliyoitoa, kwa hivyo maneno yafuatayo yameandikwa kwenye kitabu cha 1 Timotheo 2:5 "maana yuko Mungu mmoja, na pia yuko mmoja anayewapatanisha watu na Mungu, binadamu Yesu Kristo". Kwa hivyo ni kupitia tu kwa Yesu Kristo, ambaye ni mpatanishi kati ya Baba na Watu, ambapo twaweza kukifikia kiti cha enzi cha Mungu.11

Je, "Mariamu", au Papa, au makuhani, waweza kusamehe dhambi?

Kanisa katoliki pamoja na Papa, ambao wanataka kumwinua "Mariamu", pia hufundisha kuwa Papa na makuhani waweza kuwasamehe watu dhambi. Hali kadhalika katika baadhi ya madhehebu ya kiprotestanti na dini zingine kama vile Freemasons imeruhusiwa mtu kumwendea kuhani ili kuungama, na baada ya kuungama dhambi mtu huambiwa: dhambi zako zimesamehewa.

Huku tukiuchunguza mtindo huu, swali muhimu la kuuliza ni hili: Je, tutawaendea "Mariamu", Papa na makuhani (binadamu walioanguka na wafao), au tutamwendea Yesu Kristo ili kuupokea msamaha wa dhambi? Biblia hudhihirisha wazi kuwa dhambi ikitendeka, wale wanaohusika wapaswa kulisuluhisha kosa hilo wao kwa wao. Husema hivi: "Jihadharini: ndugu yako akikukosea, mkemee; akitubu umsamehe".12 Kuhani au Papa hana jukumu lolote la moja kwa moja katika kesi kama hii. Mambo yakishasuluhishwa kwa wale walio kosewa, yapasa kumwendea bwana katika sala ili kupata msamaha wa dhambi. Yesu atuambia tumwombe Baba wetu wa mbinguni hivi: " Tusamehe makosa yetu, kama nasi tunavyowasamehe walio tukosea"12 Naye Yohana ayasema maneno haya namna hii: " "Watoto wangu, ninawaandikieni mambo haya, kusudi msitende dhambi. Lakini ikijatokea mtu akatenda dhambi, tunaye mmoja ambaye hutuombea kwa Baba, ndiye Yesu Kristo aliye mwadilifu kabisa.12 "Ni kupitia kwa Yesu tu ambapo mwenye dhambi anaweza kusamehewa na kukifikia kiticha enzi cha Mungu. Yesu pekee ndiye mwokozi wetu, mpatanishi wetu na mtetezi wetu.

Ni kwake yeye ambapo yatupasa kuzipeleka dhambi zetu.

Tukishazikubali dhambi zetu, tukishazitubu na kumgeukia ili kuupata msamaha wa dhambi, basi hapo hutupatia ahadi hii "Tukiziungama dhambi zetu, basi, Mungu ni mwaminifu na mwadilifu, naye atatusamehe dhambi zetu na kututakasa uovu wote"

Mizimu ufunguo muhimu katika jaribio la kuukusanya ulimwengu

Hebu na tulirudie swala la "Mizuka ya Mariamu", au maonyesho ya mizimu. Kuwasiliana na mizimu bila shaka utakuwa ni ufunguo muhimu katika jaribio la kuzikusanya dini zote za dunia mnamo siku za mwisho. Biblia yashuhudia jambo hili pale isemapo; "kisha, nikaona pepo wabaya watatu walio kama vyura, wakitoka kinywani mwa yule joka (shetani, pepo) kinywani mwa yule mnyama (kanisa katoliki) na kinywani mwa yule nabii wa uongo (waprotestanti walioasi). Hawa ndio roho za pepo wafanyao miujiza. Ndio wanaokwenda kwa wafalme wa ulimwengu wote na kuwakusanya pamoja kwa ajili ya vita kuu siku ile ya Mungu mwenye nguvu".13 Leo hii twaona jinsi njia inatayarishwa ili kuutimiza unabii huu. Mataifa ya dunia yana yaunganisha nguvu zao za kisiasa, kiuchumi, kijeshi na katika mbinu za shetani za kuukamilisha mkusanyiko huu- hasa kidini. Biblia yatuambia kuwa nguvu zote potovu za dunia zitaunganika pamoja nyakati za mwisho. Imeelezea kuwa hawa watakuwa na nia moja, na watamkabidhi mnyama uwezo na nguvu zao. Ni dhahiri kwamba upapa ndio utakaoongoza katika pambano hili. Ndiyo, Biblia yasema kuwa dunia yote itamstaajabia huyo mnyama (yaani upapa).13 Biblia yaendelea kusema kuwa nguvu hizi ndizo zitakazofanya vita dhidi ya mwana kondoo na wafuasi wake. Nguvu za dunia hii zitajipanga kama watawala wanaostahili kutiiwa zaidi ya Biblia, lakini Biblia yasema, "Usimwamini binadamu, uhai wake haudumu kama pumzi. Yeye anafaa kitu gani?" Na pia: "Mwenyezi mungu asema hivi: alaaniwe mtu anayemtegemea binadamu, mtu ambaye anategemea nguvu za binadamu, mtu ambaye moyo wake umeniacha mimi mwenyezi Mungu".14

Baada ya yote hayo tiliyoyachunguza kufikia sasa, ni dhahiri kwamba "Mariamu" atakuwa na jukumu kubwa katika jaribio hili linaloendelea la kuzikusanya dini zote chini ya paa la Kirumi. Papa pia amedhihirisha jinsi anavyoutamani muungano huu: "Mwaka wa

2000 utasherehekewa kama jubilii kuu, ambayo lengo lake la mwisho ni umoja wa Wakristo wote, hadi walifikie lengo lao, ambalo ni kuwa na jamii kamili.15

Jinsi ya kuafikia umoja wa kweli

Umoja wa kweli haupatikani kupitia kwenye ukatoliki, au kwenye kuviamini "vizuka vya Mariamu" au kwenye kura za muungano wa dini. Umoja wa kweli hupatikana tu pale tusemapo ndiyo kwa yesu kristo na njia yake ya kutuokoa kutoka dhambini. Yesu Kristo asema: naomba "ili wote wawe kitu kimoja. Baba! Naomba wawe ndani yako, ili wawe ili wawe kitu kimoja ndani yetu..." Mara tu tukisema ndiyo kwa yesu, na kumkubalia Roho kuingia ndani ya mioyo yetu, basi hapo msingi wa ule umoja wa kweli huimarishwa. Kisha tutazipokea nguvu zinazohitajika ili kuyatenda mapenzi ya mungu. na maisha yetu pia yataambatana na mapenzi ya mungu. Tabia ya mungu itadhihirika maishani mwetu, sio kwa sababu sisi wenyewe niwema, bali ni kwa sababu Roho mtakatifu hutujaza na nguvu, Pamoja na uwezo wakupambanua unohitajika katika kufanya uamuzi bora wakati wa kutoa maneno, pia matendo, tuendeleapo na maisha ya kila siku.17

Biblia husimulia kuhusu masalio fulani wachache ambao watabaki waaminifu hadi mwisho. Hawa ni wale "washikao amri za mungu, na imani ya Yesu".18 Tukishazikubali dhabi zetu na kupokea msamaha na wokovu wa Yesu, basi hapa twajua kuwa tutazipokea nguvu zote zinazohitajika ili kuendelea kuwa wafuasi waaminifu wa Yesu. Watu wengine hata wataipokea neema inayotosha kuwawezesha kuishi hadi kurudi kwa Kristo.18 Ni ujuzi wa kufurahisha kiasi gani watakaokuwa nao hawa wakiwa pamoja na Kristo! Naomba sisi sote tujitahidi kusimama imara tukiwa upande wa Kristo hadi mwisho.

Twaweza kufanya nini?

Kwako wewe ambaye bado haujafanya uamuzi kamili wa kumfuata yesu, nasema hivi: Itwae Biblia yako na ukaisome. Mwulize Bwana abariki kusoma huko kwako, kisha uanze, kwa mfano, kwa kuzisoma barua zote za Yohana, yule mwanafunzi aliyependwa sana na Kristo, na hapo utaweza kumfahamu Yesu Kristo aliye mwokozi wa ulimwengu". Na uhai wa milele ndio huu: kukujua wewe uliye peke yako Mungu wa kweli, na kumjua Yesu Kristo uliyemtuma".18

Yesu Kristo, aliye mwokozi wa ulimwengu, yuarudi hivi karibuni! Ni tumaini lililonjema kiasi gani kwa siku za usoni! Ombi langu ni kwamba wewe nami tutakuwa na moyo wa kutaka kumfahamu Yesu, na kufanya urafiki naye SASA, ili tuweze kupaa pamoja naye hadi, kwenye makao yetu yaliyoko mbinguni palw ajapo kuwachukua watoto wake. Natarajia kukutana nawe huko!

Pokea salamu nyingi kutoka kwa Bente na Abel Struksnes


Vidondoo:
1. "Thunder of Justice" by Ted and Maureen Flynn.
2. Isaia 8:20; Mathayo 7:15-20; 1 Yohana 4:1
3. Mhubiri 9:5-6,10; Zaburi 146:3-4; aburi 115:17-18
4. 1 Wathesalonike 4:13-18; 1 Wakorintho 15:52-58; Ufunuo 1:7, Yohana 14:1-3
5. Kumbukumbu 18:10-12; 1 Samueli 28:3-20
6. 2 Wathesalonike 2:9; 2 Wakorintho 11:13-15; Mathayo 24:23-27
7. Ufunuo 1:13-15, Matendo 8:10; Ufunuo 14:9-11
8. Zekaria 14:4-9, Ufunuo 20 na 21
9. Kutoka 2:4-6
10. The Bulletin with Newsweek, Septemba 2,1997
11. 1 Yohana 5:7; Yohana 17:21-24 na 14:6; Roma 6:23, Wahibirania 8 na 9, Yohana 3:17
12. Luka 17:3-4, Mathayo 6:12, 1 Yohana 2:1-6, 1:9
13. Ufunuo 16:13-14; 13:3; 17:13-14
14. Isaia 2:22; Yeremia 17:5
15. "The Third Millenium", p.26-31
16. Yohana 17:20-23
17. Yohana 15:4-5; 2 Petero 1:4; 1 Yohana 1:9
18. Ufunuo 14:12; 1 Wakarintho 10:13; Wafilipi 4:12; Yohana 17:3
19. "Docrinal Catecism", p.147 na "The convert's Catecism of Catholic Doctrine" (1977ed.) p.50;"Catholic Record", Sept 1, 1923


[Back to the Main Page!]


This page belongs to Abel Struksnes. For more information contact Christian Information Service, Bente & Abel Struksnes, Vestrumsbygda 26, 2879 Odnes, Norway or send me an e-mail at abels@online.no